ATCL isiishie kwenye Dash8-Q400,ijifunze zaidi na haya mazuri kutoka RwandAir

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,820
We are excited to let you know that we are heading to Toulouse,France to bring our first A330 "Ubumwe" to the land of a thousand hills.

Tarehe 28/09/2016 Rwanda italeta moja kati ya ndege zake mbili mpya aina ya Airbus330(200 and 300 series) zitakazokuwa zikifanya safari zake kati ya Kigali na Asia na Ulaya.Moja ya ndege hilo wameipa jina "UBUMWE"

Ndege hizo A330-200 ina uwezo wa kubeba abiria 261 kwa wakati mmoja na nyingine A330-300 ina uwezo wa kubeba abiria 300 kwa wakati mmoja.

Rwanda itakuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kumiliki ndege aina ya A330-200/300.Ujio wa ndege hizo unafanya Rwanda kuwa na Dash8-Q400,Boeing,CRJ-900 ambazo zinasafairi sehemu mbalimbali za Afrika na Asia.

image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg

Hili ni "somo" kwa ATC toka RwandAir,ambao miaka kadhaa iliyopita waliqnza kwa kumiliki Dash8-Q400 na leo wanashusha A330-2/3 brand New.Sasa Rwanda anaenda kuwa mshindani mkubwa wa KQ ktk soko la usafiri wa anga Afrika ya Mashariki.Hii ni changamoto kwa ATCL inayofufuka toka ktk usingizi wa kutafunwa na "majizi" na "mafisadi" ambao kumbadili twiga tu wa nembo ya ATCl toka yule aliyesimama mpaka kuja yule aliyeinama iligharimu zaidi ya milioni 100,mchoro ambao angeweza kupewa kijana wa Fine Arts na akauchora.

ATCL iliyokuwa inaenda kushonesha uniform za Wahudumu wake Singapore na Malaysia na mtu anayeenda kusubiria kushoneshwa kwa nguo hizo anakaa huko miezi mitatu mpaka nguo zinakamilika,haiwezi kufikia hatua hii ya RwandAir kama upuuzi huo utaendelea.

Tuendelee kuitakia ATCL yaliyomema,ili kama vile "tulivyoshauriwa" kununua Dash8-Q400 na Rwanda,basi nasi tufuate nyayo na hatimaye miaka sita ijayo tuwe na "Ubumwe" yetu ya ATCL...Airbus 330/200
 
Duh, Kama utani vile? Hawa si ndio waliyumba yumba sana miaka ya 1994?

Mambo ambayo ilibidi tufanye sisi wanafanya wenzetu?

Hivi sisi tuna nini jamani? Roho inaniuma sana? Viongozi wetu tumewakosea nini mpaka mnatutenda nini?

Tumebaki kujisifia tu "kisiwa cha amani", "kisiwa cha amani", amani gani kutiana jaka la roho tu!
 
Yaani kuna muda ata Mungu anatushangaa yaani huyo twiga amekula milioni Mia yaani ata watoto wadogo ukiwaambia wachague mmoja watachagua Wa zamani kulikuwa Na humuhimu gani kubadilisha zaidi ya Kula ela tu
 
Duh, Kama utani vile? Hawa si ndio waliyumba yumba sana miaka ya 1994?

Mambo ambayo ilibidi tufanye sisi wanafanya wenzetu?

Hivi sisi tuna nini jamani? Roho inaniuma sana? Viongozi wetu tumewakosea nini mpaka mnatutenda nini?

Tumebaki kujisifia tu "kisiwa cha amani", "kisiwa cha amani", amani gani kutiana jaka la roho tu!
Tatizo tulilonalo sisi ni watu kama wewe; ambao mnajua nini kifanyike ama mnaona uchungu kwenye maendeleo lakini you don't step up and take responsibility.

Usipojiongeza na kuwania nafasi za uongozi na za maamuzi katika siasa, ukubali kuongozwa na akili ndogo.
 
Ha ha ha ha ha ha kat.ph kuna ukweli umeuongea hapo
 
Tatizo tulilonalo sisi ni watu kama wewe; ambao mnajua nini kifanyike ama mnaona uchungu kwenye maendeleo lakini you don't step up and take responsibility.

Usipojiongeza na kuwania nafasi za uongozi na za maamuzi katika siasa, ukubali kuongozwa na akili ndogo.
Uongozi wa Tanzania ni Mgumu! Ni fursa, ukiweka uzalendo mbele mauti yanakua nyuma yako thus why mimi binafsi sipendi, Ila inauma sana, hivi Mkuu kweli sisi ni wakupitwa kimaendeleo ya usafiri wa anga na Rwanda na Somalia kweli? Dah.. Hii nchi ingekua ni duka ningeshaifunga zamani sana.
 
Naona Rwanda imeamua kutuvua nguo kabisa
Kagame ni Mjanja sana. Ukikubali awe mshauri wako kua nae makini sana.. Anakwambia "hizi simu za Nokia za tochi ni ngumu sana, kwa wewe kutokana na mazingira ya kazi zako itadumu sana, unajua mimi mwenyewe natumia hizi hizi nokia za tochi tena six button kabisa ile, achana na masmartphone, hayadumu yatakufilisi tu, kila siku inataka bundle" na wewe ukamsikiliza then kesho yake unamkuta katulia beach anakula upepo mwanana na headphone masikion anakula mziki wa taratibu huku akiperuzi JF kupitia iphone7 yake mpya kabisa...

Maananinah..
 
Huku watu wanachonga sana kuhusu ATCL na wengine wala hawajui ndege ziko vipi.Muhimu tutoe ushauri na kama tunapinga basi tupinge kwa lengo la kupata mafanikio zaidi na wala tusibeze.
 
Ndiyo maana wamemruhusu Kagame kuendelea kuwaongoza.

Rwanda hakuna ujinga ujinga wa watu kukosoa na kubeza kila kitu kama bongo.
 
Sasa hapo ndiyo tumpongeze Magufuli kwa sababu bila kutuletea hzo turboprop hata kiti cha ndege maana yake tusingekuwa nacho.
 
Fuatilia Corporate plan ya ATCL kwanza.Mipango ni mikubwa na inshallah karibuni hapa itakuja bombardier CS300 itafuatiwa na B737-800/Airbus A320 na kuzidi kuongeza idadi.airline si ndege tu kuna vingi vinaendana navyo.Kuhusu kwamba ununuzi wa Q400 ulitoka Rwanda unakosea fuatilia bajeti ya wizara ya uchukuzi za miaka miwili nyuma
 
Mkuu acha ubishi wa vijiwe vya kahawa!Siku ya Mahakama Rais akiwahutubia Majaji,hakimu na watumishi wa mahakama alisema ataleta Airbus.
Baada ya ushauri na siku ile ya ujio wa Kagame kwenye ziara hapa Bongo mwezi wa July,akiwa Ikulu Rais anasema alikutana na CEO wa RwandAir na alishauriwa kununua Q400 kwa kuanzia badala ya Airbus...Hili nalo ni la kubisha??
 
Back
Top Bottom