ATCL imepata hasara ya Tsh. Bilioni 27 mwaka 2021/2022

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,370
8,107
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma, Jerry Silaa imeonesha kuwa hasara ya shirika Shirika la Ndege Nchini (ATCL) imepungua kutoka Tsh. Bilioni 36 mwaka 2020/21.

Aidha ameishauri Serikali kuharakisha mchakato wa utekelezaji wa kuhamisha umiliki wa Ndege 11 kutoka Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) kwenda Shirika la Ndege (ATCL) ili kuondokana na tatizo la kuwa na mtaji hasi wa Tsh. Bilioni 239.

Kamati hiyo pia imeeleza kuwa Shirika hilo limekuwa na ongezeko la mapato kutoka Tsh. Bilioni 58 mwaka 2018/19 hadi Tsh. Bilioni 239 mwaka 2021/22 na hasara imekuwa ikipungua ambapo mwaka 2018/19 hasara ilikuwa Tsh. Bilioni 48, mwaka 2019/20 Tsh. Bilioni 60, mwaka 2020/21 Tsh. 36, mwaka 2021/22 Tsh. Bilioni 27.


Mwaka wa Fedha 2019/2020, ilipata hasara ya TZS Bilioni 60.24
 
Hakuna watu wanaojielewa wa kuongoza hilo shirika, au kama wapo, basi wanafanya kazi kwa mazoea, bado hawajawa serious, haiwezekani kila siku TTCL habari zao ziwe zinahusu hasara tu, wakati rasilimali zote zipo upande wao.
 
Jamqa yangu alikuwa anasafiri tz to usa kwa shirika fulani. Ila anatokea mwanza ndo akapandie dar.

Flight inatoka saa 6;00 usiku na ATCL mwanza dar inatoka saa 12:00 jion ikawa sawa ili akaunge na ile .
Cha kushangaza ndege ilikuja saa 7;30 usiku ambapo flight yake ya us ishaenda.

Kilichofuata...
Atc yetu iliwagharamikia wale watu malazi full. Ndani ya siku 4 ndo wakapata ndege nyingine kwa gharama za kampuni ya wanyonge atcl.

Fikiria mtu amenunua bidhaa kwako kwa 100 then inatokea shida ya uzembe unamgjaramikia 4,000. Kwann kampuni isijiendeshe kwa hasara?

Juzi bibi alibook ndege ya saa 4;00 usiku kia to dar...lkn cha kushangaza walitoka saa 8:30 usiku. Walikaa airport kwa zaidi ya saa 4 kusubr ndege.
Yaan alitoka home saa 1 jion na akafika home saa 9 usiku huu ni mwendo wa gari kabisa ...

Mashirika yetu kuna uzembe mwingi sana unafanyika
 
Hakuna watu wanaojielewa wa kuongoza hilo shirika, au kama wapo, basi wanafanya kazi kwa mazoea, bado hawajawa serious, haiwezekani kila siku TTCL habari zao ziwe zinahusu hasara tu, wakati rasilimali zote zipo upande wao.
Umekurupuka
 
Hilo shirika la ndege linaloendeshwa kwa hasara kila siku inashindikana nini kuleta wataalamu wawe wanasimamia na kuliendesha kwa mkataba?

Ni aheri mkubali wenye uwezo wafanye kazi wawe wanalipwa % ya faida kulikoni kujazana wamatumbi kwenye bodi hadi level za watendaji.

Bodi iwe ya wazungu tu toeni takataka zote ambazo hazijui mambo ya anga. Kufanyike re-shuffle watu wafanye kazi.
 
Biashara ya Ndege ni Pasua kichwa, hizo shughuli waachieni Watu Binafsi ninyi chukueni kodi

Sasa hivi Serikali ndio inagharamia kila kitu kwa hela za Kodi ya Wananchi

Na hili jambo Wapinzani wameliongelea sana wakaitwa wasaliti.
 
Maswali ya kujiuliza Kabla ya kuona hasara pekee

Je, wakati shirika linakabidhiwa hizo ndege, lilikuwa na mtaji wa kuendesha shirika hill? Na ni kiasi gani?
 
Angalia mashirika makubwa ya Ndege Duniani, nani wanaoyaendesha:

Sir Timothy Charles Clark KBE FRAeS (born 22 November 1949) is a British business executive and the incumbent President of UAE flag carrier Emirates since January 2003. He was also the Managing Director of SriLankan Airlines until 2008.

Kama tunataka ATCL ikue na kuwa miingoni mwa mashirika ya ndege yanayotengeneza faida, tuajiri CEO mzungu mwenye uelewa na ujuzi wa kutosha katika biashara hii. Emirates, katika top management, wapo wazungu, na ndio waliojenga Emirates.
 
Rwanda Air yenyewe wameikabizi Qatar
Kenyairways nayo inahemea Mashine.
 
Back
Top Bottom