ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!.

MTATIRO: ATCL NA HASARA YA BILIONI 60
Ni muhimu sana tuwe tunafuatilia taarifa, wakati ATCL yetu (shirika linalofufuliwa) likitajwa kupata hasara ya shilingi Bilioni 60 kwa mwaka mmoja, na baadhi ya watu kuifanya kuwa ajenda kubwa na jambo la kushangaza sana, nataka mfuatilie pia hasara za baadhi ya mashirika makongwe na makubwa zaidi barani Afrika.

Mathalani, Shirika la Ndege la Kenya (Kenya Airways) limepata hasara ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 700 (mara 11 ya hasara ya ATCL) katika kipindi hicho hicho ambacho ATCL imepata hasara ya tzs Bilioni 60.

Na shirika la ndege kongwe zaidi Afrika, Ethiopian Airlines, limepata hasara ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania Tzs Trilioni 1.1 (Bilioni 1,100) ambayo ni hasara kubwa mara 18.3 zaidi kuliko ATCL.

Sote hatufurahii hasara hata kama sisi tuna hasara ya Bilioni 60, lakini kwa sababu mbili tu za sasa... uchanga wa ATCL na dunia kuzongwa na KORONA zinaweza kuifanya ATCL ijikongoje, wakati mashirika makubwa kama KE Airlines na ETH Airlines yakizongwa pia na korona.

Pia kwa mwaka jana peke yake, mashirika makubwa zaidi ya ndege duniani, kama – Delta Air Lines, American Airlines, Lufthansa Group, United Airlines, Air France-KLM, na IAG yamerekodi hasara kubwa kabisa kihistoria ya zaidi ya Dola za Marekani Bilioni 110 ambayo ni zaidi ya shilingi trilioni 2,500 za Tanzania.

Mwisho wa siku na katikati ya changamoto hizi, tunakubaliana kuwa ATCL inahitaji mikakati na mbinu za hali ya juu kibiashara ili itoke hapo ilipo, ikiwemo kuacha kabisa kufanya kazi kwa mazoea.

Julius Mtatiro,
 
Si kazi ngumu kwa rais kuua shirika binafsi au hata la serikali, lakini ujinga kufanya hivyo.
 
Mungu ibariki jf
 
Mkuu Mtatiro we jilie tu hela za UDC kaka
 

 
Mwambie mama Samia,kibaraka wewe.
 
What now?
 
Mtatiro hayo mashirika uliyoyataja hapa yote yana ndege nyingi na yanafanya safari nyingi za kwenda huko duniani kuliko sisi. So ni lazma yawe na hasara kubwa kutuzidi. Ukifanya uwiano wa sisi na wao sisi tuna hasara kubwa, manake ni kwamba tungejua na ndege nyingi na safari nyingi hasara yetu ingekua kubwa kushinda wao.
Ni lazma tujikite kwenye kutatua changamoto tuliyo nayo na sio kujilinganisha na mashirika mengine ambayo hatulingani nayo.
Jana Mh. Raisi amemhimiza CAG kuwa muwazi kama kuna shirima la uma halifanyi vizuri aseme Ili hatua stahiki zichukuliwe, ikiwemo kuyanusuru haya mashirika yetu.
Mh. Raisi alikuwa sahihi Sana, kwanza ametaka uwazi, lakini amronesha Nia thabiti ya kuokoa ama kukabiliana na mambo kama haya.
Kutoa takwimu kama hizo sidhani kama ni sahihi, mtatiro Julius haupo sahihi KWA maoni yangu.
Viva mama Samia, aluta continua
 
Ndugu ukilinganisha basi ulinganishe kweli. Air Tanzania ni shirika dogo sana, hivyo hasara ni kubwa. Ukiangalia Kenya Air, wana ndege 39 wakihudumia kimataifa. Ukipenda kulinganisha, linganisha kilomita zinazohudumiwa, au mapato yote kulingana na hasara.
 
Pascal Mayalla
Je mchango wa ATCL katika kukuza utalii na biashara ndani na nje nchi ni chini au zaidi ya hiyo billion sitini?
Je inasaidia wafanya biashara wa ndani kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kulipa kodi?🤔
Breakeven point ya ATCL ni lini (projected)?
Just thinking out of the box
 
Nakerwa na "chawa" wanaodai Corona imesababisha hasara ATCL. Mwaka 2015/16 tulipata hasara ya 94.3Bil. Corona ilikuwepo? Mwaka 2016/17 hasara 109.3Bil na mwaka 2017/18 hasara 113.8Bil. Je kulikua na Corona? Hebu acheni utetezi wa kijinga.

Hivi mkiulizwa Corona imesababishaje hasara mnaweza kujibu? Ndege zetu zinaruka ndani. Je kuna safari yoyote ya Dar KIA ilishindwa kufanyika kwa sababu ya Corona?

Yani kwa kuwa mmesikia KQ na Ethiopia wanalalamikia Corona na nyie mnajificha kwenye kichaka hichohicho? Ethiopia wana ndege 67 zinazoenda Ulaya, Marekani na China. Baada ya corona safari zimepungua. So wakisema wamepata hasara wanaeleweka. ATCL inaruka Dar Chato halafu mnajitetea corona? Abiria wa Chato wamewahi kupungua sababu ya corona?

Tupongeze juhudi za JPM kufufua ATCL, lakini tulaumu wapambe waliomshauri vibaya na kusababisha hasara hii.

Wakati ndege zinanunuliwa ZZK alishauri namna bora ya kuendesha shirika ili kuepuka hasara (anticipated). ZZK ni mtaalamu wa uchumi na alitoa ushauri kitaalamu. Akasema mashirika mengi hujiendesha kwa hasara, so tuwe na mkakati maalum kuepuka hasara au ikitokea iwe ndogo. Akadevelop economic model ya kuendesha ATCL.

Lakini akatukanwa na kuonekana si mzalendo. Leo waliomtukana ndio wanajitetea kuwa hata mashirika mengine hupata hasara. Idiots.!

Kenya Airways wanaweza kupata hasara ya 700Bil lakini thamani ya shirika lao ni 25Tril. Hasara ni sawa na 2%. Sisi tunapata hasara ya 100Bil wakati thamani ya shirika letu ni 1.8Tril, sawa na 6%. Sasa kati yetu na Kenya nani mwenye hasara zaidi?

Tusikimbilie kuona wakenya wamepata hasara kubwa kwa sababu figures zao ni kubwa, kumbuka thamani ya shirika lao ni kubwa pia. Leo Bakhresa akipata hasara ya 500M ktk biashara, wewe ukapata hasara ya 20M usijipe moyo, eti Bakhresa kapata hasara kubwa zaidi yangu. Utakua poyoyo.

Mwaka 2016/17 tulinunua Bombader kwa 90Bil. Halafu mwaka huohuo tukapata hasara 109Bil. Yani hasara ilitosha kununua Bombadier nyingine na chenchi ikabaki 🤣.

Mtafuteni ZZK na wengine waliotoa maoni wakati ndege zinanunuliwa mfanyie kazi maoni yao. Acheni upambe nuksi. Halafu mama hafagilii wapambe wala wapiga mapambio. Mambo yamebadilika. Jiongezeni.!

●NImeiona whatsap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…