ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!.

kaka Mayalla , achana na hao watu ambao kwao kutwa kucha ni kutafuta "loophole" ya serikali ya Magufuli na kupinga na ukionekana unaitetea serikali kwa kazi zake nzuri unaonekana adui wao. cha kustaajabisha hili genge la kupinga kazi nzuri za JPM lipo mitandaoni tu ila mitaani halipo.
Swali langu moja tu,

Imesharudishwa IATA?
 
Wanabodi,

Japo mimi ni miongoni mwa wale tuliopinga ununuzi wa ndege kwa cash money, na serikali yetu kufanya matumizi makubwa kama haya ya manunuzi makubwa kwa kutumia fedha za umma bila idhini ya Bunge, kwa sababu fedha za umma zinaongozwa na sheria, taratibu na kanuni, mtu hata ukiwa nani, huwezi tuu kujichotea fedha za umma na kuzitumia kununulia chochote bila kufuata sheria, taratibu na kanuni ikiwemo idhini ya bunge, unless matumizi hayo ni ya dharura, lakini mimi ni mmoja wa massuporter wakubwa wa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na rais Magufuli kufufua uchumi wa taifa letu, ikiwemo kulifufua Shirika la Ndege la ATCL.

Baada ya kuwasili kwa Bombadier, nikashauri serikali yetu, tutumie political will kuinusuru ATC na ushindani usio sawia.
Je, ATCL inahujumiwa kibiashara? Tutumie a political will kuinusuru au tuiache iangamizwe na ushindani? - JamiiForums

Fast Jet nao wakapunguza sana nauli zao na kuamua kupeleka ndege zao routes zile zile za ATC kwa bei poa zaidi, kwa vile Fast Jet wanatumia JET, na ATC wanatumia pangaboi, Fast Jet aliendelea kuipiga bao ATC.

Ujio wa Dreamliner umekuja kufunga kazi. Japo siungi mkono kurusha dege kubwa kama dreamliner kwa domestic routes ambazo ni route fupi fupi, sio tuu tunaichosha bure dreamliner yetu, bali pia tunaichakaza kwa paa shuka paa shuka ndani ya muda mfupi, lakini baada ya kuipokea taarifa hii kutoka humu humu jf, African airline Fastjet reveals urgent need for more cash - JamiiForums
kiukweli sasa ndio naungana na Watanzania wengine kumpongeza rais Magufuli kwa ununuzi wa ndege hizi. Pia sasa nalipongeza shirika la Ndege la Tanzania, ATCL kulirusha hili lidude routes za ndani za Mwanza na Kilimanjaro, kwa sababu kufuatia ujio wa Dreamliner, sasa Fast Jet, inapumulia mashine, na sio tuu itasitisha huduma zake Tanzania na kufungasha rasmi, bali Fast Jet, itakufa rasmi kwasababu roho ya Fast Jet, ni biashara ya Tanzania.

Kufuatia Dreamliner ya ATCL kuruka Mwanza na Kilimanjaro, Fast Jet na Precision zimekosa abiria wa Mwanza na Kilimanjaro, hivyo sasa Fast Jet, ni soon atakubali matokeo na kunyanyua mikono yake juu, atabaki Precision, hivyo kama anataka usalama na kuendelea ku survive, asarender routes za Mwanza na Kilimanjaro kwa ATCL, yeye aende routes nyingine za mikoa mingine ambayo haina ndege kama Singida, Shinyanga, Songea etc.

Kufa kufaana, hivyo taarifa za Fast Jet kupumulia mashine ni habari njema kwa Watanzania wazalendo na ATC yetu, kwa sababu nimeisha safiri na Dreamliner safari 8, na hakunahata safari moja ndege ilijaa, hivyo nikaogopa kama ni hii, then nikajisemea kimoyo moyo kuwa hii Dreamliner inaoparate kwa hasara, lakini kutokana na zile mbwembwe za mapokezi ya ndege hii, no one can dare say that!, hivyo hasara hiyo itabebwa kimya kimya kufa kizungu na tai shingoni, hivyo kifo cha Fast Jet ni neema kwa ATC ambapo sasa dreamliner yetu itajaa.

Japo sio ustaarabu kufurahia matatizo ya mwenzako, kama kifo cha Fast Jet kwa sababu, ni Fastjet ndio walituokoa wakati ATC ilipokufa na PAA wakawa wanatukomoa!. Besides wafanyakazi ni Watanzania wenzetu, na Fast Jet, ilikuwa inafanya biashara halali na kuchangia uchumi wa taifa, hivyo tusiibeze Fastjet au kufuraia kifo chake, lakini tukubali tukatae, mgeni alineemeka wakati mwenyeji akichechemea, sasa mwenyeji kapona, inabidi mgeni arudi kwao.

Tena kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikifanywa ni shamba la bibi, kwa kila mtu kutoka anakotoka na kuja kujichumia na kujivunia as if Tanzania haina wenyewe, kwa vile Fastjet ni shirika la kigeni, then faida yote inapelekwa huko nje kwa wenye hisa, hivyo ATC sasa imeonyesha, kwenye usafiri wa anga, Tanzania ina wenyewe. Hivyo hata Fast Jet wakifungasha, abiria bado wataendelea kupanda ATCL, hivyo taifa kuendelea kupata mapato, na kwa vile ATC bado inaleta ndege nyingine 4, itaweza kuwameza wafanyakazi wote wa Fast Jet.

Kuna mwanajf huyu alisema jambo la maana sana hapa, Hakuna abiria wa kushindanisha kwa "afya" mashirika matatu ya ndege kwa safari za ndani - JamiiForums
Hivyo naamini PAA watajiandaa yasiwakute ya Fastjet.

Hivyo sasa ATC sio tuu itatawala soko, bali sasa ndio itarudisha heshima ya nchi, inarudisha heshima Taifa, na huu utaratibu wa kuwafungasha virago watu, uendelee kwa routes za Afrika Mashariki, tuje routes za Ghuba, India na China, kisha tufunge kazi na New York na London.

Poleni sana Fast Jet, Hongera ATCL
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums

Ushauri wa Bure kwa ATC: Anzisheni frequently fliers na fanyeni over booking kwa waiting list. - JamiiForums
Ndege ya ATCL yachelewa kuondoka ndani ya muda; watoa ufafanuzi! - JamiiForums

Tupunguze "kuisimanga" ATCL, haijengi zaidi ya kukatisha tamaa - JamiiForums

Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa ...
Update 1
Very objective and constructive contribution
Satire
 
Achana na hao Mabeberu IATA sisi tunaweza kuanzisha ya kwetu kupitia SIDO na kutambulika kimataifa. Tuwe wazalendo
IATA vs SIDO tena?
Mbona tofauti Mkuu?
IATA inatuwezesha kutambulika kimataifa na hata agencies za nje zinaweza ku book kwenye ndege zetu ziiatupatia abiria wakala commission yao.

SIDO hata kutengeneza Water Well Drilling Machine kama za PAT wanashindwa tunaishia kuagiza nje katika zama hizi tunazoziita za Tanzania ya Viwanda.
 
Tirana,
IATA vs SIDO tena?
Mbona tofauti Mkuu?
IATA inatuwezesha kutambukika kimataifa na hata agencies za nje zinaweza ku book kwenye ndege zetu ziiatupatia abiria wakala commission yao.

SIDO hata kutengeneza Water Well Drilling Machine kama za PAT wanashindwa tunaishia kuagiza nje katika zama hizi tunazoziita za Tanzania ya Viwanda.
SIDO ni zaidi ya IATA ndugu. Usituchukulie poa
 
True, ATC ndio habari kuu hadi jamaa wanatuonea wivu na kukamata ndege yetu kwa deni la nineteen forty kweusi!.
This is not fair.
P

Sikuamini umechuchumaa kiasi hiki (stooping too low). Kwa wanaoheshimu utawala wa sheria wanaamini deni ni hai mpaka litakapolipwa kwa namna ilivokubaliwa. Hata sisi kama nchi tuna mikopo na tunailipa bila kujali muda wake!! Kwako fairness ni kukataa kumlipa mdeni wako!

Kuna madeni ya ndani, nadhani unaona ni fair kuwa hayalipwi. Ukweli ni kuwa kama kungekuwa kuna namna ya kushikilia mali za serikali kulazimisha serikali ilipe madeni - ingetokea hivo. Kukosekana kwa mechanism hiyo isifanye fairness iwe ni pale inaposhindikana kulazimisha kulipwa deni.

Sisi sio hata wa kuonewa wivu - ni wa kuhurumiwa. Umeshasikia ET au hata KQ wakishikiliwa ndege zao nje ya nchi???

Tujifunze kuona haki kama double-edged sword!!!
 
Sikuamini umechuchumaa kiasi hiki (stooping too low). Kwa wanaoheshimu utawala wa sheria wanaamini deni ni hai mpaka litakapolipwa kwa namna ilivokubaliwa. Hata sisi kama nchi tuna mikopo na tunailipa bila kujali muda wake!! Kwako fairness ni kukataa kumlipa mdeni wako!

Kuna madeni ya ndani, nadhani unaona ni fair kuwa hayalipwi. Ukweli ni kuwa kama kungekuwa kuna namna ya kushikilia mali za serikali kulazimisha serikali ilipe madeni - ingetokea hivo. Kukosekana kwa mechanism hiyo isifanye fairness iwe ni pale inaposhindikana kulazimisha kulipwa deni.

Sisi sio hata wa kuonewa wivu - ni wa kuhurumiwa. Umeshasikia ET au hata KQ wakishikiliwa ndege zao nje ya nchi???

Tujifunze kuona haki kama double-edged sword!!!
CAG kwenye report yake alilitaja hili deni amekuwa akifanya hivyo akiua madhara yake lakini kwakukuwa bunge liliamua kutikufanya kazi naye walilipita tu kama hawalioni.

Mimi na Amini kama bunge kingefanya kazi yake vema tusingekuwa kwenye kadhia hii, Maadamu limeshatokea basi tukae chini na mdai tuone jinsi gani tutamalizana naye kwa Mazungzo.
 
Back
Top Bottom