ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!.

Sikuamini umechuchumaa kiasi hiki (stooping too low). Kwa wanaoheshimu utawala wa sheria wanaamini deni ni hai mpaka litakapolipwa kwa namna ilivokubaliwa. Hata sisi kama nchi tuna mikopo na tunailipa bila kujali muda wake!! Kwako fairness ni kukataa kumlipa mdeni wako!

Kuna madeni ya ndani, nadhani unaona ni fair kuwa hayalipwi. Ukweli ni kuwa kama kungekuwa kuna namna ya kushikilia mali za serikali kulazimisha serikali ilipe madeni - ingetokea hivo. Kukosekana kwa mechanism hiyo isifanye fairness iwe ni pale inaposhindikana kulazimisha kulipwa deni.

Sisi sio hata wa kuonewa wivu - ni wa kuhurumiwa. Umeshasikia ET au hata KQ wakishikiliwa ndege zao nje ya nchi???

Tujifunze kuona haki kama double-edged sword!!!

Mkuu

Jinga hilo!

Lilishafungua uzi eti linafurahi mke wake anakaa Marekani na lenyewe lipo Tanzania!

Like really??

Dont waste bando lako kwa hilo punguani mkuu!

Bure kabisa!
 
Sikuamini umechuchumaa kiasi hiki (stooping too low). Kwa wanaoheshimu utawala wa sheria wanaamini deni ni hai mpaka litakapolipwa kwa namna ilivokubaliwa. Hata sisi kama nchi tuna mikopo na tunailipa bila kujali muda wake!! Kwako fairness ni kukataa kumlipa mdeni wako!

Kuna madeni ya ndani, nadhani unaona ni fair kuwa hayalipwi. Ukweli ni kuwa kama kungekuwa kuna namna ya kushikilia mali za serikali kulazimisha serikali ilipe madeni - ingetokea hivo. Kukosekana kwa mechanism hiyo isifanye fairness iwe ni pale inaposhindikana kulazimisha kulipwa deni.

Sisi sio hata wa kuonewa wivu - ni wa kuhurumiwa. Umeshasikia ET au hata KQ wakishikiliwa ndege zao nje ya nchi???

Tujifunze kuona haki kama double-edged sword!!!

Hivi uko serious hujamwelewa P??????
 
Ndege IPO mbioni kurudi. Wanasheria wetu nguli wapo huko kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

Acha kubagaza ndugu. ATC ni yetu sote
Wameenda kumtafuta Lawyer wakuwasaidia huko maana kwa uwezo wa Wanasheria wetu hatuwezi
 
kaka Mayalla , achana na hao watu ambao kwao kutwa kucha ni kutafuta "loophole" ya serikali ya Magufuli na kupinga na ukionekana unaitetea serikali kwa kazi zake nzuri unaonekana adui wao. cha kustaajabisha hili genge la kupinga kazi nzuri za JPM lipo mitandaoni tu ila mitaani halipo.
Haya kiko wapi sasa? Siyo kila anayetoa mawazo kinyume na fikra za Magufuri ni mpinzani. Wengine wanataka tufuate taratibu kwenye mambo strategic ya nchi. Kwa mfano haiingii akilini Rais na Mpwawe Dotto ndiyo waliofanya manunuzi ya ndege. Hii ni kinyume cha Sheria na taratibu za fedha na hizo ni dalili za kwamba wamepokea RUSHWA. Huyu Magufuri anadanganya watu kuwa anapiga vita RUSHWA kwa maneno wakati kivitendo ana dalili zote za kupokea RUSHWA. Hata wasipojibu leo watakuja kujibu hata miaka 50 baadaye.

Hayo ndiyo tunapinga na siyo kuwa na ndege za ATCL.
 
Huu uzi ulipoanzishwa ulikuwa na Nia ya kuishauri serikali kupunguza ushindani wa biashara, wakati huo nadhan target ilikuwa Fast jet

Mtoa Mada fat jet kweli haipo Tena , Leo hii nauli ya mbeya to dar kwa Atcl ni 384000 one way., with fast jet nimewahi kusafiri kwa sh 38500 mwanza, huku mbeya ilikuwa ni 19000the highest

Si kwa mbaya ila naamini wengi wetu sasa tumerudi kwenye usafiri wa mabasi
 
Wanabodi,

Japo mimi ni miongoni mwa wale tuliopinga ununuzi wa ndege kwa cash money, na serikali yetu kufanya matumizi makubwa kama haya ya manunuzi makubwa kwa kutumia fedha za umma bila idhini ya Bunge, kwa sababu fedha za umma zinaongozwa na sheria, taratibu na kanuni, mtu hata ukiwa nani, huwezi tuu kujichotea fedha za umma na kuzitumia kununulia chochote bila kufuata sheria, taratibu na kanuni ikiwemo idhini ya bunge, unless matumizi hayo ni ya dharura, lakini mimi ni mmoja wa massuporter wakubwa wa hatua mbalimbali zinazochukuliwa na rais Magufuli kufufua uchumi wa taifa letu, ikiwemo kulifufua Shirika la Ndege la ATCL.

Baada ya kuwasili kwa Bombadier, nikashauri serikali yetu, tutumie political will kuinusuru ATC na ushindani usio sawia.
Je, ATCL inahujumiwa kibiashara? Tutumie a political will kuinusuru au tuiache iangamizwe na ushindani? - JamiiForums

Fast Jet nao wakapunguza sana nauli zao na kuamua kupeleka ndege zao routes zile zile za ATC kwa bei poa zaidi, kwa vile Fast Jet wanatumia JET, na ATC wanatumia pangaboi, Fast Jet aliendelea kuipiga bao ATC.

Ujio wa Dreamliner umekuja kufunga kazi. Japo siungi mkono kurusha dege kubwa kama dreamliner kwa domestic routes ambazo ni route fupi fupi, sio tuu tunaichosha bure dreamliner yetu, bali pia tunaichakaza kwa paa shuka paa shuka ndani ya muda mfupi, lakini baada ya kuipokea taarifa hii kutoka humu humu jf, African airline Fastjet reveals urgent need for more cash - JamiiForums
kiukweli sasa ndio naungana na Watanzania wengine kumpongeza rais Magufuli kwa ununuzi wa ndege hizi. Pia sasa nalipongeza shirika la Ndege la Tanzania, ATCL kulirusha hili lidude routes za ndani za Mwanza na Kilimanjaro, kwa sababu kufuatia ujio wa Dreamliner, sasa Fast Jet, inapumulia mashine, na sio tuu itasitisha huduma zake Tanzania na kufungasha rasmi, bali Fast Jet, itakufa rasmi kwasababu roho ya Fast Jet, ni biashara ya Tanzania.

Kufuatia Dreamliner ya ATCL kuruka Mwanza na Kilimanjaro, Fast Jet na Precision zimekosa abiria wa Mwanza na Kilimanjaro, hivyo sasa Fast Jet, ni soon atakubali matokeo na kunyanyua mikono yake juu, atabaki Precision, hivyo kama anataka usalama na kuendelea ku survive, asarender routes za Mwanza na Kilimanjaro kwa ATCL, yeye aende routes nyingine za mikoa mingine ambayo haina ndege kama Singida, Shinyanga, Songea etc.

Kufa kufaana, hivyo taarifa za Fast Jet kupumulia mashine ni habari njema kwa Watanzania wazalendo na ATC yetu, kwa sababu nimeisha safiri na Dreamliner safari 8, na hakunahata safari moja ndege ilijaa, hivyo nikaogopa kama ni hii, then nikajisemea kimoyo moyo kuwa hii Dreamliner inaoparate kwa hasara, lakini kutokana na zile mbwembwe za mapokezi ya ndege hii, no one can dare say that!, hivyo hasara hiyo itabebwa kimya kimya kufa kizungu na tai shingoni, hivyo kifo cha Fast Jet ni neema kwa ATC ambapo sasa dreamliner yetu itajaa.

Japo sio ustaarabu kufurahia matatizo ya mwenzako, kama kifo cha Fast Jet kwa sababu, ni Fastjet ndio walituokoa wakati ATC ilipokufa na PAA wakawa wanatukomoa!. Besides wafanyakazi ni Watanzania wenzetu, na Fast Jet, ilikuwa inafanya biashara halali na kuchangia uchumi wa taifa, hivyo tusiibeze Fastjet au kufuraia kifo chake, lakini tukubali tukatae, mgeni alineemeka wakati mwenyeji akichechemea, sasa mwenyeji kapona, inabidi mgeni arudi kwao.

Tena kwa muda mrefu Tanzania imekuwa ikifanywa ni shamba la bibi, kwa kila mtu kutoka anakotoka na kuja kujichumia na kujivunia as if Tanzania haina wenyewe, kwa vile Fastjet ni shirika la kigeni, then faida yote inapelekwa huko nje kwa wenye hisa, hivyo ATC sasa imeonyesha, kwenye usafiri wa anga, Tanzania ina wenyewe. Hivyo hata Fast Jet wakifungasha, abiria bado wataendelea kupanda ATCL, hivyo taifa kuendelea kupata mapato, na kwa vile ATC bado inaleta ndege nyingine 4, itaweza kuwameza wafanyakazi wote wa Fast Jet.

Kuna mwanajf huyu alisema jambo la maana sana hapa, Hakuna abiria wa kushindanisha kwa "afya" mashirika matatu ya ndege kwa safari za ndani - JamiiForums
Hivyo naamini PAA watajiandaa yasiwakute ya Fastjet.

Hivyo sasa ATC sio tuu itatawala soko, bali sasa ndio itarudisha heshima ya nchi, inarudisha heshima Taifa, na huu utaratibu wa kuwafungasha virago watu, uendelee kwa routes za Afrika Mashariki, tuje routes za Ghuba, India na China, kisha tufunge kazi na New York na London.

Poleni sana Fast Jet, Hongera ATCL
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums

Ushauri wa Bure kwa ATC: Anzisheni frequently fliers na fanyeni over booking kwa waiting list. - JamiiForums
Ndege ya ATCL yachelewa kuondoka ndani ya muda; watoa ufafanuzi! - JamiiForums

Tupunguze "kuisimanga" ATCL, haijengi zaidi ya kukatisha tamaa - JamiiForums

Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa ...
Update 1
Very objective and constructive contribution
ATC hasara bilioni 60!.
Taarifa ya CAG.
Kuna vitu kuna watu tulisema humu, tukanyooshewa vidole vya kukosa uzalendo!. Sasa ukweli umethibitika!.
60 billions kwa mwaka!, it's not a joke!
Duh...!.

P
 
ATC hasara bilioni 60!.
Taarifa ya CAG.
Kuna vitu kuna watu tulisema humu, tukanyooshewa vidole vya kukosa uzalendo!. Sasa ukweli umethibitika!.
60 billions kwa mwaka!, it's not a joke!
Duh...!.

P
Rip Magufuli
 
ATC hasara bilioni 60!.
Taarifa ya CAG.
Kuna vitu kuna watu tulisema humu, tukanyooshewa vidole vya kukosa uzalendo!. Sasa ukweli umethibitika!.
60 billions kwa mwaka!, it's not a joke!
Duh...!.

P
Nafasi ya Msigwa itakufaa
 
ATC hasara bilioni 60!.
Taarifa ya CAG.
Kuna vitu kuna watu tulisema humu, tukanyooshewa vidole vya kukosa uzalendo!. Sasa ukweli umethibitika!.
60 billions kwa mwaka!, it's not a joke!
Duh...!.

P
Ukiwashauri wanasema una njaa au sio mzalendo. Time will tell!
 
Back
Top Bottom