Elections 2010 Atangaza kumvaa baba yake kwenye ubunge

Jamani tuwape shavu waliousika kutujengea
baraza jipya la mitiani lililopo maeneo ya mbezi
beach makonde
 
Ni bora nchi iuzwe alafu kila mtu apewe chake kieleweke
Umakini unahitajika katika kuchangia mada muhimu kama hii kwani imekuwa ikituzawadia viongozi wa kiaina kwa mtindo huu wa sisi wapiga kura kufanya mzaha kwenye mambo ya msingi.

Kama ni suala la nchi kuuzwa ili sisi tugawane kwani mauzo ya ngorongoro mwenzetu ushagawiwa shilingi ngapi? Mauzo ya migodi na makampuni ya umma ambayo wewe unayafahamu umegawiwa shilingi ngapi? Au ni wewe uliyekuwa unaongoza maandamano ya kusifia spichi ya muheshimiwa kule TBR?
 
changa la macho hilo, anataka kupunguza mashambulizi kwa dingi yake. siamini kama hilo si dili kati yake na huyo dingi wake....ili kupunguza mashambulizi au wapinzani.
 
Yani huyu jamaa anaenda kuwaabisha watu wa rorya maana hata kuzungumza kiswahili vizuri hajui sijui bungeni atatumia lugha gani
 
Siasa bana

Yaani wananchi ni wapuuzi sana kama wakikubaliana na propaganda hii

1: Hoteli ya Lakairo ni ya Philemon Sarungi na baadhi ya watu na Lameck anaisimamia tu

ni kweli hoteli ni ya sarungi yeye ni msimamizi tu,may be sarungi anataka kulipa fadhili
 
Ki msingi Lameck ni kijana mwenye mitazamo ya maendeleo. naamini kuwa anaweza kufanya mengi akipewa nafasi. Pia naamini kuwa hata akikosa ubunge bado anaweza kuendelea na moyo wake wa maendeleo katika jamii ya Rorya hasa katika nafasi ya udiwani wake. Ila nawakumbusha kuwa Kijiji cha Mika bado hawana hata dispensary, maji ya kunywa hakuna, pamoja na kuzungukwa na vijiji vya Utegi na Kiterere ambako kuna umeme na miundo mbinu, naomba uongozi wa kipindi kijacho uone uwezekana wa changamoto kwa KIJIJI CHA MIKA!
Lameck usikate tamaa endelea na wito wako, kama ni chaguo la wananchi wa Rorya basi watakupa kura.
Nakutakia kila la kheri...
 
Nilimsikiliza leo akitangaza nia yake kupitia ITV.

Jamani mtu anaweza kuwa anasaidia kutoa misaada katika misiba na kutoa michango kijijini lakini ukweli utabaki kuwa ingawa ni haki yake ya kimsingi kugombea, Lameck atapwaya katika kuwawakilisha Wananchi wa Rorya Bungeni endapo atachaguliwa.

Kama walivyosema wengine uwezo wake wa kuchambua, kujenga au kuchangia hoja Bungeni utakuwa wa kuchekesha.

Eti anasema atakuwa anawaamuru makatibu Tarafa, atakuwa hategemei bajeti ya serikali katika maafa / matatizo bali yeye mwenyewe n.k Aidha, aliifagilia sana elimu yake ya darasa la saba huku akiponda wasomi maana eti ''wanazima simu usiku'' na hivyo wakitafutwa hawaonekani!
Pia alitamba kuwa ana uwezo mkubwa maana wafanyakazi wake ( wa Lacairo) hawajawahi kukosa mshahara! Kisha akaitimisha kwa kibwagizo cha Kijaluo. Yetu macho kuona nani ataibuka kidedea huko ukweni kwetu.
 
Maji hufuata mkondo. Inawezekana. Mbona watoto wa wanasheria ni wanasheria, madaktari pia, wahasibu nk. Kuipenda kazi ya baba yako na kujitahidi uwe hicyo inawezekana Tatizo ni pale utakapopewa tu kwa sababu ya baba yako au ndugu yako.

Hapana...Udaktari haurithishwi...lazima usome miaka 18 hivi sasa usilinganishe na siasa...unaweza kumrithisha mtoto wako kisiasa bila yeye kufanya jitihada yoyote ile...ndio maana watu wote wanakimbilia huko....mbona hwakimbilii pale Mlimani kuchukua fomu?
 
1. Lameck Airo na Sarungi wanatoka mji wa utegi.
2. Alikuwa mpiga debe mkuu wa sarungi kwa muda mrefu.
3. amesoma utegi primary, na Kotwo darasa la saba, kama kajiendeleza sina uhakika.
4. Lackairo hotel ni yake, jamaa alianza kufanya biashara ya toka akiwa primary school, enzi hizo biashara za magendo toka kenya. biasahra yake ilipopanuka akaamia Mwanza.
5.Jamaa ni mchakarikaji sana, na amewasaidia baadhi ya watu masikini wa Rorya, Sarungi yeye alikuwa amelala.
6. Ubunge kwake ni maji marefu, hajui kujenga hoja, kupambanua mambo, angebaki kwenye udiwani.
7. Umasikini uliyokithiri Rorya na tanzania kwa ujumla ndo inayosababisa wananchi kuwaona wenye vijisenti kama mungu mtu.
8. Ndo kati ya madiwani waliyoleta vurugu kuhusu makao makuu ya rorya iwe wapi, rushwa ilikuwa nje nje.

Ila jamaa angendelea na biashara zake asitafutana na mambo ya siasa angefika mbali sana, maana biashara kaianza utotoni. Bungeni hawezi kufungua mdomo.
 
Back
Top Bottom