Atangaza kumvaa baba yake kwenye ubunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atangaza kumvaa baba yake kwenye ubunge

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanza Madaso, Apr 29, 2010.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Naomba kuuliza huyu Lameck Airo ndo mwenye Lacairo Hotel Mwanza Kirumba?

  Atangaza kumvaa baba yake kwenye ubunge

  [​IMG]
  Mbunge wa sasa wa jimbo Rorya, Prof. Phillemon Sarungi.

  Lameck Airo ametangaza nia ya kugombea ubunge ili kushindana na baba yake mdogo kupitia Chama Cha Mapindizi (CCM) katika jimbo la Rorya mkoani Mara.

  Airo ambaye ni diwani wa kata ya Koryo (CCM) na kamanda wa vijana wa wilaya ya Rorya ni mtoto wa mdogo wake mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Prof. Phillemon Sarungi.

  Ingawa hajatangaza nia, kuna kila dalili kwamba Sarungi ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 10, atatetea tena kiti chake.

  Airo alitangaza uamuzi huo katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa jumuia ya wanawake wa chama hicho (UWT) ikiwa ni mara yake ya pili kutangaza nia hiyo.

  Alisema kama mwana-CCM ni haki yake ya msingi kujitokeza kugombea ubunge katika jimbo hilo ili aweze kutoa mchango wake wa kuharakisha maendeleo.

  Alisema kwa muda mrefu alikuwa mpiga debe mkubwa kwa mgombea wa CCM ambaye ni baba yake mkubwa, hivyo ni wakati wake sasa na yeye kupigiwa debe.

  Akifungua mkutano huo, Airo ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliwataka wanawake wa chama hicho kuunganisha nguvu zao pamoja katika kuhakikisha chama hicho kinaibuka na ushindi wa kimbunga kwa nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais katika uchaguzi wa mwaka huu.

  Akitoa salamu za serikali za wilaya hiyo, mkuu wa wilaya ya Rorya, Kanali mstaafu Benedict Kitenga, alisema kuwa serikali ya wilaya yake inasikitishwa na mila za wakazi wa wilaya ya Rorya kuwakandamiza wanawake kwa kushindwa kuwapa nafasi za maamuzi hasa za kugombea uongozi.

  “Mimi nawaomba hali hii ninayoiona hapa kwetu ya kuwatenga wanawake kwa kushindwa kuwapa nafasi za maamuzi itasababisha tusifikie kauli yetu ya uwakilishi wa 50 kwa 50. Nawa ombeni tubadilike ili wanawake wawezeshwe na wakiwezeshwa wanaweza,” alisema kanali Kitenga

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ndiye mmiliki Mazee! Ninafahamiana naye kimtindo
   
 3. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Asante mkuu Masa kwani sikujua kuwa huyu Bwana anatoka ule mkoa.
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamaa chenji anayo ila nadhani ubunge ni kazi kubwa sana kwake aendeleze biashara zake tu! Shule yake nina wasi was sana maana huwa hajui hata kujenga hoja
   
 5. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Tatizo anataka kupambana na Mkongwe bora kama angekuwa kwenye game kwa muda mrefu lakini kwa kuanza tu na anataka ubunge sidhani kama ataambulia chochote.
   
 6. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Tena wengi wao licha ya kutoka mikono mitupu huwa wanafirisika kabisa...Nadhani huto tujisenti twake kama tunamuasha atashangaa vitakapoyeyukia humo CCM...
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Confusion iliyopo ni kudhani kwamba kila mwenye chenji basi ana sifa za kuwa kiongozi na msingi wa imani hiyo ni kule kujua kwamba rupia itapenyezwa kila penye udhia. Ukifuatilia sana inawezekana tukaambiwa kwamba hata elimu yenyewe ni ya mashaka! Lakini na yeye amevutwa na waliomtangulia ambao anajua wanafanana naye na walipjaribu tu wakaukwaa. Na ndio hao ambao kule mjengoni wamebaki kuwa spectators. Kiwango cha kufikiri na kujenga hoja cha baadhi ya wabunge wetu ni cha kuogofya na kutia aibu sana!
   
 8. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280
  Port, si unajua hawa interests zao? anataka kugombea aingie CCM kusudi mambo yake yamnyokee. Shame on our system that people cant make their living without subjecting their interests into politics..too bad....Na akishindwa..ole wake aingie upinzani....ataambiwa LACAIRO imejengwa sehemu ya barabarani na hivyo inabidi ivunjwe kupisha ujenzi wa barabara..lol...
   
 9. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  mimi namfahamu sana huyu jamaa elimu yake ni darasa la saba, ila alijiendeleza kidogo nadhani atahitimu mwaka huu form kama aliendelea na shule aliyoianza mwaka 2007
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160

  Kiwango cha mwisho (minimum qualifications) kwa anayegombea ubunge/Mbunge ni ELIMU ya kiwango kipi?
   
 11. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #11
  May 7, 2010
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Siasa bana

  Yaani wananchi ni wapuuzi sana kama wakikubaliana na propaganda hii

  1: Hoteli ya Lakairo ni ya Philemon Sarungi na baadhi ya watu na Lameck anaisimamia tu

  2: Sarungi amechoka kisiasa so anataka kumwachia mtu mwingine

  Sarungi hagombei mwaka 2010 so hii ni Propaganda ya kijinga sana..

  shame on you guys..kama mtu unajua una uwezo wa kugombea usitumie uongo uongo tu
   
 12. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #12
  May 7, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  I know this guy, he has some relationship with Prof Sarungi. His education is apparenltly not clear if he went to school. Dependable sources describe him as some one who never had a chance to complete std four. He left school in the middle of grade four. So it is very true that he may not be a right candidate to take Rorya in the next five years after election.

  I am of the same opinion with one of the members of the JF that, it is a silly idea to think that your money can guarantee/earn you good leadersip even if you dont have other preliquesites of leadship.
   
 13. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #13
  May 7, 2010
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Tutaona na kusikia mengi mwaka huu

  nimesikia hata Mwandishi wa Habari mkoani Lindi atagombea kiti cha baba yake katika jimbo la Lindi Mjini,Nchii hii sasa ni kugawana vyeo tu,baba kwa mtoo yahani we acha tu
   
 14. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #14
  May 7, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Na hilo ndilo kosa kubwa tunalofanya watanzania kama anavyoandika Padre Privatus Karugendo kwenye Raia Mwema ya wiki hii. Kila anayepata umashuhuri kwenye fani nyingine anadhani kuwa umashuhuri wake hauwezi kukamilika bila kuwa Mbunge!! Ushauri wako ni mwema. Wakati mwingine ni vyema mtu ukaendelea na shughuli zako zilizokufikisha hapo ulipo na ukawa mtazamaji tu wa vipindi vya Bunge!!

   
 15. M

  MJM JF-Expert Member

  #15
  May 7, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Maji hufuata mkondo. Inawezekana. Mbona watoto wa wanasheria ni wanasheria, madaktari pia, wahasibu nk. Kuipenda kazi ya baba yako na kujitahidi uwe hicyo inawezekana Tatizo ni pale utakapopewa tu kwa sababu ya baba yako au ndugu yako.
   
 16. M

  Mkono JF-Expert Member

  #16
  May 7, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 569
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mi sioni ajabu! kwani issue kama ni madarasa mboni wapo wengi,au hadi Msemakweli Keinerugaba amtaje! Kupata ama kukosa itategemea na elimu juu uchaguzi imewafikia kwa kiasi gani wananchi wa Ryora,kama watakuwa sawa kimtazamo na wananchi wa jimbo la kwetu kule Kyerwa basi mjue kabisa jamaa mwakani tutamuona ndani ya mjengo ,hawa wanawakubali sana wenye nazo.
   
 17. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Gooodest
   
 18. Jungumawe

  Jungumawe JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2010
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 246
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kama ni kweli Basi Tanzania bila utajiri inawezekana
   
 19. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,828
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  yale yale tu ya uprince na uprinces ila wapiga kura wanatumika kwa umbumbu wao:angry:
   
 20. M

  Mwanambati New Member

  #20
  May 9, 2010
  Joined: May 9, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni bora nchi iuzwe alafu kila mtu apewe chake kieleweke
   
Loading...