- Thread starter
- #121
Pole sana ndgu yetu, kuna ndugu yetu aliwahi kuwa na matatizo km yako alitibiwa kila hospital ikiwa ni pamoja na muhimbiri na Lugaro lkn hakupata nafuu mwisho akakata shauri kwenda kwa watalaamu wa tiba kienyeji bahati mbaya tulipoteza. Likini kuna rafiki yangu alikuwa na matatizo km yako kwa sasa anaendelea vizuri lakini iligundulika kuwa alikuwa na tatizo kwenye uti wa mgongo na kusababisha kubanwa kwa mishipa ya fahamu hivyo kupoteza kumbukumbu, kuota ndoto mbaya, kukosa nguvu na nk. alipimwa kimipo cha MRI sina hakika na jina lake mi siyo Dakatari nahishi hivyo pale muhimbili ni laki 7 agha khan Dsm inaweza kuwa zaidi. lkn hivi karibuni nilikutana na mama mmoja kwenye basi katika maongezi tukazungumzia ugonjwa km huo, aliniambia kuwa yeye alikuwa anaumwa vibaya mpaka alihisi kurogwa lkn ilikuja kugundulika kuwa mishipa ya fahamu ilikuwa imebanwa kwenye uti wa mgongo. kwa sasa anafanya mazoezi kwa kutumia technolojia ya Korea ya kitanda cha umeme maarufu km huduma ya seragem hapa Dsm. jaribu kuangalia vitu hivyo huenda una tatizo hilo.
Pia jaribu kuulizia historia au wewe mwenyewe vuta kumbukumbu km hukuwahi kuumia mgongo au ajari katika michezo ya utotoni, au kuanguka kidogo na nk. ukipata jawabu fanya utafiti utapata jibu then nilazima umpate daktari bingwa nafikiri wa mifupa hao wengine watakula pesa zako na mwisho watakwambia umelogwa.
Polse sana. km ukifanikiwa leta majibu hapa ili tujue na tuwasaidie wengine pia.
Asante kwa uzoefu wako juu ya hili kaka mshino, historia ni mwalimu mzuri tunaweza tumia vizuri kuendelea mbele.
Hakuna matata, kwa lolote nitaweka mrejesho hapa mungu akituweka hai.
Kila la kheri!