Shakidinkili
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 458
- 174
Maelezo yako yanavuta matapeli wazidi kukuibia kwa sababu kichwani kwako umeamini kulogwa. Umesema nyie ni maskini, sasa hao watu wawaonee wivu gani kwa raha gani miliyonayo hapa duniani. Ninakuomba ueleze kinagaubaga unaumwa kitu gani, yaani aidha kichwa hakiponi, tumbo au kiungo gani hasa na maumivu yakoje. Mimi sio mwumini wa dini ya USHIRIKINA, bali yako mambo mengine ni ya kimila tu. Nitakupa mfano mmoja. Dada mmoja alizaliwa katika familia maskini lakini Mungu akamjalia kupata elimu na bahati nzuri enzi za Mwalimu elimu ilikuwa bure mpaka upeo wa akili yako, hivyo yeye alipata elimu ya chuo kikuu. Alianza kazikama Mwalimu na na muda mfupi baadaye akajenga nyumba yake ya kisasa ya kuishi kijijini kwa wazazi wake, akajaliwa kupata mtoto wake wa kwanza lakini yule mtoto alimtesa sana mama yake kwa kuugua kila wakati. Yule dada alizunguka mahospitali mengi pasipo mafanikio na vipimo vyote havikuonyesha maradhi yanayomsibu mtoto. Mwisho aliamua kwenda kwenye tiba mbadala (kienyeji) na bahati nzuri alikutana na mtu sio tapeli na wala hakumpa dawa yoyote bali alimwambia kuwa huko kwenu kuna mtu japo wewe humfahamu alifariki wakati wewe hujazaliwa, alikuwa anaugua ukoma, huyo mtu analalamika kuwa wewe ni kizazi chake umefanikiwa katika maisha na umejenga nyumba nzuri, hivyo na yeye anaomba ukamjengee nyumba. Yule binti alifunga safari hadi kwa wazazi wake na kuliulizia hili, aliambiwa ni kweli kuna mjomba wake huyo dada, yaani kaka wa mama yake alikufa zamani kwa ugonjwa wa ukoma na wakampeleka kwenye kaburi lake. Alichofanya ni kununua cement na kuajiri mafundi wakajengea kaburi la huyo Mjomba na kufanya sala kwa imani ya dini yake. Basi kuanzia siku hiyo tatizo lake lilikoma na mtoto hakuugua tena.