Mkuu nimeguswa haswa na uzi wako, mama yangu alifariki nikiwa shule ya msingi miaka 17 iliyopita. Haijawahi kupita siku sijammis. Graduations, harusi, kupata watoto, nikiwa kwenye misukosuko, neema,vipindi vyote hivyo nilitamani awepo tufurahi wote, anifariji, aone wajukuu. Nimeishi zaidi ya nusu ya umri wangu wa sasa bila yeye, upendo wangu kwake haujawahi kupungua na nahisi kumhitaji kila siku ila ndio hivyo alipangalo mola. Pumzika kwa amani mama,Amein!
I love my dad! The best dad ever (until you ask my daughter then she'll tell you that I'm the best dad in the whole wide world)
Leo MCHUNGUZI HURU uko sahihi kabisa tena 100% ila kama title tu inavyojieleza its really at your own risk comment za humu zinaliza :crying: :crying:jamani its so sad :sad: :sad:to loose one of your parents,POLENI :sorry: :sorry:SANA MLIOWAPOTEZA WAZAZI WENU I CAN FEEL THE PAIN THAT GOES WITH YOUR FEELINGS AND WORDS.
Matola, familia zinatofautiana sana. Kuna familia mama is everything, Kuna familia mama ni bread winner na ana authority coz Baba ameshindwa kuongoza familia.Baba yangu ndio kila kitu kwangu, huwa nashindwa kuelewa janaume zima lisipojuwa umuhimu wa Baba nadhani wengi wao ni mimba za kubambikwa hawana uhakika kama wanaowaita Baba kama ni Baba zao kweli.
Baba akifa mara nyingi familia nyingi zinasambaratika mababa wengi wako jela kwa makosa waliyofanya kutafuta pesa kuprotect family huku nje mimama inatoombwa tu.
Matola, familia zinatofautiana sana. Kuna familia mama is everything, Kuna familia mama ni bread winner na ana authority coz Baba ameshindwa kuongoza familia.
Kila mtoto ana hero wake kutokana na michango ya hawa wawili katika malezi tangu utoto.
Nani kama mamaa by christian bella
Ni wapi niliposema Familia zinafanana? Ulipaswa umjibu mleta mada post yako na siyo mimi.
Baba yangu na mama yangu wote wapo hai, ila hakuna kama Baba yangu.
nimebakia kumuota mama yangu kila siku now 15yrs
Hapa duniani hakuna mtu anayeishi maisha magumu kama yule aliyefiwa na mama yake mzazi.
Ni bora ya mtu asiye na pesa, atahangaika atatafuta na ipo siku atazipata hata kama ni uzeeni atapata tu lakini ukimpoteza mama ndio imetoka hiyo. Mama hautaweza kumtafuta, mama hana mbadala, mama ni mmoja tu, ukimkosa huyo uliyenae hutampata mama mwingine.
Mtu asiye na mama anakuwa kwenye wakati mgumu sana hasa nyakati za:
1. GRADUATION 2. HARUSI 3. MAFANIKIO 4. WAKATI WA SHIDA (Karibia nyakati zote tu kiukweli)
Katika hayo matukio ndio ambapo kila mtu anamkumbuka sana mama yake, utakapokuwa kwenye harusi unatamani mama yako angekuwepo, utakapokuwa kwenye graduation unawish mama yako angekuona unapomaliza chuo.
Mtu anapomzungumzia mama yake basi nawewe unatamani mama yako angekuwepo, mtu akipigiwa simu na mama yake unatamani mama yako angekuwepo labda angekupigia simu.
Mtu asiye na mama kila akikumbuka mama yake alipokuwa akimuita, akimfulia nguo, akimnyooshea nguo, akimuwekea chakula na kumfundisha mambo mengi ya kimaisha ataishia kulia tu.
Uchungu wa kumkosa mama hauna kifani wanajamiiforums, ukimkosa mama unaweza ukajiuliza unaishi ili iweje sasa?
POLENI WOTE MLIOFIWA NA MAMA ZENU PIA NISAMEHENI KWA KUWAKUMBUSHA MACHUNGU NA KUWATOA MACHOZI.
Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)
Don't be hostile for no reason..! Umesema huelewi janaume zima lisiloelewa umuhimu wa baba ndani ya nyumba...what does that translate into?
Huwezi kupata 100% katika dunia hata uwe jiniazi kiasi gani wacha kujidanganya.
So he is..!Tafsiri unavyoweza Baba yangu is my number one
So he is..!
But not everyone's dad is an icon..!
Asante sana WalimweusiPole sana