Kila mmoja wetu anahitaji upendo au kupendwa....ni jambo lenye kuleta hisia za kupendeza kuwa na mtu maishani mwako ambaye kwa upendo wake wewe unapata sababu ya kuishi na kuyatazama maisha katika hali ya kupendeza....kosa kubwa kwenye mapenzi ni kuviweka kwenye mzani mmoja MAPENZI na MALI...wakati mwingine tunatakiwa tuziache nyoyo zetu ziamue....kwani si kila wakati kwenye maisha tunahitaji fedha na mali kukamilisha furaha zetu..bali kuna wakati kuwa tu karibu na tuwapendao ni zaidi ya raha maishani...ni raha kwa sababu kila tukiwa nao na raha tuzipatazo tunajihisi kama tumeshapata kila kitu maishani
I hope mapenzi unamanisha matashi mema, kujitolea kwa 100% kwa mtu mwingine, kusamehe bila kuombwa msamaha.
kama ni hivyo tuko pamoja,
Ila katika ndoa unatakiwa pamoja na hayo yote uongeze ziada kwa kuwa kiapo kilikufunga na huyo mwenzi kwa baadhi ya mambo, so inabidi auminifu binafsi na uvumilivu wa ziada. hakuna pa kupumulia kwa hio ni ngumu zaidi kuutekeleza huo upendo. Majaribu na madhaifu ni mengi.
Pia ujue kuwa pesa inapendwa tu hivi hivi, pesa husaidia kulainisha;
mfano,
- inasaidia mtu kuwa msafi au na mvuto zaidi (mashoping na mastyle huburudisha macho) mkiwa wakweli mtakubali,
- inasaidia pale mtu anapohitaji space kidogo (leo nitapitia hapa klabu kidogo ... wakati hutaki kuadress jambo kwani unajua mwenza au wewe hauko stable, bado hasira ni mbichi na unaweza kuharibu zaidi),
- inasaidia kupunguza uchovu unaopelekea stress na mikwaruzo isio na maana, huweka wasaidizi, kufurahia sikukuu na kusafiri kusaidia ndugu kwa pesa nk.
Ila kama tujuavyo pesa haitoshi, na sio msingi wa maisha ya ndoa. pesa nyingi kwangu mfano 10,000 sio lazima iwe nyingi kwako. swala hapa ni mtazamo, hicho kiasi kwako kinakuridhisha? mimi ukinipatia kiasi cha kwenda mtumbani mara moja kwa mwezi ni kama sh 5000 kwa mwezi kwa personal effects nitakuwa naelea kwa raha, ila kwa mwingine ni kashfa.
mimi ukinipeleka beach na baiskeli yetu kila siku ya iddi nitakuwa wako milele ila mwingine bila Zurich au Trinidad unadharauliwa na kuonekana -----.