At the end fahari ya mwanamke ni mwanaume

At the end fahari ya mwanamke ni mwanaume

Hunyu

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
4,774
Reaction score
4,341
Habari za usiku huu wapendwa, natumai weekend ilikuwa poa sana.

Leo nikiwa kwenye nyumba ya ibada fulani hivi, basi kukawa na sherehe ya akina mama. Kina mama walikuwa wamejilemba wakionekana wenye furaha kwenye nyuso zao. Kilichonijia kichwani ni kwamba, wanafuraha hawa kwasababu 90% wana waume hawa.

Nikakumbuka mada nyingi zilizowahi kutolewa hapa Jamii Forums kutetea single parent family nikaanza kuzitafakari na kuona hazina ukweli wowote na kwamba kwa namna moja au nyingine zinapotosha kizazi hiki cha sasa.

Naturally, a female should be possesed by a male hiyo ndio fahari na usalama wake kutokana na alivoumbwa na mwenyezi Mungu. Mwanamke anasikia fahari, protection na safe sana akiwa na mume around, Haya mengine ni kujifariji tu hakiyanani.

Msipotoshe jamii kwasababu katika ujana mlikosea na kajikuta nje ya qualification za kuwa na familia yenye baba na mama kwa pamoja. Au kwasababu ya matakwa fulani fulani usipotoshe jamiii kuwa single parent family ndio mpango. Maana kwa upande mwingine that is selfish.

Beijing things and technology ni kati ya vyanzo vya kuwafanya wanawake wengi wajifariji kuwa inawezekana kuwa na familia zao bila kuhitaji wanaume but ukweli unabaki palepale kuwa wanawahitaji wanaume,tusiendelee kuharibu jamii.

Kama uliharibu na ikashindikana kuishi na mwenza wako basi jitahidi watoto ulionao kuwaambia ukweli sio kuwajengea chuki kuhusu mzazi mwenzio na wakajikuta wanachukia ndoa. Madhara yake ni makubwa kuliko unavojifurahisha kwa kauli unazowapandikizia watoto wako.

Turudi ktk lengo la Mungu kumuumba Adamu na Eva ambalo ni kutengeneza couple itakayotimiza makusudi ya Mungu kwa kusaidiana lakini pia kuzaa watoto watakao lelewa na wazazi wao.


 
Kaka mimi nakubaliana na wewe kwa 100%. Unajua hata hao wanaojitia tough kuwa mume hana kazi kwake na kujaribu kuwapotosha wengine deep down in their hearts they wish they chose a right man. Hakuna mwanamke asiyetamani Mume. Hilo napinga.

Kweli unafikiri wanavyolala peke yao siku baada ya siku huku wakiwaona wenzao wanamiliki waume na familia zenye upendo hawaoni wivu. Nyumba iliyokosa baba hata malezi ya watoto huwa yanakuwa mabovu tu. Mume ni muhimu kwao na hilo wanalijua sema pale mume anapokosekana ndio huwa hawakawii kutoa kauli za kujifariji.
 
Ofcoz huwa najihic beuriful nkiwa na a real nan
 
Hilo nalo neno....

Mm nawaangalia tu wanaojifariji kuwa ndoa sio lolote wala sio chochote, hata wapinge vp lakn ukweli utabaki palepale.
 
Wanawake, kubalini kuolewa mitala, wanaume wenyewe siku hizi wachake

Unajua kwanini mko wachache?ni kwasababu mnajiua kila siku kwa kuwa na wanawake lukuki! eti mnatukomoa! wakati sisi tunapokea nyinyi mnatoa! unajua lita unazopoteza za protini kwa bao moja unalopiga?likewise unajua kazi ya protini mwilini?
Mungu hakuwaumba wachache hata kidogo hiyo pamoja na sababu nyingi ndizo zinawaondoa duniani matokeo yake mtatuacha tunajinenepea
 
Hunyu

Mtoa mada unashangaza unapoangalia upande mmoja. Umeshajiuliza kama wewe unaweza ishi bila mwanamke? Na wewe pia unajisikia raha unapokuwa na kiumbe cha kike infact huwezi kuishi bila mwanamke huwezi! si bora wanawake wanajaribu kuendesha familia zao wenyewe nyie mnaweza. kwa hiyo usijishaue bure kwa kuwa kila mtu anamuhitaji mwenzie.

Kinachotokea wanawake kuamua kuishi peke yao ni kuwa wamekosa upendo ule mlioamuliwa kuwapenda hao viumbe mmekuwa waongo na wadanganyifu kwao that's why
 
Last edited by a moderator:
Si kila mwanaume ni fahari ya mwanamke bali ni yule mwanaume anayetambua thamani ya mwanamke na kujua kuwa mwanamke anataka nini na kwa wakati gani na kumtimizia kwa wakati muafaka mahitaji yake...ni yule mwanaume anayemuheshimu mwanamke si tu kwa uanamke wake bali tu kwa mazuri anayomtendea.....ni yule anayejua kuwa mwanamke ni malikia na anaonyesha umalikia wake kwa vitendo......
 
Hii thread imenifanya nitafakari na nikumbuke mambo mengi
Kila mwanamke anahitaji mwanaume awe ubavuni mwake unaposema unataka kuwa single parent kuna muda unaweza ukawa na vyote lakini moyo una uhitaji bado . hakuna kitu kibaya kama upweke .unaweza kuwa na mtoto wako lakini bado ukajiona hujakamilika kuwa na family, kuishi kama family kuna raha sana
 
Hakuna starehe inayokamilika kwa mwanaume bila mwanamke
 
Back
Top Bottom