Pole sana kwa mihangaiko yote hii.Nadhani kwa mizigo inayotoka Uingereza kuja Tanzania kwa wakati huu inashughulikiwa na kampuni binafsi iyayoitwa Priority Mail ambayo ofisi zake ziko uwanja wa ndege wa Mwl. JKNIA. Kwakuwa wewe ni mteja, unayo haki na wajibu wa kuhakikisha unapata haki yako.Huduma bora ni haki yako. Kwa ushauri wangu endelea kufuatilia katika ngazi za juu ikiwa ni pamoja na kuwaona mameneja wa ngazi za juu wa Posta hadi kwa mtendaji mkuu.Kumbuka uwe na particulars ikiwa ni pamoja na nambari za ufuatiliaji za mizigo yako ili uwarahisishie ufuatiliaji na nina imani watakusaidia.Kumbuka huitaji ruksa au kibali cha kuwaona hao viongozi bali ni utashi na ujasiri wako tu wa kufuatilia haki yako.Nina imani utaweza kupata mwanga au suluhisho la suala lako.