Vincent Cosmas Mwagala, Askofu wa Jimbo Katoliki la Mafinga “Mafingensis" atazungumza na vyombo vya habari, kesho, 30.09.2025 saa 4 asubuhi na kutoa taarifa mintaarafu kuhusu Padre Jordan Kibiki
24.09.2025 Kamanda wa Polisi (RPC) Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi aliwaeleza waandishi wa habari kwamba kwa mujibu wa uchunguzi wao, walibaini Padre Jordan Kibiki alijiteka kwa kuwa alizidiwa na madeni.
Kwamba, Padre Jordan Kibiki wa kanisa Katoliki Jimbo la Mafinga hakutekwa na kupotea kama ilivyoelezwa. Bali alitoa taarifa za uongo kupitia WhatsApp akidai ametekwa na kusafirishwa kwenda Mbeya.
Kamanda wa Polisi (RPC) Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi alisema baada ya uchunguzi wa polisi alikutwa Mbalizi, Mbeya. Padre Jordan Kibiki ni padre katika Kanisa la Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, Mafinga..
Polisi walimkata na kumshikilia Padre Jordan Kibiki. Polisi wakamuhoji kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo kupitia mitandao ya kijamii. Polisi wakasema watamfikisha Mahakamani..
Kwa kuwa polisi wametoa taarifa yao wakikanusha taarifa ya Padre Jordan Kibiki, kesho ni zamu ya kusikiliza taarifa ya Kanisa Jimbo Katoliki la Mafinga. Tusikie, ni kweli Padre Jordan Kibiki ALIJITEKA au ALITEKWA.
==
Pia soma >>>
GE2025 - Polisi: Padre aliyedai ametekwa, hakutekwa. Alisafiri mwenyewe kwa basi na kwenda Mbeya
View attachment 3480903