Majs
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 229
- 485
Askofu Msaidizi wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Katanga katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Elisha Tendwa amesema baadhi ya Watanzania ambao wamekuwa wakitoa malalamiko juu ya utawala wa Rais John Magufuli siku moja wangefika Congo wasingethubutu kutoa lawama hizo.
"Mimi nafanya kazi ya umishenari kule DRC, nimetumwa na Kanisa Anglikana Tanzania, ni mojawapo ya njia ya kueneza amani duniani, nina miaka mitano tangu niende huko na nimetembelea majimbo mengi nimejionea nchi ile ni tajiri na yenye rasilimali nyingi lakini watu wake wanaishi kwa hofu ya vita ni wakimbizi ndani ya nchi yao, huwezi kulinganisha na nchi kama Tanzania," amesema.
Amesema kuwa ni vema kabla ya watu kutoa lawama kwa Serikali juu ya mambo mbalimbali ni vema wakalinganisha na kufanya tathmini juu ya hali ilivyo kwa nchi nyingine ikiwemo nchi ya DRC.
"Kwanza naishukuru Serikali ya Tanzania ambayo imekuwa ikitoa mchango wake kwa hatua mbalimbali ili kurudisha amani kule Kongo na naamini ipo siku amani ya kudumu itarejea kule Congo," amesema.
Amesema kuwa hali ya maisha ya Tanzania ukilinganisha na DRC ni tofauti kwa maeneo mengi ikiwemo amani na hali ya shughuli za kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja.
Naye Ofisa Habari na Mawasiliano wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Yohana Sanga alisema kutokana na mchakato wa uchaguzi wa kumpata Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam unaoendelea, ni vema waumini wa kanisa hilo wakaacha kujiingiza kwenye makundi yenye nia mbaya.