Askofu Ruaichi: Waumini Waombeeni Viongozi Watambue Kuna Njaa

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,334
72,799
Askofu mkuu wa jimbo la Mwanza Mhashamu Thadeus Ruwaichi amewataka waumini wafunge Novena kuliombea taifa juu ya baa la ukame na njaa pia kuwaombea viongozi watambue kuwa BAA HILO LIPO NCHINI KWA SASA.

Amesema hayo katika Parokia ya Pansiasi katika ibada ya kutoa kipaimara kwa vijana wa kikristo.
Kauli hii inatutaka waumini na raia kuwaombea wale viongozi wanaosema hakuna ukame wala njaa kwa vile wameona majani ni ya kijani.

Jee Askofu mkuu naye hajui kuwa mwenye kujua kuwa kuna njaa na ukame ni mtu mmoja tuu na tusubiri mpaka atamke?

Source: Ndani ya Kanisa Pansiasi.
 
Mmmh, mwaka huu, duuh.. sms sent..!! Huu mchakamchaka mkali, huku Lowassa, kule Kanisa Katoliki, pale Mashekhe, Zitto yule kulee..

Wote wanamnyooshea vidole Mh. Rais, najiuliza, Kanisa Katoliki ni kubwa zaidi ya CCM, zaidi ya CDM, zaidi kifedha, je wao mchango wao ni nn ktk hili la njaa..? wanaangalia serikali na CCM tu..? Kama hawana mchango kutoa chakula kidogo na wana mahela kibao, wafunge mdomo, sbb nachoona ni kukosoana tu, wakati kanisa lina mahela kibao, waisaidie serikali kidogo.. hawa watu, kweli nyani ni nyani..

Rekebisha hapo ni NOVENA..!!
 
1484496906585.jpg
Hivyo ndivyo hali ilivyo huko Karagwe, Kagera 12/1/2017
 
Mbona ni kijani au tunaona je sisi wengine??
Kijani ingine inasababishwa na mvua moja au mbili,na mvua hizo ni rahisi kufanya nyasi ziwe kijani.

Mazao ya chakula kama mahindi hayatastawi mpaka kuvunwa kwa mvua moja au mbili

Hata misenyi alikowaambia eti ni pa kijani,labda kamvua kalinyesha wiki moja kabla
 
Askofu mkuu wa jimbo la Mwanza Mhashamu Thadeus Ruwaichi amewataka waumini wafunge Novena kuliombea taifa juu ya baa la ukame na njaa pia kuwaombea viongozi watambue kuwa BAA HILO LIPO NCHINI KWA SASA.
Amesema hayo katika Parokia ya Pansiasi katika ibada ya kutoa kipaimara kwa vijana wa kikristo.
Kauli hii inatutaka waumini na raia kuwaombea wale viongozi wanaosema hakuna ukame wala njaa kwa vile wameona majani ni ya kijani.
Jee Askofu mkuu naye hajui kuwa mwenye kujua kuwa kuna njaa na ukame ni mtu mmoja tuu na tusubiri mpaka atamke?
Source; Ndani ya Kanisa Pansiasi.
Sijawahi kujuta kumfahamu Ruwaichi.
Mungu azidi kumpa busara na hekima.
 
Baada ya kuzuia Bunge laivu la dodoma,sasa yamezaliwa mabunge laivu karibu mia.

Sasa wananchi wameamua kuongea wenyewe baada ya wawakilishi wao kubanwa,

Ndani ya Bunge rahisi sana kupata muafaka,huku mtaani kila mtu na lake hakuna wa kutukutanisha kutupa muafaka,

Waliotaka nchi ziwe na mabunge hawa kuwa wajinga,walijua Bunge ni coolant, breathing space kwa kero za nchi
 
Back
Top Bottom