BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
WITO KWA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUKUTANA NA CHADEMA NA ACT WAZALENDO KUTATUA TATIZO LA KUENGULIWA KWA WAGOMBEA.
Tarehe 29 Agosti 2020, nimetoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kukutana na Uongozi wa CHADEMA na ACT Wazalendo kwa lengo la kuzungumza na kutatua tatizo la kuenguliwa kwa Wagombea wa Udiwani na Ubunge kupitia vyama hivyo kulikofanywa na Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi! Nimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutafakari kwa kina na kupima kwa uzito jambo hilo kuhusiana na suala zima la kutenda HAKI kwa mustakabali wa nchi kupitia Uchaguzi Mkuu wa 28 Oktoba 2020.
Nimeyasema hayo kama maneno ya utangulizi nilipokuwa natoa Sala katika Ufunguzi wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Tundu Lissu katika Viwanja vya Tanganyika Packers vilivyoko Kawe jijini Dar es Salaam.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani