Maongezi kati ya Mwandishi wa habari na Baba Askofu Mwamakula

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
109,585
2,000
Wiki hii, Mwandishi mmoja kutoka Chombo kimoja cha Habari maarufu katika nchi za Afrika Mashariki alimhoji Askofu Mwamakula kuhusiana na "Matembezi ya Hiyari"! Ufuatao ni muhutasari (paraphrased) wa mahojiano hayo!

Simu: Tilililili! Talalilalila! Tololololo!

Askofu Mwamakula: Halo! Ninaongea na nani?!

Jibu: Naitwa .... Ni mwandishi wa habari wa...

Askofu Mwamakula:
Unasemaje?

Mwandishi: Nataka kukuhoji kuhusu "Matembezi ya Hiyari"!

Askofu Mwamakula: Karibu!

Mwandishi: Tunataka kujua kama "Matembezi ya Hiyari" yamepata kibari kutoka Kanisa la ....!

Askofu Mwamakula: Kanisa halihusiki katika kuandaa kwa kuwa yanaandaliwa na Askofu kwa nafasi yake. Askofu anao wajibu kwa watu wote wakiwemo hata wapagani!

Mwandishi:
Tunataka kujua majimbo mengine ya Kanisa la ....yatashirikije!

Askofu Mwamakula: Hili siyo suala la Kanisa la ....! Ni suala la Watanzania wote pasipo kujali dini zao au makabila yao!

Mwandishi: Sasa mnadai Katiba Mpya, kwa nini msiende Mahakamani?

Askofu Mwamakula: Mahakama zetu ni zao la Katiba iliyopo kwa hiyo haziwezi kujipinga na wala haziwezi kwenda kinyume na Katiba iliyopo!

Mwandishi: Tena mnadai Tume Huru ya Uchaguzi, kwani iliyopo ina shida gani?

Askofu Mwamakula: Mimi ni shabiki wa Simba, wewe?

Mwandishi: Yanga!

Askofu Mwamakula: Simba ndiyo mabingwa watetezi! Unaonaje kama wao ndio wangeteua TFF, wateue marefa, wateue makamisaa, nk?

Mwandishi: Ha ha ha! Haiwezekani!

Askofu Mwamakula: Kwa hiyo Tume iliyopo ni huru?

Mwandishi: Ha ha ha! Siyo Huru!

Mwandishi:
Unawaambiaje wanaokukosoa kuwa unachanganya dini na siasa?

Askofu Mwamakula: Hivi watu wanapouana kutokana na vurugu za Uchaguzi kutokana na ufinyaji wa haki na upendeleo Askofu haitwi kuendesha ibada za mazishi?

Mwandishi: Anaitwa!

Askofu Mwamakula: Askofu akiwaambia watu kuwa ili kuepuka kuuana ni vizuri tutengeneze mfumo wa haki utakaozuia mauaji atakuwa anakosea?!

Mwandishi:
Hapana!

Askofu Mwamakula:
Kuna swali lingine?!

Mwandishi: Hakuna Baba Askofu, kama tukikuhitaji tena tutakutafuta!

Askofu Mwamakula:
Hakuna shida! Karibu!
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,791
2,000
Kwani askofu Mwamakula hamuamini Robert Amsterdam wa Chadema kwamba atatuletea katiba mpya kupitia ICC?
 

mlimilwa

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,334
2,000
Hahahahahahahahahahahahahahaha...

Mwamakula ni nyoko huyo.
Siku ingine mwandi akitumwa amuhoji huyo mzee atajihudhuru na uwandishi siku hiyohiyo.
 

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
289
500
MWANDISHI.....hewa!

Mleta topic ......Mwamakula.

Msanifu ....Bandekile

Platform ......jamiiforums

Picha inaendelea vema ukaanza kumeza dawa za maumivu mapema ili zitangulie mwilini.

Labda zitakusaidia siku hiyo.
 

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
937
1,000
Huyo mwandishi wa habari hana akili kabisa.cheti chake kichunguzwe

Halafu huyo anayejiita askofu hajui kazi yake.Katiba za makanisa zinatakiwa kuhakikiwa vizuri.askofu huyu ajifunze kufuata katiba ya kanisa lake.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,152
2,000
Mwandishi: Tunataka kujua majimbo mengine ya Kanisa la ....yatashirikije!
Askofu Mwamakula: Kwa hiyo Tume iliyopo ni huru?

Mwandishi: Ha ha ha! Siyo Hur

Askofu Mwamakula: Askofu akiwaambia watu kuwa ili kuepuka kuuana ni vizuri tutengeneze mfumo wa haki utakaozuia mauaji atakuwa anakosea?!
Kwanza Askofu mkuu hatakiwi kutoa tamko lisiloshirikisha vikao cha viongozi wa majimbo kwenye maswala ya kitaifa

Pili Askofu hatakiwi kushauri sijui kutengeneza mfumo ya haki yeye wanatakiwa tu kuhubiri watu watubu na kuiamini Injili mtu aliyetubu na kuiamini Injili huwa mtu wa haki automatically akisha kuwa mtu wa haki atatenda haki automatically

Yesu ni jibu aliacha jibu la kumaliza migogoro yote duniani kuwa ihubiriwe Injili ya kutubu na kuiamini injili kama solution hakutuma kitu kingine Askofu Mwamakula ni mpotofu kapotoka kuacha wito kanisa lake wamtimue
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
4,434
2,000
Kwanza Askofu mkuu hatakiwi kutoa tamko lisiloshirikisha vikao cha viongozi wa majimbo kwenye maswala ya kitaifa....
Kwa hiyo Askofu kutoa tamko la kulaani ukandamizaji wa demokrasia Tanzania mpaka pawepo na kikao? haki ya kutoa maoni yake iliyopo kisheria unataka aitumie wapi?

Wacha kutupigia kelele.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,152
2,000
Kwa hiyo Askofu kutoa tamko la kulaani ukandamizaji wa demokrasia Tanzania mpaka pawepo na kikao? haki ya kutoa maoni yake iliyopo kisheria unataka aitumie wapi?
Askofu ni Askofu ndani ya kanisa na nje ya kanisa hana maoni binafsi maoni yake yanatakiwa kuwa ya Mungu masaa 24

Mtume Paulo alitamka wazi kuwa baada ya wito kuitwa kuwa mtumishi wa Mungu alitamka wazi kuwa sio Mimi tena bali ni Kristo .Umimi umesulubishwa

Anachofanya Mwamakula hajui wito kuwa ukiitwa na Kristo u Mimi unasulubiwa

Maoni binafsi hayana nafasi

Askofu Mwamakula ni mpagani aliyevaa joho la uaskofu
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,152
2,000
Kwa hiyo Askofu kutoa tamko la kulaani ukandamizaji wa demokrasia Tanzania mpaka pawepo na kikao? haki ya kutoa maoni yake iliyopo kisheria unataka aitumie wapi?

Wacha kutupigia kelele.
Yesu alitaka kuwa mtume na viongozi wake si wa huu ni mabalozi wake duniani

Kama balozi hatakiwi kuingilia mambo ya ndani ya nchi yeyote duniani sababu so raia wa nchi yeyote anatakiwa aseme kile alichotumwa na nchi yake iliyomtuma ambacho ni tubuni na kuiamini injili
 

Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Feb 10, 2017
1,836
2,000
Wiki hii, Mwandishi mmoja kutoka Chombo kimoja cha Habari maarufu katika nchi za Afrika Mashariki alimhoji Askofu Mwamakula kuhusiana na "Matembezi ya Hiyari"! Ufuatao ni muhutasari (paraphrased) wa mahojiano hayo!...


Amakweli nyuzi za leo ni FACT COMEDY mbavu zangu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom