Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Magufuli, Majaliwa, Janet Magufuli. Mwita Waitara. Lukuvi, nk ni waalimu kitaaluma wameacha chaki wamekimbilia kwenye siasa. Je wamechanganyikiwa?
 
Jeshi la Polisi linamkamata mtu na kumuweka ndani na baada ya kelele nyingi kutoka kwa jamii, mtuhumiwa huandaliwa mashtaka.

Jamhuri inamtuhumu na kumshtaki kwa makosa mbalimbali mazito yasiyodhaminika. Baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kesi hutajwa lakini kesi huahirishwa na mtuhumiwa anaambiwa hawezi kujibu lo lote kwa kuwa 'upelelezi unakuwa bado haujakamilika'!

Kila inapofikia tarehe ya kesi kutajwa, waendesha mashtaka wa Serikali huiambia Mahakama kuwa kesi bado haijakamilika na Hakimu au Jaji hulazimika kuiahirisha tena kesi hadi tarehe nyingine. Huo ndio unakuwa mwanzo wa mateso na kukomolewa kwa mtuhumiwa. Biashara zake na kazi zake huathiriwa vibaya sambamba na familia yake achilia mbali afya yake kuathiriwa akiwa mahabusu!

Inaonekana katika nchi yetu, sisi sote tunakosa ujasiri wa kuhoji ukiritimba huu wa Sheria zetu unaochochewa na watendaji wenye husuda na roho mbaya wanaotumia mwanya wa vipengere kandamizi vya Sheria zetu na hivyo kuwatesa na kuwakomoa wale wasiopatana nao ndani na nje ya mfumo wa Serikali.

Haki yoyote iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokataliwa (justice delayed is justice denied). Hivyo, kuchelewesha kusikiliza kesi za waliotuhumiwa huku wakiachwa kusota mahabusu ni sawa na kuwacheleweshea na kuwanyima haki yao.

Kwanini umkamate mtu na kumtuhumu na kisha kumshtaki lakini unamuweka mahabusu miezi na hata miaka kwa kisingizio cha upelelezi kutokukamilika katika zama hizi?

Hivi ni kiongozi gani au mamlaka gani inayoweza kufidia hasara za mtuhumiwa aliyecheleweshewa haki hadi kuathirika na kupata magonjwa hadi kifo? Mambo haya yanaumiza sana moyo wangu kwani kwa njia hii watu wengine husigina haki za wengine.

Mambo haya hayatakiwi kufanyika katika nchi inayosadikika kuwa na idadi kubwa ya waumini wa dini zinazofundisha kuhusu haki na upendo ikiwemo dini ya Kikristo. Hasira ya Mungu iko dhahiri kwa mtu mmoja mmoja, jamii au taifa lo lote ambalo watawala na viongozi wake husigina haki za wengine (Amos 5:1-27).

Wiki hii ninawaombea wale wote ambao bado wako mahabusu wengine hata miaka kadhaa kwa sababu upelelezi wa kesi zao 'haujakamilika'.

Ninawaomba wahusika yaani washitaki na wale wote wanaohusika na uendeshaji pamoja na 'upelelezi' wa kesi hizo waingiwe na utu na roho ya huruma huku wakijua kuwa hata wao wenyewe ni wakosefu pia kwa namna moja au nyingine. Ninaomba watu wengine tuungane katika maombi haya lakini kikubwa zaidi tuungane katika kupaza sauti zetu kwa mamlaka husika.

Ninawaomba Mahakimu na Majaji katika Mahakama zetu hasa wale wanaosikiliza kesi za namna hiyo kuwa wakali kwa waendesha mashtaka na wapelelezi 'wanaoonekana kucheza mchezo wa kuchelewesha kesi'. Hakimu au Jaji ni mdau muhimu sana katika upatikanaji wa haki kwa wakati.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
Thanks so much, asante sana baba askofu, mungu wa abraham, isaac and jacob akupe maisha marefu na afya jema na akuongeze usujaa wa kuwatetea wanyonge,Mimi naona hii ni ukatili na uyama unayofanywa na hii serikali ya awamu ya 5, huwezi fikisha mtu mahakamani kaa hujakamilisha uchunguzi, maana ndio umusitaki mtu unafanya huo uamuzo kulingana na ile ushahindi ambao uko nae na ambao tayari umeukusaya, cha ajabu unafikisha mtu kortini huna ushahindi sababu huna uchunguzi kamili kisha unaomba korti iahirishe hii kesi mara kadhaa, wakati wingine miaka, kaa ile kesi ya mashee, katika mataifa ambayo inaheshimu haki na binadamu , mtu hufikiswa kortimni pale ushahidi upo , yaani uchunguzi umekamilika, sasa ona vile huyu ndugu yetu kabedera anavyoteseka na kila mara akiletwa kortini uchunguzi unasemekana bado haujakamilika, JE HII NI HAKI KWELI???? asante tena baba askofu kwa kuliongea hili, asante kwa kuwa tofauti na "MAASKOFU NA WACHUNGAJI NA MITUME WENGINE" ambao kazi yao siku hizi imekuwa ni kupigia ccm magoti na kuisifu bila kuona ile maovu inatendwa na ccm. Kweli siku ya mwisho yesu atasema, ONDOKENI KWANGU SIWAJUI HATA KIDOGO, barikiwa sana baba askofu, na kweli MWANA KONDOO AMESHINDA KIFO NA MAUTI
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Unataka kumaanisha nini?????? palöe haki ya binadamu inavujwa tusiongee????? Je unaifahamu kazi ya askofu au mchungaji ni gani???ß wewe enda kwa kina kakombe, gwajima na mwingila, hao ndio wanapiga makofu pale watu wanaumizwa, Sisi weye roho ya ubinadamu tutaongea mpaka maovu YAKOME!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ni kufanya vizuri kwenye eneo lako la specializatio.

Mfano mleta mada Ni Askofu ambaye ukimwambia onyesha Makanisa yako hata matatu tu yalipo dar es salaam anaingia mitini na kutokomea gizani.Kwake hakujaendelea Hana matawi.

Kwa mkulima maendeleo ni kuongeza uzalishaji na kuongeza kipato kupitia kilimo.
hapo ndipo uwezo wako wa kufikiria umefika wewe mwana UVCCM????????????????????????
 
Hayana maana yoyote ubaguzi aliopiigania wa kijinga kabisa alipigania wazungu wasibague waafrika ili waafrika kusini weusi wajinafasi kubagua waafrika wenzao wa nchi zingine.Umeshaona Afrika kusini mzungu yeyote anafukuza waafrika na kuchoma maduka ya waafrika weusi? Desmond Tutu alipigania Vita ya kijinga sababu Afrika kusini ubaguzi ni.mkubwa wa waafrika kusini weusi kuwabagua waafrika wenzao weusi wa nchi zingine.Angebaki tu Kanisani kusalisha sababu Hakuna ubaguzi alioumaliza
Kweli Yehodaya umelewa upuuzi. Wanachokifanya wale weusi wa South Africa ni sawa uvccm wanavyofanya dhidi ya watu wa itikadi tofauti. Tena bora wao wanafanya hadharani, tofauti uvccm wanavyofanya kwa kujificha (wasiojulikana).
 
Kwahiyo kwa maoni yako siasa waachiwe wanasiasa tu sisi wengine tujikitenkwenye taaluma yetu
Hivi mtume Issa ajulikanaye kama Emmanuel, Yesu Kristo alisema ya kaisari mpeni kaisari na ya Mungu mpeni Mungu alikuwa na maana gani?
 
Wasio na taaluma wachape kazi wapi?
Ndio.Ndio maana huwa tunapiga kura kuchagua madiwani na Wabunge ili wao wawakilishe mawazo yetu huko.mbele sisi tuendelee kuchapa kazi kwenye taaluma zetu
 
Askofu ameongelea haki,wengi tunaweza tusione hili kwa kuwa hatukuwai kutendewa uovu wa namna hiyo. Hatukuwai kubambikiwa kesi au kuwa na mtu wa karibu kubambikiwa kesi. Lakini viongozi hawa wa dini wanapaswa kukemea pale haki inapominywa au kunyimwa. Leo upo unakula maisha uwezi kujua machungu ya wale ambao wamo ndani kwa kwakuwa mtu fulani ameamua iwe hivyo. Tunajenga misingi itakayokuja kutuangamiza.
 
Ni ukatili wa hali ya juu kumuweka MTU ndani then ndo unaanza kuutafuta ushahidi na mahakimu wanakenua meno tu.
 
Uoga wa kukaa kimya ni sawa na uasi kwa Mungu. Biblia inawataka Maaskofu kupaza sauti kukemea matendo maovu.

Ole wao wale wanaotupigia kelele mitaani kukemea mspepo na kuacha kuhubiri kweli ya Yesu.

Tunamkumbuka yule mwanamke aliyeshitakiwa kwa kufanya umalaya. Yesu alimsaidia pale alipoinama na kuandika dhambi za wale waliomzingira kwa Nia ya kutaka kumuua.

Leo tunaishi kwa kukomoona na hakuna kiongozi was dini MWENYE uthubutu kukemea. Bora askofu umenena
Mkuu muda mwingine mnakosea kwa taarifa yako si kila kiongozi wa dini anayekemea ni wa kweli wengine wana agenda zao za siri.Kiongozi wa dini anayemjua Mungu vizuri huongozwa na Roho Mtakatifu na si kwa matukio na hisia zake mwenyewe.Kwa hiyo viongozi wengine wanaweza wasifanye hivyo unavyotaka wewe wawafanye kwani Mungu hajawaambia wafanye.Ushauri wangu kwako ,hao wanaofanya kawaulize ni Mungu amewaagiza mfanya hayo au ni akili zenu na matukio?
Mnalaumu viongozi wa dini wamekaa kimya,je kama wako wanaombea hayo mambo na hawapendi publicity?Kuna viongozi wa dininawaangalia wanatumia vibaya idadi za memebers walio nao wakizani ni wao kumbe ni wa Mungu.Kwa imani yetu sisi wakristo kila mamlaka inatoka kwa Mungu,kwa hiyo kama kuna tatizo lolote juu ya mamlka husika tunaenda kwa aliyeiweka ambaye ni Mungu.Pia waulize wanapokemea publically ni Mungu anakuwa amewaambia wakemee publically au ni akili zao?Kama Mungu anataka ufikishe ujumbe kwa kiongozi yeyote atakuwekea mazingira ya kiongozi yule kukutana na wewe au ukiomba kuonana naye hakataliwa.
Kuna mtu anaweza akawa anajiita au anaitwa mtumishi wa Mungu duniani lakini Mungu hamtambui,kiongozi yeyote wa dini ya kikristo akianza maneno maneno na serikali ambayo kwa mujibu wa biblia kila mamlaka inatoka kwa Mungu inabidi uwe naye makini.Wakristo hawafundishwi kujipigania wanafundishwa kumtegemea Mungu awapigania muda mwingine Mungu anaweza kuwapigania kwa namna kusiko kwa kibinadamu.Biblia katika kitabu cha efeso inasema vita vyetu si juu ya damu na nyama.Lakini pia inashangaza ukiona mkristo anapigana vita vya kimwili,hapa nielezeee yamkini kuna watu hawajaelewa,siku moja Mungu alituambia tunapigana vita kimwili kwa sababu tulikuwa tunamwangalia mwenye tatizo.
Kama kiongozi anashida,unachotakiwa kujua ipo roho nyuma ya hiyo shida au tabia au chochote anachofanya,unachotakiwa siyo kupigana na huyo kiongozi au kumsema vibaya bali upambane na roho inayosababisha hayo matatizo na siyo mtu anayetenda.
Kuna watu hamjanielewa,kama unaona haki haipo Tanzania,usipambane na mahakimu na watawala bali pambana na Roho zinazowafanya mahakimu,polisi na watawala wafanye hayo wanayofanya.Ukilijua hili huwezi kumpoint mtu,anyway yamkini hii elimu ni ya level ya juu kuliko uelewa wa wengi.Si lazima unielewe leo unaweza nielewa baada ya wiki,mwezi au miaka.
Ushauri kwa wakristo(naongelea wakristo kwa sababu imani zingine wanautaratibu wao na njia zao) kama kuna tatizo lolote katika nchi wakumkimbilia ni Mungu.haijalishi watu watasema mmekuwa "brain washed" care not.Ukianza kutumia akili zako,Mungu huwa anakuacha upambane mwenyewe.
Kuweni makini sana na wanaojiita watumishi wa Mungu wakiyatumia maandiko kwa interest zao,unapoamua kutumia njia zako maana yake Mungu ameshindwa.Wewe kama ni mtumishi wa Mungu kweli always jiulize swali hili,hicho unachofanya Mungu amekuambia ukifanye?
Wito:kama kuna mtu hujampokea Yesu,saa nma wakati wa wokovu ni sasa,kuna mambo mengi siwezi kuyaandika hapa lakini niseme tu,muda uliopoteza klwenye maisha yakumchukiza Mungu unatosha .Amua leo umpokee Yesu afanyike kuwa Bwana na mwokozi wako,dini bila Yesu haina msaada kwako.
 
Jeshi la Polisi linamkamata mtu na kumuweka ndani na baada ya kelele nyingi kutoka kwa jamii, mtuhumiwa huandaliwa mashtaka.

Jamhuri inamtuhumu na kumshtaki kwa makosa mbalimbali mazito yasiyodhaminika. Baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kesi hutajwa lakini kesi huahirishwa na mtuhumiwa anaambiwa hawezi kujibu lo lote kwa kuwa 'upelelezi unakuwa bado haujakamilika'!

Kila inapofikia tarehe ya kesi kutajwa, waendesha mashtaka wa Serikali huiambia Mahakama kuwa kesi bado haijakamilika na Hakimu au Jaji hulazimika kuiahirisha tena kesi hadi tarehe nyingine. Huo ndio unakuwa mwanzo wa mateso na kukomolewa kwa mtuhumiwa. Biashara zake na kazi zake huathiriwa vibaya sambamba na familia yake achilia mbali afya yake kuathiriwa akiwa mahabusu!

Inaonekana katika nchi yetu, sisi sote tunakosa ujasiri wa kuhoji ukiritimba huu wa Sheria zetu unaochochewa na watendaji wenye husuda na roho mbaya wanaotumia mwanya wa vipengere kandamizi vya Sheria zetu na hivyo kuwatesa na kuwakomoa wale wasiopatana nao ndani na nje ya mfumo wa Serikali.

Haki yoyote iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokataliwa (justice delayed is justice denied). Hivyo, kuchelewesha kusikiliza kesi za waliotuhumiwa huku wakiachwa kusota mahabusu ni sawa na kuwacheleweshea na kuwanyima haki yao.

Kwanini umkamate mtu na kumtuhumu na kisha kumshtaki lakini unamuweka mahabusu miezi na hata miaka kwa kisingizio cha upelelezi kutokukamilika katika zama hizi?

Hivi ni kiongozi gani au mamlaka gani inayoweza kufidia hasara za mtuhumiwa aliyecheleweshewa haki hadi kuathirika na kupata magonjwa hadi kifo? Mambo haya yanaumiza sana moyo wangu kwani kwa njia hii watu wengine husigina haki za wengine.

Mambo haya hayatakiwi kufanyika katika nchi inayosadikika kuwa na idadi kubwa ya waumini wa dini zinazofundisha kuhusu haki na upendo ikiwemo dini ya Kikristo. Hasira ya Mungu iko dhahiri kwa mtu mmoja mmoja, jamii au taifa lo lote ambalo watawala na viongozi wake husigina haki za wengine (Amos 5:1-27).

Wiki hii ninawaombea wale wote ambao bado wako mahabusu wengine hata miaka kadhaa kwa sababu upelelezi wa kesi zao 'haujakamilika'.

Ninawaomba wahusika yaani washitaki na wale wote wanaohusika na uendeshaji pamoja na 'upelelezi' wa kesi hizo waingiwe na utu na roho ya huruma huku wakijua kuwa hata wao wenyewe ni wakosefu pia kwa namna moja au nyingine. Ninaomba watu wengine tuungane katika maombi haya lakini kikubwa zaidi tuungane katika kupaza sauti zetu kwa mamlaka husika.

Ninawaomba Mahakimu na Majaji katika Mahakama zetu hasa wale wanaosikiliza kesi za namna hiyo kuwa wakali kwa waendesha mashtaka na wapelelezi 'wanaoonekana kucheza mchezo wa kuchelewesha kesi'. Hakimu au Jaji ni mdau muhimu sana katika upatikanaji wa haki kwa wakati.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
Askofu wa kanisa feki,Moravian hatuna kanisa kwa jina kama hilo.Hata kwao huyo Mwamakula huko Itunge Kyela hakuna hilo kanisa.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Mawazo mflisi kabisa ya mtu aliyekula Maharage ya jana!!!!!!
 
Yesu alitamka wazi kabisa utawala wangu SI wa dunia hii.Ukiona Askofu anajihusisha na mambo ya utawala wa dunia hii huyo SI Askofu wa Yesu
Nilikuwa sijui kumbe na wewe ni POYOYO wa kutupwa!!!Hufai kabisa hata kutumika popote!!!!.
 
Back
Top Bottom