Askofu Mwamakula: Ole kwa Taifa lisilotenda HAKI kwa watu wake! Unamkamata mtu eti upelelezi haujakamilika karne hii?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Jeshi la Polisi linamkamata mtu na kumuweka ndani na baada ya kelele nyingi kutoka kwa jamii, mtuhumiwa huandaliwa mashtaka.

Jamhuri inamtuhumu na kumshtaki kwa makosa mbalimbali mazito yasiyodhaminika. Baada ya mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kesi hutajwa lakini kesi huahirishwa na mtuhumiwa anaambiwa hawezi kujibu lo lote kwa kuwa 'upelelezi unakuwa bado haujakamilika'!

Kila inapofikia tarehe ya kesi kutajwa, waendesha mashtaka wa Serikali huiambia Mahakama kuwa kesi bado haijakamilika na Hakimu au Jaji hulazimika kuiahirisha tena kesi hadi tarehe nyingine. Huo ndio unakuwa mwanzo wa mateso na kukomolewa kwa mtuhumiwa. Biashara zake na kazi zake huathiriwa vibaya sambamba na familia yake achilia mbali afya yake kuathiriwa akiwa mahabusu!

Inaonekana katika nchi yetu, sisi sote tunakosa ujasiri wa kuhoji ukiritimba huu wa Sheria zetu unaochochewa na watendaji wenye husuda na roho mbaya wanaotumia mwanya wa vipengere kandamizi vya Sheria zetu na hivyo kuwatesa na kuwakomoa wale wasiopatana nao ndani na nje ya mfumo wa Serikali.

Haki yoyote iliyocheleweshwa ni sawa na haki iliyokataliwa (justice delayed is justice denied). Hivyo, kuchelewesha kusikiliza kesi za waliotuhumiwa huku wakiachwa kusota mahabusu ni sawa na kuwacheleweshea na kuwanyima haki yao.

Kwanini umkamate mtu na kumtuhumu na kisha kumshtaki lakini unamuweka mahabusu miezi na hata miaka kwa kisingizio cha upelelezi kutokukamilika katika zama hizi?

Hivi ni kiongozi gani au mamlaka gani inayoweza kufidia hasara za mtuhumiwa aliyecheleweshewa haki hadi kuathirika na kupata magonjwa hadi kifo? Mambo haya yanaumiza sana moyo wangu kwani kwa njia hii watu wengine husigina haki za wengine.

Mambo haya hayatakiwi kufanyika katika nchi inayosadikika kuwa na idadi kubwa ya waumini wa dini zinazofundisha kuhusu haki na upendo ikiwemo dini ya Kikristo. Hasira ya Mungu iko dhahiri kwa mtu mmoja mmoja, jamii au taifa lo lote ambalo watawala na viongozi wake husigina haki za wengine (Amos 5:1-27).

Wiki hii ninawaombea wale wote ambao bado wako mahabusu wengine hata miaka kadhaa kwa sababu upelelezi wa kesi zao 'haujakamilika'.

Ninawaomba wahusika yaani washitaki na wale wote wanaohusika na uendeshaji pamoja na 'upelelezi' wa kesi hizo waingiwe na utu na roho ya huruma huku wakijua kuwa hata wao wenyewe ni wakosefu pia kwa namna moja au nyingine. Ninaomba watu wengine tuungane katika maombi haya lakini kikubwa zaidi tuungane katika kupaza sauti zetu kwa mamlaka husika.

Ninawaomba Mahakimu na Majaji katika Mahakama zetu hasa wale wanaosikiliza kesi za namna hiyo kuwa wakali kwa waendesha mashtaka na wapelelezi 'wanaoonekana kucheza mchezo wa kuchelewesha kesi'. Hakimu au Jaji ni mdau muhimu sana katika upatikanaji wa haki kwa wakati.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana, injinia afanye Kazi za uinjinia Sana, askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
 
Ni kufanya vizuri kwenye eneo lako la specializatio.

Mfano mleta mada Ni Askofu ambaye ukimwambia onyesha Makanisa yako hata matatu tu yalipo dar es salaam anaingia mitini na kutokomea gizani.Kwake hakujaendelea Hana matawi.

Kwa mkulima maendeleo ni kuongeza uzalishaji na kuongeza kipato kupitia kilimo.
Kwahiyo kwa maoni yako siasa waachiwe wanasiasa tu sisi wengine tujikitenkwenye taaluma yetu
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana,injinia afanye Kazi za uinjinia Sana,Askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Kiongozi yeyote wa dini akifumbia maovu Ni heri aachane Na uongozi wa dini akalime
 
Ni kufanya vizuri kwenye eneo lako la specializatio.

Mfano mleta mada Ni Askofu ambaye ukimwambia onyesha Makanisa yako hata matatu tu yalipo dar es salaam anaingia mitini na kutokomea gizani.Kwake hakujaendelea Hana matawi.

Kwa mkulima maendeleo ni kuongeza uzalishaji na kuongeza kipato kupitia kilimo.
Ni hoja ya kitoto sijapata kuiona mkuu
 
Kwahiyo kwa maoni yako siasa waachiwe wanasiasa tu sisi wengine tujikitenkwenye taaluma yetu
Ndio.Ndio maana huwa tunapiga kura kuchagua madiwani na Wabunge ili wao wawakilishe mawazo yetu huko.mbele sisi tuendelee kuchapa kazi kwenye taaluma zetu
 
Uoga wa kukaa kimya ni sawa na uasi kwa Mungu. Biblia inawataka Maaskofu kupaza sauti kukemea matendo maovu.

Ole wao wale wanaotupigia kelele mitaani kukemea mspepo na kuacha kuhubiri kweli ya Yesu.

Tunamkumbuka yule mwanamke aliyeshitakiwa kwa kufanya umalaya. Yesu alimsaidia pale alipoinama na kuandika dhambi za wale waliomzingira kwa Nia ya kutaka kumuua.

Leo tunaishi kwa kukomoona na hakuna kiongozi was dini MWENYE uthubutu kukemea. Bora askofu umenena
 
Ninavyojua mtuhumiwa akikaa je anaweza kuvuruga ushahidi....ndiyo maana huwa wakati mwingine huwa wanawekwa ndani...Pia wakati mwingine uwekwa ndani kwa usalama wao. Tuheshimu kazi za wenzetu jamani.
 
Ili nchi iendelee inahitaji kila mtu abobee kwenye eneo lake mfano mkulima alime Sana,injinia afanye Kazi za uinjinia Sana,Askofu afanye Kazi za Uaskofu Sana nk ukiona Askofu anavua kofia la Uaskofu kageukia fani ya Sheria au upelelezi ujue nchi inaanza kuchanganyikiwa na kuendelea itakuwa vigumu
Hii tafsiri haipo duniani!
Ni tafsiri ya viongozi waovu wanaopenda kunyanyasa na kutesa watu bila kuhojiwa!

Maovu lazima yakemewe na kila mtu!! Sasa hivi mtu anabadilishiwa mashtaka na kupewa yasiyodhaminika ili kumkomoa kwakuwa tu kamsema kiongozi aliyemchagua yeye mwenyewe!!

Hapana, ushetani huu lazima tuukatae!
 
Ndio.Ndio maana huwa tunapiga kura kuchagua madiwani na Wabunge ili wao wawakilishe mawazo yetu huko.mbele sisi tuendelee kuchapa kazi kwenye taaluma zetu
Kwahiyo yukiletewa sera na miongozo isiyoturidhisha au haina maslahi maoana ya sekta zetu , yukinyimwa haki na uhuru , au tunalipa kodi hatuoni mrejesho kwenye huduma za jamii tukaamua kupaza sauti zetu NI MBAYA
 
Back
Top Bottom