BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Baadhi ya watu wanashangaa Askofu Mwamakula kuwatetea CHADEMA! Wapo wanaoshauri Askofu awe anafanya mara moja moja lakini sio kila mara. Wakati wa janga la UKIMWI, tulizika ndugu zetu wengi. Lakini hatukuchoka kulia kila ndugu alipokufa eti kwa sababu tulilia misiba ya jana na juzi. CHADEMA wapo katika msiba mzito. Kila siku viongozi na wanachama wao wanakamatwa, wanavunjiwa Ofisi zao, wanapigwa, wanabambikiwa kesi, wanaswekwa ndani, wanaporwa chaguzi, nk. Tunaweza kuchoka kulia nao lakini tusichoke kuwatetea wanapopigwa bila sababu. Kijijini, adui alipofiwa hatukumsusia kuzika.
Jana, Askofu aliongea na Catherine Ruge, Katibu Mkuu wa BAWACHA. Alimshauri kuongoza kwa umakini wakati wenzake wako kizuizini. Leo tumeambiwa kuwa Catherine amekamatwa na Polisi alipokwenda Kisutu kusikiliza Kesi ya Mbowe. Amekamatwa pamoja na viongozi wengine wa BAWACHA akiwemo Makamu Mwenyekiti wao Shariffa na Suzana Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA. Kukamata viongozi wengi namna hii pasipo sababu za msingi kunaweka ombwe la uongozi. Wafuasi wao wakiamua 'kucheza mdundiko' uraiani, hakuna atakayewatuliza.
Katika mazingira haya, sisi Askofu hatuwezi kunyamaza. Hatuwezi kuacha kupaza sauti eti kwa sababu tulifanya vile jana! Ni nani anayeweza kufurahia mapumziko wakati jirani anaomboleza? Tunalitaka Jeshi la Polisi kumuachia Catherine Ruge na wenzake pasipo masharti ye yote. Tutunze utulivu uliopo, tusiweke mianya ya kuuondoa.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula