BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,767
- 288,340
TANZANIA! TANZANIA! TANZANIA! SIKIA SAUTI YA ASKOFU!
Askofu Mkuu Oscar Romero wa Kanisa [Roman] Katoliki nchini El Salvador alipokuwa akitetea haki hakuwa na nia ya kugombea nafasi za kisiasa nchini El Salvador! Askofu Mkuu Desmond Tutu wa Kanisa Anglikana Afrika Kusini Alipotetea haki hakuwa na lengo la kupata uteuzi wa kisiasa nchini Afrika Kusini!
Kadharika, Askofu Mkuu Janani Luwum wa Church of Uganda (Kanisa Anglikana la Uganda) alipotetea haki nchini Uganda hakuwa na nia ya kutafuta nafasi za kisiasa katika nchi ya Uganda! Pia Askofu Henry Okullu wa Kanisa Anglikana Kenya alipopigania haki hakuwa anatamani kugombea nafasi za kisiasa nchini Kenya!
Maaskofu wa Kanisa Katoliki walipoamua kusaidia maridhiano katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo hawakukusudia kuchukua nafasi za kisiasa katika DRC! Maaskofu wa Malawi walipopambana kuondosha mfumo wa kidikiteta na kupigania haki katika nchi ya Malawi wakati wa Rais Hastings Kamuzu Banda hawakuwa wanatamani nafasi za kisiasa!
Katika Tanzania ya leo, Askofu Mwamakula pamoja na Maaskofu wengine wanapotetea haki, Tume Huru ya Uchaguzi, na Katiba Mpya sio kuwa wanatamani nafasi za kisiasa! Kama walivyofanya watangulizi wao katika nchi zao kama ilivyoelezwa hapo juu, Maaskofu wa Tanzania na wao wanatimiza wajibu wao unaombatana na Wito wao Mkuu uliothibitishwa kupitia viapo vya Kiaskofu!
Haiwezekani katika jamii wakakaa kimya wote! Jamii ambayo watu wote wamenyamazishwa na kukubali kukaa kimya inakuwa imeondokewa na dhamiri ya Mungu! Tunaamini kuwa Tanzania bado ina dhamiri ya Mungu ndio maana sauti za Maaskofu hata kama ni chache sana zingali zinasikika!
Usipotoshwe na wala usitishwe na watu wachache wanaonufaika na mfumo usiotenda haki! Ungana na Askofu Mwamakula katika "Matembezi ya Hiyari" ya kuhamasisha umuhimu wa Kuundwa Tume Huru ya Uchaguzi na kuandikwa kwa Katiba Mpya!
Askofu atawajulisha Watanzania wote na ulimwengu kwa ujumla tarehe ya kuanza kwa matembezi hayo!
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula.