Nianze kwa kusema namuheshimu Askofu Kulola kama mtumishi kamili wa MUNGU. Kama utumishi Tanzania, ameufanya na hakuna swali katika hilo.
Lakini lazima niseme kuwa u-CCM wake unatia kinyaa sasa maana amezidi. Wakati wa uchaguzi alikemea kila mtu aliyeonekana kama anashabikia CHADEMA. Akaweka mkutano mkubwa sana pale Biafra Kinondoni akielezea kwanini bila CCM nchi itaingiwa na vita. Hata pale Askofu mwenzie, Kakobe aliposhauri washirika wake waende ibada jumamosi ili jumapili waitoe kwa ajili ya kupiga kura, Kulola alimtusi vibaya sana. Namnukuu maneno yake akisema, "wanaosema washirika waende kupiga kura jumapili wamelaaniwa". Hapo hapo akatangaza kwa wachungaji wa kanisa lake la EAGT (mimi nilidhani linatakiwa kuwa la Mungu) kuwa yeyote atakayefuata wazo la Askofu Kakobe ambaye alimuita "pepo" atashughulikiwa. Mimi najiuliza hivi huyu mzee haoni aibu? Waliposema JK ni chaguo la Mungu tuliwakubalia matokeo yake JK kaua nchi. Leo hii hatudanganyiki tena maana inaelekea wengi wanafikiri kwa kutumia matumbo kama Mrisho Gumbo alivyosema.
Kwa yeyote ambaye hajasoma utumbo huu, tafadhali soma habari hapo chini iliyotokea katika gazeti la Habari Leo.
Askofu: Muombeeni Kikwete, msimwandame
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God (EAGT), Moses Kulola, amewataka Watanzania kumwombea Rais Jakaya Kikwete katika kazi zake na waache kumwandama kwani ana mzigo mkubwa wa kufikiria wananchi.
Aidha, amewataka Watanzania kutokubali kushawishika na mtu yeyote, ili kujiepusha kusababisha uvunjifu wa amani huku akisisitiza kuwa nchini hakuna maisha magumu ikilinganishwa na nchi jirani.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam , Askofu huyo alisema umefika wakati wa Watanzania kuweka pembeni ushabiki wa kisiasa na kuungana kumwombea Kikwete ili nchi ibarikiwe na Mungu, kwani utawala unaruhusiwa na Mungu anayeuweka na kuuondoa.
Amesema, ameamua kutoa rai hiyo kwa Watanzania akiwa ni kiongozi wa dini kutokana na jinsi anavyoona uvunjifu wa amani unavyotokea katika nchi nyingine, hivyo Watanzania waepuke kushawishiwa na kujiingiza katika vurugu zitakazosababisha kuvunjika kwa amani.
Amesema, Kanisa lake lina wanachama wa vyama tofauti, lakini katika kuhakikisha amani iliyopo inalindwa kwa maslahi ya Watanzania wote, inapaswa kuwa kitu kimoja katika kumwomba Mungu.
Amesema, hali hiyo inatokana na kuwa Mkuu huyo wa Nchi halali na usiku kucha roho yake inatapatapa nchi nzima kuangalia sehemu yenye matatizo, ili kuhakikisha wanapata ufumbuzi.
"Roho ya Rais wetu haitulii kwani kukiwa na magonjwa ni lazima atafute njia ya kuwa salama, hivyo tumwombee kwa Mungu ili awe pamoja naye, ili nchi iongozwe na Mungu, kwani tusipowapenda viongozi, wananchi tunamchukiza Mungu," amesema Kulola leo .
Amesema, kinachotakiwa ni kumwombea hadi amalize muda wake wa uongozi na kupata mtawala mwingine wa nchi; uchochezi utakaosababisha vurugu na uvunjifu wa amani usikubaliwe hata kidogo, kwani kuna nchi zilikuwa na amani mtu au kundi la watu likasababisha amani kutoweka.
"Sisi hatuna maisha magumu kama nchi zingine, watu wasilaumu tu wafanye utafiti na kuhakikisha kile wanachosema, mimi nimezunguka nchi nyingi kuna zenye maisha magumu ya kukosa hata chakula," amesema.