Askofu Chimeledya asema leo mwisho kwa Mokiwa, anaviachia vyombo vya dola vifanye kazi

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Akizungumza wakati wa ibada maalum ya kuhitimisha mchakato wa kumtaka Mokiwa ajiuzulu leo, Askofu mkuu wa Anglikana nchini, Dk Jacob Chimeldya amesema leo ndio mwisho wa mchakato huo na watu warudi makanisani mwao kuendelea na huduma za kiroho.

Askofu Chimeledya ameonya kwamba chochote kitachoendelea baada ya ibada hiyo kitakuwa ni uvunjifu wa amani na kwamba ataviachia vyombo vya dola vifanye kazi yake.

Mwananchi
 
Dr Jakob chimeldya askofu mkuu anglikana visasi ni kitu kisichompendeza MUNGU hili ni razma litakurudi amini usiamini kwa hayo uyatendayo juu ya mtu huyu hakika kabla ya juwa kuchwa macho yako yatafifishwa, tubu na ujitenge na hayo.
 
Halafu bado mnataka NILIPE sadaka? (kiingilio?_)

Show yenyewe haina mvuto kama hivyo

Acheni maigizo

DINI YA KWELI NI UPENDO TU

Haya mengine ni NJAA zenu tu!

Mokiwa usitoke, Halafu tuone kinachotokea

Hivi ndio nyie akina mokiwa huwa mnasamehe dhambi makanisani?

Ahahaha

ahahah

ahahah

Mara tatu inatosha!

WAJINGA NDIO ...

FaizaFoxy
Huyo ndo askofu wa TISS au?
 
Dr Jakob chimeldya askofu mkuu anglikana visasi ni kitu kisichompendeza MUNGU hili ni razma litakurudi amini usiamini kwa hayo uyatendayo juu ya mtu huyu hakika kabla ya juwa kuchwa macho yako yatafifishwa, tubu na ujitenge na hayo.
Yeye ameingiaje? Nani kamwingiza kama sio wale ma black suits na miwani myeusi? Na ile gari alilopewa mbona linajulikana?Mwache aendelee tu Mungu wa mbinguni anamuona
 
Wanagombania Madhabahu.........waanzzishe makanisa yao,mbona Gwajima,Lusekelo na EFATHA wana move fresh tu.Kakobe ndio kidooogo ana ugomvi na watu wake
 
Watu bwana kamtendea nini ?hakuna aliekamilika lakini kiutumishi ukikutwa na dosari ili kulinda kazi ya Mungu lazima uchukuliwe hatua
 
Hii aibu kubwa sana kwa waumini wote . Kama viongozi wameshindwa kukaa chini na kumaliza tofauti zao na kanisa lisimame imara. Sisi waimini tukimbilie kwanani?hapo lazima kitakuwa na mpasuko ndani kwa ndani,tuombe Mungu usifumuke juu itakuwa hatari sana
 
Mokiwa ni kichwa na yuko vizuri mtu yule! hana roho na madhabahu za kimaskini zinazombeba na si askofu wa kumpoteza kirahisi waglicana wakipoteza hapo wataharibu!
 
Askofu Mkuu wa kanisa la Anglikana Tanzania,Dk Chimeledya amesema kwamba leo ndo mwisho wa aliyekuwa askofu mkuu wa jimbo la Dsm Dk Valentino Mokiwa kulitumikia kanisa hilo. Kuanzia leo si mdhamini tena na akikaidi agizo hilo, ataviachia vyombo vya dola vishughulike nae.

Askofu Chimeledya asema leo ndiyo mwisho
 
Nadhani ifike wakati Mokiwa akae pembeni amemtumikia Mungu kama kiongozi Anglikana kwa muda mrefu ameshika mpaka madaraka makubwa ya juu kabisa ya uaskofu mkuu Tanzania kwanini asiachie wengine hivyo vyeo? Ni kwanini basi kama anataka kuendelea kumtumikia Mungu asimtumikie kwa namna nyingine kwani kumhubiri Mungu lazima uwe Askofu? Huu ulipumba unampunguzia heshima yake
 
Back
Top Bottom