Askofu Mhogolo amshambulia Dr Slaa na CHADEMA; asema anawahadaa Watanzania na Siasa za Utapeli

Haya tunarudia kusema...ASKOFU HUYU ANA NJAA NA HAJASOMA....umeridhika?

Unajua alieweka sumu ya kuhubiria watu wa kanisa fulani wachague chama fulani ndio ametufikisha hapa hutakaa hata siku moja lile kanisa usikie wanakuja na kauli kama hizi sana sana makanisa kama ya padri Mhogolo na mengineyo ndio utawasikia wakitoa kauli kinzani kama hizi.

Ushauri wangu chama kina muda wa kujipanga sisi tusio jali maswala ya udini tutavutika chama kikijuvua joho la udini ijapo kuwa ni vizuri kutumia viongozi wa kidini ili kuvuta wafuasi ila isiwe kutumia wa dini moja au dhehebu fulani tu hii ni hatari.
 
Ukweli ni kwamba anataka sana umaarufu huyu Dr. Slaa, alitegemea kupata u:eyeroll1:rais kwa urahisi lakini kwa kuwa wa alitaka kuwafanyia ubaya wakuu wa serikali zilizopita. Mungu apishie mbali na janga lake. TUMUOGOPE
KAMA UKOMA
 
Huyu dr slaa jamani tumuache abwabwaje ila tuangalie tu asitupandikize mbegu ya chuki
ya kuchukiana wenyewe kwa wenyewe. Hakuna lisilo na mwisho.
 
In the name of jesus, i do appreciate and like what you have preached to us may god bless you
you and the nation as a whole.
 
wanaJF let'z act as the great thinkers. Nimesoma coments zote nimegundua kuwa wengi tuna argue kishabiki na labda bila kufikiri kwa kina.

Mi nadhani kabla hatujamshambulia Askofu Mhogolo kuwa ana hatia, au kumtetea kuwa hana hatia tujiulize kwanza uhalisia wa hiyo thread.

Je ni kweli Askofu Mhogolo aliyasema hayo? Huyu MLENGO WA KATI ameleta tuhuma. Lakini hakuna evidence yoyote ya kudhitisha tuhuma hizo. Angalau angeleta atachment ya video tuhakikishe hayo yalitoka kwenye kinywa cha Mhogolo tungeweza kuargue kama tulivyofanya.

Lakini kuanza kumshambulia Askofu bila kudhibitisha tuhuma ni ufinyu wa fikra. Kwanini tuamini kuwa aliyosema MLENGO WA KATI hayajaongezwa chumvi.? Na kama huyo Askofu alitoa maneno makali kiasi hicho vyombo vya habari na watanzania wengine walikuwa wapi? Mbona hatusikii kauli zao? Ina maana MLENGO WA KATI alikuwa kwenye hiyo ibada peke yake?

Tunapaswa kufanya Argument na si kukimbilia kutuhumu na kutukana. Let us maintain our Reputation as GREAT THINKERS!

Naiunga mkono hoja yako hasa ukitilia maanani mtazamo wa mtoa thread hii. Inawezekana alipandikiza maneno hayo kwa bishop ili watu waamini kwamba Dr. Slaa anapingwa na kanisa. Kama ndio hivyo basi mtoa thred hii hakufanya uungwana. Tunaomba waliohudhuria ibada hiyo wajitokeze na watuambie ukweli upoje. Lakini wanaJF sioni kwanini watu wajae jaziba na kumuandama askofu huyu kwa maneno makali na matusi, kwani sio lazima watu wote tuwe na msimamo/mtazamo mmoja kwenye jambo hili, kwani hata kimaslahi tunatofautiana. Kuna wanao nufaika na ufisadi kwao hawa vita dhidi ya ufisadi na kiama kwao hivyo hawata ipenda, kunawapenzi na mashabiki wa chama kinachohusishwa na ufisadi,hawa hatakama hawanufaiki na ufisadi wako tayari kukitetea kwa gharama zozote hata ikibibidi kupoteza uhai wao. Nilikuwa kijijini kwangu ambako mafisadi walihujumu dawa za zahanati, maelezo ya hovyo yalitolewa eti dawa hazikuletwa kwa sababu pesa ilitumika kukiimarisha chama dhidi ya upinzani na mtoa maelezo akashangiliwa sana! Muda na uelewa utatusaidia. Matusi na kashifa dhidi ya mtoa hoja inabomoa uelewa. Uvumilivu na ukweli (honest) ni mhimili wa busara.
 
Mbona maaskofu na Mapadre kila siku wanatwambia sisi ni wadhambi: wazinzi, mafisadi, wachafu sana, n.k. Wamepata ushahidi wapi kwamba sis ni wadhambi na kama wana ushahidi kwa nini wasitushaki mahakamani?
 
Siku zote ukweli huwa unauma. Tulia uelimishwe wewe!Unakurupuka km mfuasi wa mdundiko? UNAKOTOKEA HAKUJUI, UNAKOKWENDA HAPAJUI,KWA SHUGHULI GANI HAJUI! sipo hapa kwa ajili ya kukufikishia salam zako kwa uwapendao au uwachukiao. Napenda ujue tu kuwa stahili inayotumiwa na cdm haitofautiani na ile iliyokwisha tumiwa na NCCR Iliyokuwa ya MRM ktk shutuma za CHAVDA n.k na TLP kuhusu Bulyanhulu

So what?
 
huwa siku zote naamini viongozi wa dini huwa wanasimamia katika ukweli na haki kama sehemu ya imani ya dini zao na njia bora ya kumpendeza muumba.sasa ukishaona hata viongozi wa dini wanakwepa ukweli au kuupindisha na kuanza kuushabikia uongo kwa majina na vyeo vyao walivyonavyo katika jamii basi ujue kwa hakika something must be done by the majority of raia wema kabla taifa halijaharibika.
alafu huyu nae usiku anapiga magoti na kuomba kweli kufika mbinguni kazi
 
Huyu dr slaa jamani tumuache abwabwaje ila tuangalie tu asitupandikize mbegu ya chuki
ya kuchukiana wenyewe kwa wenyewe. Hakuna lisilo na mwisho.
Naona mzee wa Mtera (JSM) uko kazini baada ya kutajwa na Dr. wa ukweli kwamba nawe una mafungamano fulani na mafisadi. Sasa umeanza kuwatumia maaskofu rafiki zako kina Mhogoro kumchafua Dr. Pole sana. Kajivue gamba mkuu.
 
Kwa tunaomjua Askofu Mhogolo hatujasumbua akili zetu kujua ni kwa nini alisema hayo aliyoyasema! Ni Mmoja kati ya maaskofu wenye uelewa finyu na wasio na msimamo wa kweli wa Kuhubiri injili ya Bwana na kutetea roho za wanyonge! Amesababisha migogoro mingi sana katika dayosisi yake na mingi ina mrengo wa ufisadi na tamaa ya mali. Kwa kifupi sio muadilifu kabisa. ndio maana hata alidiriki kutetea ushoga ili tu aweze kunufaika na misaada ya mashoga. Ni mrafi! Kauli alizozitoa ni za kujikomba CCM! Nakushauri askofu wangu Mhogolo nenda kapige magoti mbele za Bwana na utubu! Bei yako ni rahisi mno!
 
Hivi kuna ulazima gani wa viongozi wa dini kuongelea siasa wakiwa na waumini wao hata kama hana jipya na la maana la kuongea?

silikiza viongozi kuongelea siasa si mbaya kwani mbali ya kuwakuza kiroho waumini, kazi yao nyingine ni kuwaandaa waumini wao kijamii wawe watu bora wenye maadili na kuwa na jamii iliyo na miongozo mizuri, ndio maana mbali na imani ya muumba na kuwaandaa kwenda mbinguni wanajihusisha na vitu kama kutatua migogoro ya ndoa wanahusika na misiba kuzaliwa kwa watu na elimu za kujitambua na vingine siasa ni sehemu ya maisha ya muumini au waumini hivyo yanawahusu dirct.
ila sasa kutokana na kutekwa au sijui uoga ama kuamua tu kupindisha ukweli viongozi wengi wa dini hawapendi ama wanalazimishwa kuwa na upande, wakati hawatakiwi kuwa na upande wanatakiwa kukemea mabaya ya siasa na kupromote mazuri. hali ilivyo sasa ni kuwa viongozi wetu wa dini wanakemea mazuri na kupromote mabaya. si vibaya kiongozi wa dini akihamasiha waumini kupiga kura kibaya kitakuwa akianza kumpigia debe fulani tena mchafu hapo sisi waumini tutaanza kuhoji aina ya mungu anayemtumikia.hivyo ni kawaida na ni wajibu wa viongozi wa dini kujihusisha na siasa.
 
Guys,
Kama tumefikia mahala ambapo jamii wa Watanzania wanahubiriwa na watu wa MUNGU kama akina Askofu Mhogolo kuwakumbatia Mafisadi basi hatujui tunakokwenda kama Taifa !....................... Naanza kuogopa !
 
Askofu Muhogolo mwenyewe ni clean namna gani? Anataka watu wamchimbe ya kwenye diocese yake? Udini, ukabila! Hadi afukuzwe kwa mawe hapo Dodoma? Ningekuwa yeye, ningekaa kimya!!
 
Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo wa Dayosis of Central Tanganyika Mkoani Dodoma,amemjia juu Katibu Mkuu wa Chadema na chama chake kuwa wana wachezea Watanzania kwa kujijengea umaarufu rahisi(cheap popularity).

Askof Mhogolo katika mahubiri ya Ijumaa Kuu alisema kitendo cha Dr Slaa kutaja watuhumiwa wa Ufisadi mwaka 2007 huku akiwa na Ushahidi juu ya wanaotuhumiwa na Ufisadi huku akitembea na ushahidi kwenye briefcase ni Kujitafutia umaarufu na kuwapotezea muda Watanzania.

Kama umemkamata mwizi na una ushahidi kwa nini usiende mahakamani na Watuhumiwa washitakiwe!? Kitendo cha Dr Slaa kuongeza tena orodha ya Watuhumiwa huku aliowataja haja peleka ushahidi wake mahakamani kwa orodha ya mwaka 2007 ni kazi ya pwagu na pwaguzi.

Ana wahadaa Watanzania kutokana na uelewa wao mdogo hasa vijana wanao mshabikia! Alimalizia kwa kusema Chadema imekaa na mtizamo wa kutaka watu waiunge mkono kwa fujo na maandamano lakini Viongozi wake wako kwa kujitafutia Umaarufu wa kisiasa.

Akaonya Wanapofanya maandamano yao na uvunjifu wa amani kama ya jijini Arusha wakumbuke kuna amani ya Watanzania ambao si wafuasi wa vyama.

Mhogolo uwaombe radhi watanzania kwa kututukana kama wewe unauelewa kwanini? Usimpeleke d wa ukweli mahakamani kwa kudanganya uma kama hutumiwi na hao mafisadi tunafaham ataakiwapeleka mahakamani haki haitatendeka izo mahakama zinamilikiwa nahao mafisadi jk alisha husiswa naufisadi majaji anateuwa yeye atakama haunaakili haki itatoka wapi? Mhogola kusema hatuna uelewa umekosea inaonekana hata icho cheo nijinsi gani ulikipata kimakosa watukae wanao kuletea sadaka sikuwajumuisha nawengine
 
jamani msisahau kuna watu waliropoka kuwa kuna maaskofu wanatawasafisha mafisadi nadhani hiii ni njia mojawapo. Maana haiwezekani watu wanapoteza muda wao kutetea watu then anakuja mtu anaongea vitu vya ajabu! Ndiyo maana hata maadili yamepotea kwakuwa hao viongozi wa dini wengi siku hizi ni viongozi maslahi.

sikuona haja ya yeye kusema watu wanatafuta cheap populality sijui na yeye tumuweke kundi gani maana nadhani na yeye ni walewale.
 
Hubiri kazi ya Mungu kama kweli weye ni mchungaji. Watanzania bado tuna mwendo mrefu sana wa kwenda. CDM wanaonesha njia, na wana nia ya dhati kabisa. Tunachotaka ni mfumo kubadilika, na matunda yake tumeona maandalizi ya katiba mpya. Hivi wewe askofu kesi hizi zitaenda wapi wakati mahakama wanashindwa kutoa hukumu? Suala la Mtikila na mgombea binafsi liliishia wapi? mahakama inashindwa kutoa maamuzi agaist serikali. Mtu asiposhitakiwa na hii serikali kwa makosa aliyotenda, manake ana-support fulani nyuma yake.

BWANA AWE NANYI!
 
Back
Top Bottom