Askofu Mhogolo amshambulia Dr Slaa na CHADEMA; asema anawahadaa Watanzania na Siasa za Utapeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Mhogolo amshambulia Dr Slaa na CHADEMA; asema anawahadaa Watanzania na Siasa za Utapeli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlengo wa Kati, Apr 25, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  Apr 25, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Askofu Godfrey Mdimi Mhogolo wa Dayosis of Central Tanganyika Mkoani Dodoma,amemjia juu Katibu Mkuu wa Chadema na chama chake kuwa wana wachezea Watanzania kwa kujijengea umaarufu rahisi(cheap popularity).

  Askof Mhogolo katika mahubiri ya Ijumaa Kuu alisema kitendo cha Dr Slaa kutaja watuhumiwa wa Ufisadi mwaka 2007 huku akiwa na Ushahidi juu ya wanaotuhumiwa na Ufisadi huku akitembea na ushahidi kwenye briefcase ni Kujitafutia umaarufu na kuwapotezea muda Watanzania.

  Kama umemkamata mwizi na una ushahidi kwa nini usiende mahakamani na Watuhumiwa washitakiwe!? Kitendo cha Dr Slaa kuongeza tena orodha ya Watuhumiwa huku aliowataja haja peleka ushahidi wake mahakamani kwa orodha ya mwaka 2007 ni kazi ya pwagu na pwaguzi.

  Ana wahadaa Watanzania kutokana na uelewa wao mdogo hasa vijana wanao mshabikia! Alimalizia kwa kusema Chadema imekaa na mtizamo wa kutaka watu waiunge mkono kwa fujo na maandamano lakini Viongozi wake wako kwa kujitafutia Umaarufu wa kisiasa.

  Akaonya Wanapofanya maandamano yao na uvunjifu wa amani kama ya jijini Arusha wakumbuke kuna amani ya Watanzania ambao si wafuasi wa vyama.
   
 2. O

  Olecranon JF-Expert Member

  #2
  Apr 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,371
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  Naona huyu Askofu kachemsha hasa. Dr. Slaa haongozi serikali huo uwezo wa kupeleka mafisadi mahakamani atautoa wapi? Ee Bwana naomba umsamehe kwani hajui alisemalo!
   
 3. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #3
  Apr 25, 2011
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Anaishi Tanzania gani?Labda hajaskia kuwa miongoni mwa waliokuwa kwenye list of shame ya 2007 leo hii wako mahakamani kwa tuhuma za ufisadi na wengine wameporwa ulaji ndani ya CCM na kupachikwa jina la magamba.

  Ama kweli si wote wasemao BwanA Bwana watauona ufalme wa mbingu.The so-called askofu ameona kelele za Dkt Slaa/Chadema dhidi ya ufisadi ni hatari zaidi kuliko ushetani unaofanywa na mafisadi kwa WALALAHOI!!!

  HAlafu anasema Slaa apeleke majina ya mafisadi mahakamani!!!Anamaanisha mahakama hizi hizi zilizomhukumu Chenge faini ya laki 7 kwa kosa la kuu ,au mahakama ya kina Ocampo?Tatizo la baadhi ya hawa watmishi feki wa Bwana ni they are so out of touch with the reality wanajikuta wanaropoka tu ionce wakiwa kwenye mahubiri yao.
   
 4. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #4
  Apr 25, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio wasomi wote wanajua na kuelewa, wengi ya wasomi ni wakaririaji, wafuata upepo, hawana jipya, wababaishaji. Hata maaskofu si wote wana uelewa, na wengine ni wachumia tumbo na mamluki.

  Vijana hawafuati kanga wala vitenge wala shuka wala rushwa ya kwenda mkutanoni, wanafuata sera kutegemea na mahitaji yao, kama wanasiasa akiwemo d r slaa wanafuata cheap popularity baasi waache wasiofuata cheap watafuatwa na vijana.

  How comes Askofu unakuwa mpiga debe wa ufisadi, kisema ukweli kwa akina dr slaa na chadema ni cheap popula rity? Anataka wasiasa wafanye nini? Nimesokitishwa sana na uelewa mdogo wa askofu huyu.

  Je hana chochote kinacomfanya asahau kuwa waathirika wa ufisadi ni pamoja na waumini wake?

  Je kazi ya dr slaa ni upolisi au PCCB hadi apeleke watu mahakamani kwa hela ya umma?

  Du tuna kazi wajumbe ila Mungu wa kweli atasimama katika kweli maana sio kila askofu ataoina kweli wala mbingu bali wenye unyenyekevu na wa kweli
   
 5. c

  chitage Member

  #5
  Apr 25, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 41
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  "Maaskofu wengine bwana " mawazo yao dhaaaifu kuliko hata sie walei,kutetea uovu kwa kichaka cha kutetea amani bila kutambua kuwa haki ni msingi wa amani kwangu naona ni unafiki mtupu.hivi mahakama gani anazozizungumzia,hizi zisizokuwa huru.slaa kafanya kazi ya siasa,katuelimisha na kutufumbua macho watanzania,basi na yeye ''askofu'' kama kaona slaa kafanya makosa basi ampeleke mahakamani badala ya kuzungumzia kwenye mimbari,"baba askofu "toa boriti jichoni mwako ndio uone kibanzi cha mwenzio.na bado mafisadi na watetezi wenu mtajitokeza popote mlipo,mitaani,makanisani na misikitini ili kazi yetu iwe rahisi-kuwashughulikia.
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,205
  Trophy Points: 280
  Tuletee source ili tuweze kuchangia vizuri.
   
 7. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mhogol huyu wa Dodoma au? Hivi ule ugomvi wake hapo kanisani ulishaisha (kwa wenye details)?


  hawa washakuwa corrupt wote......kuchakachuka hakuangalii eti wewe ni mkuu wa dini au kibaka?


  I bet atuja kuchukua njia ya mwenzake Mwamasika wa KKKT Dom ambae alikwa akijiminya minya sana akiwa askofu na siku alipo-step down akaibukia kwenye mchujo wa kura za maoni CCM agombee ubunge Dodoma...............wao ndio wanatafuta cheap popularity ili siku wakistgaafu wapate wa kuwaalika kugombea ubunge CHICHIEMU

  Angalau ityajulikana kuna kiumbe kinaitwa Mhogo....lol!
   
 8. b

  bulunga JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ni askofu wa kanisa gani, kuna reputable Bishops ambao wakisema kitu unakuna kichwa , lakini huyu nafikiri yeye ndo anataka cheap popularity
   
 9. KIMBURU

  KIMBURU JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 210
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Huyu ni moja kati ya maaskofu vilaza wa anglikana, ni juzi tu nimemsikia akisifia kikombe cha babu wa Loliondo na kusahau kuwa yeye kama askofu anapaswa kuwahubiria watu wake kuwa njia ya uponyaji ni YESU pekee. Halafu ni huyu huyu askofu aliyewahi kutofautiana na maaskofu wenzake kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono ushoga. Halafu bado kama yote hayo hayatoshi anaendelea kuunga mkono umafia unaofanywa na CCM. But anyway tunaendelea kumwomba Mungu amfungue.

  WANA JF TUSIMSHANGAE HUYU KIONGOZI WA DINI KWA KULETA VIPINGAMIZI DHIDI YA UKOMBOZI WA WATANZANIA KWANI HATA HARAKATI ZA YESU ZA KULETA UKOMBOZI KWA WANADAMU ZIPATA VIPINGAMIZI KUTOKA KWA VIONGOZI WA DINI WA AINA YA MHOGOLO.
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  MWASHAM BABA ASKOFU MHOGOLO:
  HUU UFISADI WA KIMFUMO NDANI YA SERIKALI YA CCM NCHINI NDIO ULITEGEMEA DR SLAA NA CHADEMA
  KWELI KUUMALIZA BILA YA USHIRIKI WETU WA MOJA KWA MOJA 'SISI NGUVU YA UMMA' KAMA TUNAVYOFANYA HIVI SASA???

  Watanzania pindi unapomuona mtu mzima na mwenye kustahili heshima nyingi sana tu katika jamii anapoanza kutoa kauli tata na zenye kupindapinda mbele ya vita vikali kama hivi dhidi ya UFISADI nchini, wala usisubiri kuambiwa kwamba ni 'Askofu Mtafutaji' bali zaidi nenda tu ukaombe kuona mtiririko wa kifedha ndani ya akaunti yake japo kwa kipindi cha miezi sita tu iliyopita na baada ya hapo utapata jibu.

  Ugunduaji wa UFISADI au wizi wa mali ya umma wala na mtu fulani kuamua kuipigia kelele kwa Watanzania tunaibiwa tuamke wala hakumfanyi huyo mpiga kelele dhidi ya wizi huo kugeuka kuwa MTUHUMIWA NA AU MTAPELI KWA HAYO MADAI YA UFISADI eti kwa sababu tu hakufungua mashitaka ama kwa BALOZI WA NYUMA KUMI na au katika kile kilichotajwa kama 'Mahakama' nchini.

  Isitoshe, jukumu la kulinda mali ya umma ni ya Umma wenyewe wa Tanzania kwa ujumla wetu na wala si jukumu la mpiga kelele dhidi ya wizi husika wala chama fulani tu cha siasa nchini. Katika hili hata Mhasham Baba Askofu yeyote nchini, ambao kazi yao ya kwanza ni kuongoza unyoofu wa mioyo na kulinda Uadilifu katika jamii yetu nzima, angeweza tu kwenda naye mahakamani kufungua mashitaka kwa niaba yetu sote Watanzania tunaoibiwa.

  Ni katika misingi hiyo miwili hapo juu ndio maana kidogo napata taaaaabu kweli kweli kusoma kitu kingine chochote kile zaidi ya UNAFIKI wa ajabu katika madai mazito ya Askofu wetu huyu wa Dodoma kuamini kwamba Bora Mfumo wa KIFISADI nchini kuliko kelele za Dr Slaa mnamo 2007 na tena hivi majuzi ambazo huonekana kuelekea kuharibu ULAJI NAFUU WA WENGI WASANYAJI WA KODI ZA UMMA.

  Lakini, mbali na yote, Mwasham Baba Askofu Mhogolo, hivyo ndio kusema kwamba kwa kiwango ambacho hata wewe unakubali UFISADI kutanda kila mahali nchini ndio tuseme ya kwamba unataka kutuaminisha ya kwamba HUKO MAHAKAMANI unakoelekeza mkono ndiko ambako huenda MAFISADI walipasamehe kuingilia kwa kupenyeza zao DONAR TATU au ndio tunaambiwa kitu gani hadi hapo?????

  Au ndio kusema ya kwamba pengine ni kwake Askofu kukisia ya kwamba HUU UFISADI WA KIMFUMO MZIMA ambao hata Rais Kikwete Mwenyewe amekua akikwepa kuushughulikia (pamoja na nguvu zote za dola tulizompa unaona Dr Slaa tu ndiye angeweza kuumaliza kwa peke yake tu ndani ya Tanzania bila hata kutuhitaji sisi Nguvu ya Umma kumaliza kabisa mchezo mzima kama ambavyo tunavyofanya hivi sasa???

  Jamani kule kukitetea Chama Cha Mapinduzi kwa Baba Askofu si kosa, bali ni kwamba kosa lake linaanzia pale ambapo anaanzo kuona ya kwamba UFISADI WA KIMFUMO unaofadhiliwa na serikali ya CCM ni jukumu la Dr Slaa peke yake au CHADEMA bila kutuita sisi Watanzania WENYE MALI ZINAZOKWAPULIWA kushiriki moja kwa moja katika vita hizi.

  Hadi hapa Baba Askofu Mhogolo, napenda nijifanye ya kwamba kwanza kabiza haukuwahi kutoa shutuma kama hizi na kwamba wala haukuamini katika haya yanayodaiwa kutoka mdomoni mwako zaidi ya kuwa mzaha tu huko mitaani.

  'Nguvu ya Umma' vita mbeeeele zaidi dhidi ya MAFISADI wa kila aina na kila kona ya nchi yetu bila kuridi nyuma.
   
 11. mangi waukweli

  mangi waukweli JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kwaiyo ukiingiliwa na mwizi nyumbani kwako na unaushahidi huendi mahakamani kwasababu wewe sio serikali.kabla ujaongea humu shauriana na mkeo
   
 12. R

  Rapture Man JF-Expert Member

  #12
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 411
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Huyu Askofu ni kiongozi kipofu. Nashauri akajifunze toka kwa Maaskofu wenye macho yanayoona. Huyu huenda kala rushwa toka kwa mafisadi.
   
 13. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #13
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Problem ya wahubiri feki ni kutokuona ukweli.Hawa wahubiri wengi kwa sasa ni wafanyabiashara wanaoiabudu ccm.huyu askofu yumo kwenye kundi la kuwanyonya watanzania kwa njia ya kukusanya sadaka na fungu la kumi.Ni kipofu.Mateso ya watanzania bila cdm hakuna kitu.Ukombozi wa mali yetu umeanzishwa na cdm kama hana habari.kazi kubwa ya wahubiri hawa ni kuabudu watawala kwa kuogopa kuumbuliwa kwa maovu yao.hana kisomo cha kutosha kumzidi Slaa kwani hata Dr alikuwa huko na alikuwa mhubiri mzuri lakini akaona ukombozi hautapatikana kupitia kanisa.akatoka.si mnafiki.
   
 14. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #14
  Apr 26, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  wewe nawe shauriana na mkeo.kama umeingiliwa na mwizi na umemwona unaendaje mahakamani.Tunapiga makelele ili majirani waje.Ndio kinachafanyika.huna mantiki wewe na kauli yako.
   
 15. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #15
  Apr 26, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Bishop Mghogolo Visits St. Andrew's
  [​IMG]

  Anapendelea sana kukweya pipa kila mara kwenda kuhubiri AMANI, UADILIFU na HAKI kwa wote huko ma-Ulaya Ulaya, Georgia Atlanta huko na nini vile huku akituacha sisi Walalahoi tukiwa tunakaribia kukata tamaa na maisha kutokana na UFISADI uliokithiri kila mahali.

  Kwa kweli hata huko Mahakamani anakotuelekeza kunategemea zaidi mtu umewatembelea na Kilo Ngapi za DONARI TATU ili ndio mtu upate kupimiwa kiasi fulani cha haki kulingana na urefu wa kamba yako.

  Baba Askofu hebu zunguka na huku Ma-Uswahilini na vijijini ukatuhubirie juu ya kitu gani anachosema Mungu juu ya wizi wa mali ya umma na kutuacha watu tukiathirika kimaisha, bila dawa mahospitalini, gharama za maisha kupaa angani lakini bado mifumo dhalimu kubahatika watetezi tena kutoka kwenye madhabahu zetu tunazoziheshimu saaaaaana.

  Baba Askofu; hebu ondoa kauli hizi haraka sana na utuombe radhi kwa ujumla wetu nchini Tanzania. Ama kweli aliyeshiba wala hapungukiwi usingizi na kelele za mwenye njaa na kuzulumiwa kila kitu - ndio kama hivi unawasikia wenye shibe wakipaza sauti wakilalamikia kero sisi Nguvu ya Umma kudiriki kupiga mayo.

  Baba Askofu Mhogolo, nitakukumbuka leo katika sala ili sote tupate msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa kushindwa kwetu kupeleka MAFISADI mahakamani huku tukitegea ama Dr Slaa au CHADEMA kufanya hiyo kazi.
   
 16. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #16
  Apr 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  huyu bila shaka mafisadi wameshajua bei yake au alishikiwa bunduki kulazimishwa kuongea haya maneno?
  naona kama anataka kutupoteza vijana , nadhani tusipokuwa makini na hawa viongozi wa dini watatuuza kama
  wale wa burundi na Rwanda, watu walikwenda kujificha kanisani wakidhani wako salama kumbe hawakujua hata padri
  alikua na ukabila, akaenda kuwachomea wakachinjiwa kanisani
  ningekuwa mimi ni yeye ningejishungulisha na mambi zaidi kwa ajili ya nchi, vijana na viongozi wake kwa ujumla
   
 17. Wa Mjengoni

  Wa Mjengoni JF-Expert Member

  #17
  Apr 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Fisadi na yeye...ana nyumba zimetapakaa Dodoma yote, kwa hela gani naye ni mtumishi ... ndo maana anatetea wenzake.....
   
 18. M

  MantaLine Member

  #18
  Apr 26, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuliingiliwa na majambazi, wakavunja mlango kwa 'fatuma' wakaiba gari and vitu vingi ndani wakakimbia. Wakati majambazi wakiwa kwenye deal ya kuuza hilo gari, wakakamatwa red handed. Gari, majambazi na manunuzi wakapelekwa polisi na kufunguliwa kesi. Baada ya kesi kutajwa miezi kadhaa, huku zikipigwa tarehe kisingizio uchunguzi unaendelea, mtuhumiwa wa kununua gari akaachiwa huru. Wakati gari liko polisi ikishikiliwa kwa ushahidi, vifaa mbalimbali vikaibiwa. Baada ya miaka 2 kesi ikinguruma, baba wa jambazi akaomba out of court settlement on condition they will pay for all items stolen and we agreed. So far they are yet to pay full amount agreed. Thinking back, it was a waste of time and resources dealing with police and the court on this case, leo hii mke wangu anashauri tungewapiga risasi wale majambazi. This is true story
   
 19. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #19
  Apr 26, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  jamani ahurumiwe huyo hajui atendalo amina
   
 20. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #20
  Apr 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  kuna viongozi wa dini wakiongea huwa nawasikiliza kwa makini. Mhogolo ni pumba tu. Yaani muangalizi wa kondoo wa bwana anaongea hivi hata haya hana. Ndo manabii wa uongo hao.
  Kuna
   
Loading...