Askofu Malasusa kukimbia nchi kama Jerry Mngwamba?

Malasusa yuko kwenye kama time ya amani inayounganishwa na baadhi ya viongozi ambao wengi wao w anaonekana kama mahakama wa serikali hivyo kusoma waraka kawa one a haya matumizi wenzie wa serikali hivyo mwacheni atengwe aende zake
 
Hawezi Mimi namshauri afungue Kanisa lake aliite K.K.K.K.T( Kanisa la Kiinjili na Kilutheri la Kweli Tanzania)
Then amuajiri mama yako nafasi ya uhasibu ili kanisa liwe kubwa na wewe upate ela
Wazo lako zuri amekusikia
 
Naona hatari ya mgawanyiko, huenda ikaibuka KKKT ya Kaskazini na KKKT ya Nyanda za juu kusini. Kufanya kazi na hawa watu inabidi uwe smart sana.
Kanisa la Kristo halitagawanyika kamwe. Wanaoliombea ligawanyike wataumbuka. Hatutampa nafasi shetani na wafuasi wake.
 
Acha kubishana na biblia wewe, kama kusingelikuwa na migawanyiko kanisani Kristo asingeliombea umoja. Aliombea kanisa liwe moja maana alijua migawanyiko itakuwepo tu.
 
Waumini tumetulia tuliiiii wanasiasa sasa porojo nyiiiiingi nasubiri jumapili ifike niende kanisani kikaibadike
 
Hawezi Mimi namshauri afungue Kanisa lake aliite K.K.K.K.T( Kanisa la Kiinjili na Kilutheri la Kweli Tanzania)

Na siku akianzisha hilo nadhani atapewa Go ahead kabla hajajaza form. Kwa kugawa watu, hamjambo. Kuanzisha kanisa lake sio dawa. Dawa ajue, ni wapi aliangukia akatubu. Kiburi hutangulia maanguko. Analijua saana hilo.
 
Malyasusa hawezi kuwa mnafiki na mtu asie mwadilifu kiasi cha kuandaa waraka na kuusaini mwenyewe kisha kujifanya haujui.
Na pili atambue kanisa la kkkt sii kama makanisa yale kila mtu ana lwake. Ni busara akaanzisha lake la kujitegemea kuliko kujificha kwenye kanisa la waumini wote kwa nia binafsi.
jamani hivi mnaijua KKKT au ni kumshambulia tu <alasusa?
waandishi wengi km Mwanahabari Huru ni ushabiki tu
Askofu yeyote wa Dayosisi atachaguliwa na waumini wake tu na sio nje ya Dayosisi
haya yalitokea Iringa kwa Mdegela, Dodoma kwa Mwamasika, Arusha nk
Waumini wa DMP wanamuamini Malasusa na hawatamtoa kwani hapigiwi kura na waumini wote wa DSM na Pwani yake
hebu tutlie kwani septemba si mbali huyu jamaa atabaki na ikiwezekana anaweza kugombea tena uaskofu Mkuu km ruksa ikitokea, kwani aliupata Uaskofu huu akitokea iringa ambapo Uchaguzi wa wakati huo ulileta mgogoro mpaka wakamuomba askofu kijana wakati huo (Malasusa) aokoe jahazi
hawa kina Shoo wanaleta siasa ambazo zitaliharibu Kanisa
 
Acha kubishana na biblia wewe, kama kusingelikuwa na migawanyiko kanisani Kristo asingeliombea umoja. Aliombea kanisa liwe moja maana alijua migawanyiko itakuwepo tu.
Biblia ilikuwepo since time immemorial (Rejea torati). Kanisa la Kristo sio dayosisi ya DMP au usharika kama vile Kariakoo ama Azania Front. Naomba ulitazame 'kiroho zaidi'. Who is Malasusa by the way!! Usitazame kanisa kisiasa au kitawala. Narudia tena: Malasusa na mawakala wake wote hawana uwezo wa kuligawa kanisa la Kristo. Hata yeye analijua hilo vinginevyo anipinge Kwa kauli yake.
 
KUTENGWA kwa Askofu Dk. Alex Malasusa wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP) ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kumeleta fukuto na mjadala mkali ndani ya dayosisi hiyo juu ya hatima ya askofu huyo.

Baadhi ya wachungaji wa DMP wanasema kuna uwezekano mkubwa Askofu Malasusa akakimbia nchi kama ilivyotokea kwa Askofu Jerry Mngwamba wa kanisa hilo miaka kadhaa iliyopita.

Machi 27, 2002 kanisa hilo lilimvua Mngwamba uaskofu baada ya kuwa ametuhumiwa wizi wa Sh. 64 milioni za mfanyabiashara ya magari jijini Dar es Salaam. Naye alikuwa askofu wa DMP. Baada ya kuvuliwa uaskofu, alikimbilia Marekani ambako ilijulikana baadaye kuwa alikuwa anafanya kazi ya udereva wa teksi katika jiji la Chicago.

Kwa sakata la sasa kuhusu Askofu Malasusa, wachungaji wanadai kuwa mwenyewe amejiweka pabaya kwa kutengwa na kanisa baada ya Baraza Kuu la maaskofu wa KKKT kumtenga kwa usaliti, na kumfanya aonekane kikwazo cha imani kwa waamini wake.

Mbali na usaliti, huko nyuma amekuwa anaandamwa na tuhuma za uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa wachungaji wa kike wa kanisa lake. Amekuwa anazikanusha.

Taarifa zinasema baadhi ya wachungaji wake wamefurahishwa na adhabu aliyopewa “bosi” wao, kwani tangu Machi 24 2018 hawakufurahishwa na malekezo aliyowapa kutosoma waraka wa maaskofu katika sharika zao.

Kwao, kitendo cha Askofu Malasusa kukiuka makubaliano ya wenzake 25, ni utovu wa nidhamu na kinyume cha kanuni za kichungaji.

Wanasema kwa kuwa imebainika kuwa maelekezo yake ni matokeo ya “urafiki unaotia shaka” kati yake na serikali, wao wanautazama kama uchochezi mkubwa wa fikra na kiimani dhidi ya waamini wao.

Bila kufafanua zaidi, wanasema kutengwa kwa Askofu Malasusa kuna athari mbaya kwa dayosisi kwani hadi sasa inakabiliwa na madeni makubwa.

“Shule zinazosimamiwa na dayosisi – sekondari na chuo kikuu – zipo hoi. Mashirika ya umma, hasa NSSF na NHIF, yanadai dayosisi yetu pesa nyingi. Mradi pekee ulio salama ni benki,” anasema mchungaji mmoja, kwa sharti la kutotajwa jina.

Wasiwasi wa wachungaji ni kwamba kutengwa huku kwa Askofu Malasusa kutasababisha hata marafiki wa dayosisi kurudi nyuma.

Jitihada za kupata Askofu Malasusa ili azungumzie masuala haya hazikufanikiwa.
We we jamaa huwa ni pimbi sana maana unaandikaga uongo na uzushi mno
 
hongera ila naomba nikukumbushe

MOSI,kuna dayosisi ambazo tena mke wa askofu ana uraia pacha pia inawezekana hata mumewe akawa nao maana wamekulia huko ila baadhi ya taasisi zao hali tete walimu wa vyuo wanafikisha miezi kadhaa bila kulipwa wakisubili wanafunzi wafungue walipe ada.JE HAWA WAMETENGWA NA KKKT?
PILI,tuondoe mentaliti ya kutegemea marafiki,kwani uliamua kuwa mruteli na kuanzisha miradi ya maendeleo kwa kutegemeA MARAFIKI?
TATU,Urafiki wa mashaka wakati neno la mungu linatuagiza tutii mamlaka,je huko kanisani kuna demokrasia?wachungaji wanapigwa uhamisho kisa wakimkemea wakubwa KWENYE DILI zao,au unahisi jamii au waluteri hawajui,MADENI HAYO YA MALASUSA YAMEANZA PASAKA?
NNE,kuna askofu mmoja huko kaskazini ametumia ruzuku ya serikali vibaya au hilo ulijui?au wao wasafi?kuhusu mikopo waulize kaskazin wao walisitiriwaje maana madeni yaliandikwa hadi kwenye magazeti

hitimisho langu
KKKT TUNAIJUA KUANZIA A MPAKA Z ,USAFI WA MAASKOFU NA UFUJAJI WA MALI ZA KANISA,MAMBO MENGINE NI KAMA MAWIMBI YA BAHARI,CAG ANGEKUWA ANAPITA HUKO HATA HAO UNAO WAAMINI USINGE WAAMINI.MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE APEWE
 
jamani hivi mnaijua KKKT au ni kumshambulia tu <alasusa?
waandishi wengi km Mwanahabari Huru ni ushabiki tu
Askofu yeyote wa Dayosisi atachaguliwa na waumini wake tu na sio nje ya Dayosisi
haya yalitokea Iringa kwa Mdegela, Dodoma kwa Mwamasika, Arusha nk
Waumini wa DMP wanamuamini Malasusa na hawatamtoa kwani hapigiwi kura na waumini wote wa DSM na Pwani yake
hebu tutlie kwani septemba si mbali huyu jamaa atabaki na ikiwezekana anaweza kugombea tena uaskofu Mkuu km ruksa ikitokea, kwani aliupata Uaskofu huu akitokea iringa ambapo Uchaguzi wa wakati huo ulileta mgogoro mpaka wakamuomba askofu kijana wakati huo (Malasusa) aokoe jahazi
hawa kina Shoo wanaleta siasa ambazo zitaliharibu Kanisa
Usemayo ni kweli ila kwa Dayosisi ya Mashariki na Pwani maji marefu usilinganishe na Dayosisi za huko Vijijini
 
Back
Top Bottom