Askofu Kakobe pitia hapa

Tena walimwambia ili aruhusiwe kuingia ndani basi wamfumue nywele zake. Muda huo atakuwa anasikiliza Neno au atakuwa anahudumiwa kisaloon?

Je, tunasimamia matendo ya Sheria au Imani? Mtu anaaminije ikiwa hutaki asikilize na kufundishwa kwanza?
Pole Mkuu
 
Leo ni siku ya jumapili siku ya Bwana kwa sisi wenye imani ya Kikristo hasa born again.

Leo sijamuabudu Mungu kwa kuwa nimenyimwa fursa hiyo.
Mkuu Msanii, kwanza pole kwa maswahibu uliokutana nayo.
Kwa vile ibada ina sehemu mbili
  1. Ibada ya ulimwengu wa mwili- kwenda Kanisani kusikiliza mahubiri, kusali na kutoa sadaka na kujichanganya na watu.
  2. Ulimwengu wa Roho- Nia, kusali na kuzungumza na Mungu na kuji isolate.
Mungu ni Omnipotence, Omnipresent na Omniscience, yupo popote hadi ndani yako, ulichokosa ni ibada tu ya ulimwengu wa mwili, lakini ibada ya ulimwengu wa roho, kitendo tuu cha kuwa na nia, ukatoka, ukaenda, ukazuiliwa kwa mambo ya mwilini, wewe umeshiriki na usikute wewe ndio umesali sala ya ukweli kuliko hao wa ibada ya ulimwengu wa mwili.

Askofu Kakobe sio mtu wa mchezo mchezo!.
Askofu Kakobe Asipuuzwe: Ni kama David Koresh na Camp Davidians!

P
 
Ninashukuru kwa post yako na kumbukizi ya threads ulizozitoa.

Ninamfahamu mzee Kakobe kwa kiwango fulani ambapo nikisimama popote nitamuelezea. Lakini kuhusu huduma yake nasema sijawahi kuona binadamu anayefundisha Neno la Mungu kwa viwango vyake.

Pamoja na kwamba waumini wake wanakuwa na hofu na kutetemeka mbele yake lakini mimi sijawahi kufanya hivyo na sijui natoa wapi ujasiri huo. Sijawahi kuwa na hofu wala kufikia hali ya kutahayari bali huwa napenda kusikiliza mahubiri yake kwani yananijenga sana.

Kuna muanzilishi mmoja muhimu sana kwake ambaye ndiye aliyejitoa kwa hali zote kufanikisha usajili wa kanisa lile na hata kupata kile kiwanja na kushiriki ujenzi wa kanisa lile pale Mwenge lililikamilika kwa siku 21, alijitenga na Kakobe baada ya kuona Askofu anaenda nje ya misingi ya Neno la Mungu, yaani kuchanganya dini na siasa jambo ambalo limepelekea kanisa kupitia changamoto nyingi.

Kuhusu mkewe (Mama Sifa) ni kwamba, taarifa zake zilizotokana na uchunguzi wa TRA naamini zilimfungua au zinapaswa kumfungua Kakobe macho ya nini kinachoendelea bila yeye kujua. Kaka wa Mkewe anatajwa sana kushiriki kukwapua ukwasi wa Kanisa bila Kakobe kufahamu.

Mtoto wa kwanza wa kiume aitwaye Frank Zacharia alifukuzwa na kutengwa na famikia na kanisa zaidi ya miaka 15 sasa ambapo kwa kuwa alipatikana kabla Askofu hajamuoa mkewe wa sasa amekuwa anaishi katika mazingira ya ajabu yasiyoeleweka huku akiwa amemtelekeza mkewe na wanae ambao wamekataliwa kutambuliwa na familia ya Kakobe hivyo kuishi kwa dhiki kubwa.

Kuna mengi behind the family na hayasemwi kokote na nguvu kubwa inatumika kuyazima yasijulikane.

Kikubwa hapa ni kuona imani sasa imekuwa Kali mno. Upendo ulioletwa na Yesu umegeuka fimbo na ubaguzi. Sidhani kama yule mwanamke mzinzi aliyepelekwa kwa Yesu alimkataa kwa vidani na mapambo yake, alimkomboa na adhabu ya kifo na akamsamehe dhambi zake.

Mungu amsaidie Askofu kuelewa kuwa injili ya Yesu inapaswa kusikilizwa na watu wote ili kuwasaidia kufikia maamuzi ya hiyari
 
Naamini Mungu yupo lakini siamini katika madhebu yoyote tuliyo nayo, huwa nawaona kama maruki tu na wachumia tumbo...na huwa wananiudhi sana watu ambao watakuja kwangu kwa lengo la kunihubiria jambo la kiroho.
 
naamini Mungu yupo lakini siamini katika madhebu yoyote tuliyo nayo...huwa nawaona kama maruki tu na wachumia tumbo, na huwa wananiudhi sana watu ambao watakuja kwangu kwa lengo la kunihubiria jambo la kiroho.
Toa location tuje kukupa Neno la Bwana.

Acha zako
 
Msanii,

Pepo mchafu toka
Pepo la unafiki toka!
Namkemea pepo aliyemshika Kakobe . Kakobe ni mnafiki(hii si sifa ya Mungu bali ya kipepo).

Alijiinua kutafuta utukufu kwa kushindana na serikali, alipoona ameshindwa akaanza kuisifia Serikali.

Kuna jamaa mmoja mgonjwa alitengwa pale kwa kutokutoa 10% huku alishatoa taarifa kuwa ni mgonjwa daktari kamwambia asifanye kazi kwa miezi 8. Wakamtimua.
 
Msanii,

Pepo mchafu toka
Pepo la unafiki toka!
Namkemea pepo aliyemshika Kakobe . Kakobe ni mbafiki(hii si sifa ya Mungu bali ya kipepo).

Alijiinua kutafuta utukufu kwa kushindana na serikali, alipoona ameshindwa akaanza kuisifia Serikali.

Kuna jamaa mmoja mgonjwa alitengwa pale kwa kutokutoa 10% huku alishatoa taarifa kuwa ni mgonjwa daktari kamwambia asifanye kazi kwa miezi 8. Wakamtimua.
Aisee!
 
Msanii,

Mwambie Kakobekuna ndege nyingine zinakuja ajiandae kwenda kuzipokea.

Mwambie pia hatujui Azory Gwanda yuko wapi.

Ben Saanane yuko wapi hatujui.

Tundu Lissu kafanyiwa ukatili kama kama chatu.

Hayo mambo yote yana baraka za Jiwe.

Na kwanini hayo makanisa yao hayatoi hata msaada wa gunia la mahindi kwa watoto yatima
Fungua Uzi wako tuje tuchangie,usiwe Kama kibakuli Cha vumba hujifichi popote wajitokeza
 
Back
Top Bottom