Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,603
- 29,743
Leo ni siku ya Jumapili siku ya Bwana kwa sisi wenye imani ya Kikristo, hasa born again.
Nimetoka zangu kigamboni, nikavuka maji nikiwa na dhamira ya kupata Neno lisilogoshiwa kwenye huduma ya Full Gospel Bible Fellowship Churh pale Mwenge. Niliambatana na mke wangu.
Lengo langu ni kupata Neno ili niweze kuimarika kiimani na kujitathmin kama nipo raiti traki kwenda Mbinguni.
Naelewa sana Huduma ya Kakobe, mimi ni miongoni mwa waanzilishi enzi hizo miaka 1984 kisha alipotengana na Rodrick Mmbwambo kutoka The Gospel Evangilical Team (GET) mwaka 1988 kupelekea kuanzishwa kwa kanisa la FGBF pale Mwenge jirani na kanisa Katoliki kabla halijahamia Jamhuri Primary School mjini.
Naelewa msimamo wa kanisa lake. Naelewa viwango vya mahubiri alivyo navyo.
Nilichostuka leo ni kwamba, kutoka kwenye viwango imeelekea kuwa kwenye xtremely faith. Imani kali. Mke wangu alifika kanisani pamoja nami akiwa amevaa nguo inayositiri vyema na kilemba kama kawaida ya taratibu za kanisa lake. Neno la leo lilikuwa ni MAVAZI YA MTU ALIYEOKOKA. Neno lilipoanza nikaaona mke anainuliwa na mama mmoja mhudumu na wakatoka nje. Baada ya dakika tano mama yule akanifuata akisema mke wangu ananiita nje. Nikamuuliza kuna tatizo? Akanijibu yes, amesuka rasta na pale hawaruhusiwi waliosuka rasta kwa sababu ni nywele feki.
Nilitoka nje nikamchukua mke wangu na kuondoka. Alijiona mkosaji nikamwambia kuwa Yesu wetu alikaa na wenye dhambi hakuwabagua lakini sisi ambao ndiyo wanafunzi wake tumevuka viwango kiasi kwamba inakupasa ujitakase kwanza kabla ya kutakaswa na Yesu.
Wakati naingia nilishuhudia baadhi ya waumini wakiingia wakiwa na nguo ambazo hazina viwango na wengine unaona kabisaa wamejichubua ngozi.
Kwa namna nifahamuvyo ni kwamba ili mtu abadilike anahitaji kufundishwa Neno ili hiyari yake ifikie maamuzi ya mabadiliko. Pia kuzuia watu wasiingie kanisani kwa sababu ya kutokidhi vigezo vya kanisa ni kuwabagua na kuwatenga na Kristo kwa sababu haiwezekani mtu asiyeamini akaanza kufuata masharti ya kanisa kama hajafikiwa na Neno.
Jambo lingine ninalojiuliza kwa waamini wenzangu humu ni kwamba, ikiwa fedha, almasi na dhahabu ni mali ya Mungu na havijatajwa kama ni sehemu ya dhambi, je Kibiblia mali hizo zinatumikaje kwa utukufu wake? Watu wanazitaja kwenye mafundisho lakini hata kuvaa kidani au pete za vitu hivyo ni dhambi?
Leo sijamuabudu Mungu kwa kuwa nimenyimwa fursa hiyo.