Nina miaka mingi tangu nilipokwenda kanisani kusali tofauti na kusindikiza maharusi. Mimi hupinga ulokole kwa sababu ni brainwashing na haina tofauti na uganga wa kienyeji.
Lakini kuna wakati nasikiliza mahubiri ya walokole kwenye tv. Baada ya muda sasa nimegundua yafuatayo;
1. Kuna wahubiri ambao wanaigiza, wanapiga kelele hovyo hovyo
2. Kuna wahubiri wanahubiri chuki dhidi ya wenzao na hawa hawana mantiki
3.kuna wahubiri wanaosoma biblia peke yake, inawezekana hata magazeti hawasomi hivyo wana uchambuzi mwembamba sana kuhusu maisha na utawala wa nchi
4. Kuna kakobe peke yake, anasoma tafiti na nadharia nyingi na anachambua mambo kwa upana sana. Anajua sana kupangilia hoja kimamtiki. Lakini mwisho humalizia na vile vitendo vya uganga wa kienyeji - majini, maradhi, ajira, kutozaa, n.k
tangu wiki mbili zilizopita kakobe amekuwa akitoa elimu pana sana ya uraia kusaidia upigaji kura kwa kuchambua hoja badala ya kushabikia.
Ndiyo maana nasema askofu kakobe Jana Leo na kesho. Naomba aendelee hadi siku ya tarehe 30 October. Anatoa elimu pana yenye mantiki zisizo na ukakasi. Anafanya kazi waliyoshindwa NEC na TAKUKURU. Jana na leo kapiga shule ya rushwa elimu ambayo inatoboa mfupa. Anatumia tv ya channel ten
Asante askofu kakobe, anatoa mchango mkubwa sana kwa gharama kidogo wakati serikali inatumia mabilioni kwa taasisi ya rushwa ili isimamie na kuwalinda wala rushwa.
Siyo kila kifanywacho na viongozi wa dini ni udini
namkubali.
jamaa ni mshindi kwa ushawiwshi.
amefanya kazi nzuri kweli kweli
Kakobe ni mdini na opportunisty mfano mwaka 1995 alisema A.L Mrema ni chaguo la mungu na amepewa maono kuwa lazima atakuwa Rais wa Tanzania, Kakobe akaacha kazi ya kanisa akaingia kwenye siasa na kuzunguka na Mrema nchi nzima. Wote tunajua Mrema alishindwa vibaya na Kakobe hakusema kitu akanyamaza kimya. 2005 KaKOBE akasema JK ni chaguo la mungu na akashinda. Sasa anawahubiria waumini wake wampigie kura Dr Slaa.
Binafsi naona si sahihi yeye kuwa direct kuwataka waumini mpigie mgombea fulani. Ambacho ]Kakobe na viongozi wa dini wa madhehebu yote walitakiwa kuhamasisha waumini wao kupiga kura kwa mgombea wanae muona anawafaa, kuwe very neutral and objective. Anavyofanya kakobe ni unaweza kutafasiriwa kama udini, ingawa 2005 alimtaka JK hapo tuseme alikuwa fanatic wa JK kwa sababu ya kutaja specifically mtu anaepaswa kuchaguliwa na waumini wake, vivyo hivyo baadhi ya mashekhe
Unakosimamia kunaeleweka. So wewe kusema yote haya mi sishangai.
1.Si kweli kwamba Mrema alishindwa ... aliibiwa kura zake zote. Kama hutaki acha!
2. Sijawahi kusikia akiwadirect waumini wake wamchague Dr, slaaa ... hizo ni conclusion zako based ktk mtizamo wako mfinyu wa kidini.
3. unasema ni "opportunist" , kwa vipi? hategemei ruzuku kutoka serikalini na serikali haimpi msaada wowote, sasa ajikombe ili apate nini?
Kakobe ana elimu nzuri ya kuona mamboa kwa mapana yake, lakini ni opportunist na mbinafsi anayetafuta manufaa yake binafsi kwa kupitia migongo ya wafuasi wake.
Leo Lusekelo kamcrush Kakobe indirectly kwa kuondoa ibada Jpili ijayo kwa ajili ya uchaguzi akisema siasa ni mambo ya mpito ila Mungu ni wa milele