Askofu: JK ana joho la Mungu

Askofu: JK ana joho la Mungu

KATIBU Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), Askofu Dk. David Mwasota amesema Mungu amemvisha Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete joho la ufahamu na ujasiri kumuwezesha kupambana vita ya kukisafisha chama hicho na Serikali yake.

Askofu huyo alisema hayo baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujivua gamba hivi karibuni. Amesema Rais Kikwete na CCM mpya ndio watakaoibuka washindi katika vita hiyo inayoendelea sasa baina yake na wanachama waliopewa siku 90 kujiondoa katika nafasi zote
za uongozi kutokana na kutajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na HABARILEO Jumamosi mjini Dar es Salaam, Askofu Dk. Mwasota alisema Rais Kikwete atashinda vita hiyo kwa vile maaskofu hivi sasa wanakesha kumuombea kwa Mungu ashinde ili kukirejesha chama hicho kikongwe katika mikono ya wanyonge.

"Kama kuna kipindi Rais Kikwete ametufurahisha maaskofu basi ni kipindi hiki. Hatuna sababu ya kupata tafsiri ya nini maana ya kujivua gamba, lakini kitendo alichokifanya hivi karibuni cha kusimamia mabadiliko makubwa ndani ya CCM ili kukiosha chama hicho dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi ni cha kijasiri.

"Kugundua uovu na kupambana nao ni hekima inayotokana na Mungu. Mungu amempa ufahamu na ujasiri wa kuanza kuchukua hatua.

Mwanzo tulikuwa na shaka kama anafahamu mambo yanayoendelea, baadaye tukalaumu kwa kushindwa kuchukua hatua hata pale tume anazounda zinapomweleza hali halisi ilivyo, sasa amechukua hatua nashangaa na nasikitika sana kuona kuna watu wanalaumu na kubeza hatua hiyo tena," alisema.

Askofu Dk. Mwasota alisema maaskofu pia wameridhishwa na ahadi kwamba hatua kama zilizochukuliwa na Rais Kikwete kwenye chama, zitachukuliwa pia kwa viongozi wa serikali wanaotajwa kuhusika na vitendo vya rushwa na ufisadi.

"Sasa Rais wetu amevalishwa na Mungu, joho la ufahamu na ujasiri, ingawa vita ni kali, lakini atashinda. Ni kupitia kwa Rais Kikwete ndio nchi itatakasika kutokana na maombi, na Biblia inasema hivyo kwamba Rais wa nchi ndiye atakayeifanya nchi kutakasika au la, kutokana na kutokumbatia dhambi."

Askofu David Mwasota kwa hili na hii kauli itakubidi utoke nje kwa jamii ya waaminio na kutubu kwao kuwa umewakwaza kwa maneno yako na kuwasababisha wamkosee Mungu kwa manung'uniko. Ndiyo utaendelea kunung'unukiwa na kuipoteza heshima yako.

Je! Tukiwauliza maaskofu wote wa Kipentekoste watakubaliana na kauli yako? Je! Tukiwauliza wachungaji wote (maana nawe ni Mchungaji kihuduma, uaskofu ni cheo tu cha kuchaguliwa) wa Kipentekoste unafikiri ni asilimia ngapi watakuwa upande wako? Kwa washirika sifiki kwasababu itakuwa AIBU.

Unaposema "Mungu amemvisha Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete joho la ufahamu na ujasiri kumuwezesha kupambana vita ya kukisafisha chama hicho na Serikali yake." una maana gani na umeweka msingi gani katika hizo kauli zako? Ngoja tuzichambue kidogo kwa jicho la kithiolojia yenye mtazamo wa imani ya kikristo:-
1.Mungu -> Mungu gani unayemtaja hapa maana inajulikana kuna miungu mingi. Mungu mwenye mapenzi na chama cha siasa , ndiyo mungu mwenye mapenzi na CCM pamoja dhuruma yote waliyoifanya kwa waja wake watanzania.

2. amemvisha joho la ufahamu na ujasiri-> ili Mungu mwenye enzi, YEHOVA, amviku mtu joho la utukufu kwa kazi yake au kusudi lake mtu muhusika inabidi aweje? Ama atengenezwe vipi? Soma kitabu cha Mithali sura 1-4 halafu utueleze ili mtu apate ufahamu ni jambo gani muhimu kufanyika. Halafu tulinganishe Kikwete analo? Na itakapotokea kuwa matokeo ya maamuzi yaliyochukuliwa yakawa na madhara makubwa kuliko ilivyosasa utakubali kusema alivikwa roho/joho ya upumbavu na woga? Napata shida sana na kauli hizi.

3. kupambana vita vya kukisafaisha CCM na serikali ...ingawa vita ni kali, lakini atashinda->
Hivi CCM ikisafishwa YEHOVA atakuwa ametukuzwa ama watu wakisafishwa mioyo yao ndipo atakapokuwa ametukuzwa? Je! CCM ni takatifu kwa BWANA Mungu?
Hivi Kikwete anapamabana vita ya haki ama anakazana kuona hila (conspiracy) inatimia? Ninyi maaskofu mmewauliza waumini wenu ili mkajue kuwa hii ni vita ya haki ama mna hila? Vema, labda pengine umekataa kuiita hila ni hila.."Do not call conspiracy everything this people calls a conspiracy;" Isaiah 8:12a. Tukilipa muda suala hili, na ikatokea akashindwa kukisafisha chama na serikali yake yake mtasema nini? Maana umekwisha hitimisha atashinda.

4. Rais Kikwete atashinda vita hiyo kwa vile maaskofu hivi sasa wanakesha kumuombea kwa Mungu ashinde->
Sambamba na hoja ya hapo juu, atakaposhindwa Kikwete katika "hila" hii, tukisema mlikuwa mnamwomba Shetani mtakataa? Tukisema maaskofu ni waongo hamjui kuomba mtabisha? Mkisema hayakuwa mapenzi ya Mungu kujibu kwa wakati huu aliliruhusu hili lipite; tutawaambia wanafiki ninyi, maana mliomba kwa tamaa zenu na si sawa na mapenzi ya BWANA Mungu ndiyo maana hamkupata.
Hivi mambo yote mazuri yenye kumpa Mungu utukufu katika Tanzania yanatukia kwasababu Maaskofu wameombea?
Behold, "kiburi hutangulia maangamivu".

Maaskofu, zichambueni sana kauli zenu kabla ya kuzitoa. Inatuuma pale/kutokana na ukweli uliopo, kauli zenu kuitwa ni uropokaji[/B; hivyo ninyi kuitwa waropokaji. Kwa uchache ona kauli zenu zinavyoligharimu kanisa;
"Hata watanzania wote wakiihama, mimi nitabakia kuwa mwana-CCM''..Kulola
"Jakaya Kiwete ni chaguo la Mungu"...Kilaini
" Mungu amemvisha Rais Jakaya Kikwete joho la ufahamu na ujasiri kumuwezesha kupambana vita ya kukisafisha CCM na Serikali yake"...Mwasota.

Mnatukwaza sana. Mnatuuumiza sana.
Mnafanya tushambuliwe sana kutokana na kauli zenu.
Ninyi ni viongozi.


Nimeyaandika haya kwasababu najua kuna waumini,wachungaji na maaskofu wengi wanasoma JF na wengine ni members.
 
Ubarikiwe askofu,ongezeni maombi kwani kuzaa si kazi, kazi kulea mwana. Mwombeeni Rais.
 
Zile kauli mbiu za wana JF za wamepikiwa pilau au wamenunuliwa mbona sizioni? au zina apply kwa upande wa pili tu?
 
Mara zote nilikua naamini kwamba darasa la 4 la mkoloni ilikua elimu bora sana kuliko hata form 4 wa sasa....nina mashaka Askofu huyu hatendei haki wahitimu wenzake wa darasa la 4 la mkoloni....
 
Kwa kweli mimi sijaona huo ujasiri wa Jk anaousemea askofu. Kitu ninachoweza kuona hapa ni jk kuvuviwa ujasiri ambao hana na kumsababishia maumivu makali atakayopata kutoka kwa RACHEL. Kama kweli Jk katangaza nia ya kuwawajibisha RACHEL ijapokuwa haikuwa direct speech bali indirect, basi anakabiliwa na magumu kote kote. Akiwaondoa RACHEL chamani watamgharimu kwani yeye binafsi ni sehemu ya ufisadi wao Ref, Epa. Akiwaacha wao ndio watakaomwondoa kwani ameruhusu wachafuliwe na jamii kwa kuhusishwa na gamba linaloisumbua nyoka ccm. Na akiacha wakati ujisemee wenyewe kwa nia ya kufuata upepo wa jamii inarespond vipi basi jamii haitamwelewa Jk kwani itamwona kama mtu aliyeanzisha vita bila ya kuhesabu gharama na hivyo watamtaka yeye pamoja na watuhumiwa wake wakiachie chama.
Utakatifu ni zaidi ya watu wanavyowazia, yahitaji kujikana haswa na kuubeba msalaba wako mwenyewe kama umekataa Yesu akubebee kwa kujisalimisha kwenye KWELI.
Kweli ni nini....???
.

Japo wanadamu wanajidai ni wasanii nadhani hakuna mcheza mzuri wa drummer kama Mungu. Aki ochestrate kitu hakuna wakukipangua unajikuta wewe mwenyewe umeingia kwenye kumi na nane na ili usimlaumu anakuacha ujifunge goli ili uelewe vizuri kweli yeye ni Mungu wa Mianga. Kitendo walichokifanya serikali ya CCM na wapambe wao kujisemea kwamba mkuu analindwa na majini ni kufuru ambayo Mungu hawezi kuiacha ikapita bila kujitukuza yeye mwenyewe kwa mikono yake. Wakati huu tutaelewa kweli majini yana nguvu kiasi gani mbele ya Mungu. Mimi kama mhubiri sinabudi kulisema hili bila unafiki wala hofu maana ole nisipolisema hili maana nahesabiwa kuwa nimeipoteza roho isiyo na hatia. Watanzania wote wataelewa kuwa Mungu hadhihakiwi wala hachezewi katika serious issues zinazohusu utawala ambao yeye mwenyewe aliuweka ili kuwe na order.
 
Yaelekea kondoo wa bwana (waumini) wamemshinda kuchunga. Ushauri wa haraka na busara akachunge bata na hizo "snake". Amepata wapi ujasiri wa kuchanganya mavazi ya Mungu na Magamba ya Nyoka. Dunia kiama.
 
Zile kauli mbiu za wana JF za wamepikiwa pilau au wamenunuliwa mbona sizioni? au zina apply kwa upande wa pili tu?
The Prophet said:
Kamwambie njaa zitamuua.

Je!Unazipenda kauli hizo na za namna yake?
Binafsi sizipendi regardless zinatumika upande gani. Hao ni viongozi wa kidini/imani za watu.
 
Askofu David Mwasota kwa hili na hii kauli itakubidi utoke nje kwa jamii ya waaminio na kutubu kwao kuwa umewakwaza kwa maneno yako na kuwasababisha wamkosee Mungu kwa manung'uniko. Ndiyo utaendelea kunung'unukiwa na kuipoteza heshima yako.

Je! Tukiwauliza maaskofu wote wa Kipentekoste watakubaliana na kauli yako? Je! Tukiwauliza wachungaji wote (maana nawe ni Mchungaji kihuduma, uaskofu ni cheo tu cha kuchaguliwa) wa Kipentekoste unafikiri ni asilimia ngapi watakuwa upande wako? Kwa washirika sifiki kwasababu itakuwa AIBU.

Unaposema "Mungu amemvisha Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete joho la ufahamu na ujasiri kumuwezesha kupambana vita ya kukisafisha chama hicho na Serikali yake." una maana gani na umeweka msingi gani katika hizo kauli zako? Ngoja tuzichambue kidogo kwa jicho la kithiolojia yenye mtazamo wa imani ya kikristo:-
1.Mungu -> Mungu gani unayemtaja hapa maana inajulikana kuna miungu mingi. Mungu mwenye mapenzi na chama cha siasa , ndiyo mungu mwenye mapenzi na CCM pamoja dhuruma yote waliyoifanya kwa waja wake watanzania.

2. amemvisha joho la ufahamu na ujasiri-> ili Mungu mwenye enzi, YEHOVA, amviku mtu joho la utukufu kwa kazi yake au kusudi lake mtu muhusika inabidi aweje? Ama atengenezwe vipi? Soma kitabu cha Mithali sura 1-4 halafu utueleze ili mtu apate ufahamu ni jambo gani muhimu kufanyika. Halafu tulinganishe Kikwete analo? Na itakapotokea kuwa matokeo ya maamuzi yaliyochukuliwa yakawa na madhara makubwa kuliko ilivyosasa utakubali kusema alivikwa roho/joho ya upumbavu na woga? Napata shida sana na kauli hizi.

3. kupambana vita vya kukisafaisha CCM na serikali ...ingawa vita ni kali, lakini atashinda->
Hivi CCM ikisafishwa YEHOVA atakuwa ametukuzwa ama watu wakisafishwa mioyo yao ndipo atakapokuwa ametukuzwa? Je! CCM ni takatifu kwa BWANA Mungu?
Hivi Kikwete anapamabana vita ya haki ama anakazana kuona hila (conspiracy) inatimia? Ninyi maaskofu mmewauliza waumini wenu ili mkajue kuwa hii ni vita ya haki ama mna hila? Vema, labda pengine umekataa kuiita hila ni hila.."Do not call conspiracy everything this people calls a conspiracy;" Isaiah 8:12a. Tukilipa muda suala hili, na ikatokea akashindwa kukisafisha chama na serikali yake yake mtasema nini? Maana umekwisha hitimisha atashinda.

4. Rais Kikwete atashinda vita hiyo kwa vile maaskofu hivi sasa wanakesha kumuombea kwa Mungu ashinde->
Sambamba na hoja ya hapo juu, atakaposhindwa Kikwete katika "hila" hii, tukisema mlikuwa mnamwomba Shetani mtakataa? Tukisema maaskofu ni waongo hamjui kuomba mtabisha? Mkisema hayakuwa mapenzi ya Mungu kujibu kwa wakati huu aliliruhusu hili lipite; tutawaambia wanafiki ninyi, maana mliomba kwa tamaa zenu na si sawa na mapenzi ya BWANA Mungu ndiyo maana hamkupata.
Hivi mambo yote mazuri yenye kumpa Mungu utukufu katika Tanzania yanatukia kwasababu Maaskofu wameombea?
Behold, "kiburi hutangulia maangamivu".

Maaskofu, zichambueni sana kauli zenu kabla ya kuzitoa. Inatuuma pale/kutokana na ukweli uliopo, kauli zenu kuitwa ni uropokaji[/B; hivyo ninyi kuitwa waropokaji. Kwa uchache ona kauli zenu zinavyoligharimu kanisa;
"Hata watanzania wote wakiihama, mimi nitabakia kuwa mwana-CCM''..Kulola
"Jakaya Kiwete ni chaguo la Mungu"...Kilaini
" Mungu amemvisha Rais Jakaya Kikwete joho la ufahamu na ujasiri kumuwezesha kupambana vita ya kukisafisha CCM na Serikali yake"...Mwasota.

Mnatukwaza sana. Mnatuuumiza sana.
Mnafanya tushambuliwe sana kutokana na kauli zenu.
Ninyi ni viongozi.


Nimeyaandika haya kwasababu najua kuna waumini,wachungaji na maaskofu wengi wanasoma JF na wengine ni members.


Kubali ukweli kwani chaguo la urais wa JK ni chaguo la Mungu, askofu yuko sahihi kabisa
 
  • Thanks
Reactions: Ame
pale fj hatasifiwa askofu yoyote unless anaisisfia chadema tu. sijui angesema pengo ingekuwaje. natamani ingekuwa hivyo, tuone kama wakatoliki wangeshiriki kumtukana kama wanavyofanya kwa huyu askofu. yaelekea hakuna muumini wake alieiona ile threads. nikipata muda nitaenda kuwauliza waJF nisikie watasemaje. uhhh, lakini mengi mule jf ni mavuvuzela ya chadema. Anyway I will try.
 
Tafadhali hizo ni kauli za mtumishi wa Mungu, hazitakiwi kubezwa!

Mungu huyuhuyu muumba wa Adam na Hawa au mwingine?Hawa maaskofu wanaojipendekeza kwa watawala wa dunia watageuzwa kuni kwenye moto wa milele.
 
miaka yote tunapiga kelele za ufisadi kwa nini huyu askofu asimombee jk afunuliwe macho ana ufahamu wa kuchukua hatua.......askofu achana na ajenda ya siri
 
Kubali ukweli kwani chaguo la urais wa JK ni chaguo la Mungu, askofu yuko sahihi kabisa

mwizi wa kura? tangu lini Mungu akafundisha watu wake kuiba badala ya kukemea wizi? hopeless
 
Askofu hivi kujivua gamba kumebadilisha nini kwenye taswira ya taifa? Jamani tunataka viongozi wa dini wenye uwezo kuona mbali na sio wanaodaganywa na michezo ya kuigiza ya hawa mafisadi. Hili la kujivua gamba si lolote wala chochote bali ni danganya toto. Kama Jk ana nia ya kuwamwaga mafisadi tungeona kwa vitendo sio kuwatisha af wanaendelea kugonga 5 mitaani. Napata uchungu napoona watu wanashidwa kugundua mchezo mchafu wanaocheza wanaccm. Kwa hapa huyu dr. Amejishushia una dr wake.
 
Tulishaambiwa ni chaguo la mungu sio la watz kaeni kimya upepo mbaya upite kama ule wa mwanzo maana maaskofu na manabii tuliambiwa watakuja wauongo ndo kama hawa?

Hivi kwani Jk siyo chaguo la Mungu kweli? Ama kweli preacher inabidi badala ya kuhubiri nifundishe kwanza neno la Mungu maana watu wa Mungu wanapotea kwa kukosa maarifa. Aliyesema JK ni chaguo la Mungu ni nabii mkubwa sana ila ninyi kwakua ni babes kwenye imani ndiyo maana bado macho yenu haya oni vizuri na akili zenu haziwezi kupambanua jema na baya. JK asingekuwa chaguo la Mungu Dr. Slaa asingekuwa maarufu kiasi hiki wala CHADEMA isingependwa na watanzania. Wapendwa njia za Mungu za julikana kwao wamchao na miujiza hupewa wasiokuwa na imani. Musa alimjua Mungu kwa njia zake lakini wanawaisrael walihitaji miujiza ili kumwelewa Mungu yuko vipi na pia kuamini kuwa Musa ndiye kiongozi aliye chaguliwa na Mungu kuwavusha na kuwaongoza kwenda nchi ya ahadi. Msiingie katika dhambi ya kuwa tukana watumishi wa bwana ambao Mungu amewapaka mafuta msije mkaangamia kwa laana ya Mungu. Yoshua na dada yake walipomkebehi Musa kaka yao kwa kuoa mwanamke Muebrania huku sheria za kiyahudi zikikataza makuhani kuoa nje ya kabila la Israel walipigwa na Mungu na actually ilitakiwa wafe lakini kwa rehema za Mungu ilibidi mkosaji Miriamu apigwe kwa ukoma wa ngozi mpaka walipotambua na kutubu na huyo huyo Musa ilibidi awaombee rehema kwa Mungu.
 
Back
Top Bottom