Askofu: JK ana joho la Mungu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu: JK ana joho la Mungu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lilombe, Apr 23, 2011.

 1. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KATIBU Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Pentekoste Tanzania (PCT), Askofu Dk. David Mwasota amesema Mungu amemvisha Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete joho la ufahamu na ujasiri kumuwezesha kupambana vita ya kukisafisha chama hicho na Serikali yake.

  Askofu huyo alisema hayo baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kujivua gamba hivi karibuni. Amesema Rais Kikwete na CCM mpya ndio watakaoibuka washindi katika vita hiyo inayoendelea sasa baina yake na wanachama waliopewa siku 90 kujiondoa katika nafasi zote
  za uongozi kutokana na kutajwa kuhusika na vitendo vya ufisadi.

  Akizungumza katika mahojiano maalumu na HABARILEO Jumamosi mjini Dar es Salaam, Askofu Dk. Mwasota alisema Rais Kikwete atashinda vita hiyo kwa vile maaskofu hivi sasa wanakesha kumuombea kwa Mungu ashinde ili kukirejesha chama hicho kikongwe katika mikono ya wanyonge.

  “Kama kuna kipindi Rais Kikwete ametufurahisha maaskofu basi ni kipindi hiki. Hatuna sababu ya kupata tafsiri ya nini maana ya kujivua gamba, lakini kitendo alichokifanya hivi karibuni cha kusimamia mabadiliko makubwa ndani ya CCM ili kukiosha chama hicho dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi ni cha kijasiri.

  “Kugundua uovu na kupambana nao ni hekima inayotokana na Mungu. Mungu amempa ufahamu na ujasiri wa kuanza kuchukua hatua.

  Mwanzo tulikuwa na shaka kama anafahamu mambo yanayoendelea, baadaye tukalaumu kwa kushindwa kuchukua hatua hata pale tume anazounda zinapomweleza hali halisi ilivyo, sasa amechukua hatua nashangaa na nasikitika sana kuona kuna watu wanalaumu na kubeza hatua hiyo tena,” alisema.

  Askofu Dk. Mwasota alisema maaskofu pia wameridhishwa na ahadi kwamba hatua kama zilizochukuliwa na Rais Kikwete kwenye chama, zitachukuliwa pia kwa viongozi wa serikali wanaotajwa kuhusika na vitendo vya rushwa na ufisadi.

  “Sasa Rais wetu amevalishwa na Mungu, joho la ufahamu na ujasiri, ingawa vita ni kali, lakini atashinda. Ni kupitia kwa Rais Kikwete ndio nchi itatakasika kutokana na maombi, na Biblia inasema hivyo kwamba Rais wa nchi ndiye atakayeifanya nchi kutakasika au la, kutokana na kutokumbatia dhambi.”

  Akizungumzia habari iliyoandikwa na gazeti moja la kila siku litolewalo kwa lugha ya Kiswahili
  (Si HABARILEO), kwamba alitoa kauli iliyomshutumu, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kuwa anatoa kauli za matusi dhidi ya viongozi wa dini, Askofu Dk. Mwasota alisema habari hiyo ilipotoshwa.

  “Namfahamu Nape ni mtu mzima, ni mtu msomi na ni mtu makini, najua anachokisema katika mikutano ya hadhara ya CCM kuhusiana na ufisadi ana ushahidi navyo, hakuna matusi aliyoyatoa nakumbuka nilimwambia hivyo mwandishi huyo, lakini nashangaa kilichoandikwa.

  “Nchi inaweza kuingia katika machafuko kutokana na kuwepo kwa uwezekano wa watu mbalimbali kama wanasiasa, wasanii na vyombo vya habari kuzusha madai yasiyo ya kweli kwa lengo la kukinufaisha kikundi fulani cha watu au chama cha siasa wakati habari hizo zimepotoshwa.”

  Alisema maaskofu wanao utaratibu wa kutoa kauli zilizofanyiwa utafiti wa kina bila kukurupuka baada ya sekretarieti kuyachuja na kuyafanyia kazi mambo ambayo yanaonekana kutishia uhai wa Taifa na watu wake.

  “Mimi si msemaji wa Sekretarieti ingawa ni Mratibu. Tunapotamka jambo ujue tuna ushahidi nalo.Tumesali sana na leo kilio chetu kimesikika kwa Mwenyezi Mungu kumvisha Rais wetu, joho la ufahamu na ujasiri ili kupambana na rushwa na ufisadi, tunafurahi sana kwa hatua hii,” alisema.

  Katika matamshi yake ya hivi karibuni, Nape ameeleza kuwepo kwa njama zinazopangwa na wanaCCM wanaoshutumiwa kuhusika na ufisadi, za kutaka kumchafua Rais Kikwete na familia yake.

  Nape alisema ili kufikisha uzushi huo kwa wananchi, watuhumiwa wa ufisadi watawatumia
  viongozi wa dini, wanasiasa, wasanii na vyombo vya habari, lakini akawataka wananchi kupuuza uzushi huo na kusema CCM itapambana kwa nguvu zake zote ili kuhakikisha njama hizo hazifanikiwi.

  Tangu kufanyika kwa mabadiliko ya uongozi ndani ya CCM ulioshuhudia Sekretarieti yote, chini ya Yusuf Makamba kujiuzulu, huku baadhi ya wanachama wenye madoa ya kisiasa wakionywa kujisafisha wenyewe au kujiondoa katika chama, kumekuwa na mitazamo tofauti, hasa kutoka kwa baadhi ya watuhumiwa ambao kwa sasa wanadaiwa kutafuta njia za kujinasua. SOURCE HABARI L|EO, 23/04/2011


  WATZ TUMPE MOYO NA KUMUONGEZEA UJASIRI JK AWASHINDE MAGAMBA. CDM KWA HILI MUONGE MKONO KWA FAIDA YA TANZANIA
   
 2. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  toeni upumbavu wenu hapa. Joho la Mungu lina fananaje? lina rangi gani?

  foolish!!
   
 3. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Hata Saul alikuwa mpakwa mafuta lakini Mungu alifikia wakati akamkataa kutokana Magamba yake.
  Nyoka ni nyoka tu hata Kama atajivua Gamba atabaki kuwa nyoka tu,hata Kama watampaka mafuta atabakia nyoka tu.
   
 4. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tafadhali hizo ni kauli za mtumishi wa Mungu, hazitakiwi kubezwa!
   
 5. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kamwambie njaa zitamuua.
   
 6. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Matendo yake yanaonyesha hana Joho la Mungu maana tutawatambua kwa matendo yao,Ufisadi hata Dowans si Joho la Mungu.
   
 7. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Huyu Mchungaji alituhumiwa kumwibia mzee wa Upako mwaka jana;

  Askofu, Mchungaji mbaroni

  · Posted by GLOBAL on October 12, 2010 at 9:00am

  TUKIO la hivi karibuni la kuvamiwa kwa Mchungaji wa Kanisa la Maombezi Utashinda, Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako (pichani) na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi limechukuwa sura mpya baada ya watumishi wawili wa Mungu kuhojiwa. Waliohojiwa katika tuhuma hizo nzito za kuvamiwa kwa Mzee wa Upako na kuibiwa mamilioni ya shilingi ni Askofu David Mwasota na Mchungaji Frank Chacha ambao wanatoa huduma kwenye kanisa la Naioth Gospel Assembly lililopo Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam.

  Vyanzo vyetu vya habari vilidai kwamba Mchungaji David Mwasota alikamatwa na polisi na kuhojiwa kwa zaidi ya saa 6 katika Kituo cha Mbezi jijini Dar es Salaam kuhusiana na tukio hilo na kutakiwa kumfikisha katika kituo hicho Mchungaji wake Frank Chacha. Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, inadaiwa kuwa mara baada ya Askofu Mwasota kumfikisha kituoni hapo, Mchungaji Chacha alihojiwa kwa siku mbili mfululizo bila kupata dhamana kwa madai kwamba kama angeachiwa haraka angevuruga upelelezi wa polisi.

  “Baada ya Askofu Mwasota kumfikisha Chacha kituoni hapo, Mchungaji huyo alishikiliwa kwa muda wa siku mbili akihojiwa,” kimoja cha chanzo chetu ambacho tunakihifadhi jina lake kilisema. Iliendelea kudaiwa kwamba Mzee wa Upako alihisi kuwa Mchungaji Chacha alihusika na tukio hilo kutokana na ujumbe mfupi wa maneno (SMS) aliomtumia, hivyo akaamua kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.

  Inadaiwa kwamba ujumbe uliotumwa kwenda kwa Mzee wa Upako ulikuwa ni wa kumpa pole kuhusiana na tukio la kuvamiwa na majambazi kisha kuporwa mamilioni ya pesa usiku wa kuamkia Septemba 27, mwaka huu. Hata hivyo, vyanzo hivyo vilisema kwamba ujumbe aliotumiwa Lusekelo haukuwa na nia mbaya ila aliutilia mashaka kwa kuwa ulimuuliza kama alimkosea Mungu kutokana na kukumbwa na balaa hilo.

  “Hilo la kuambiwa kwamba amemkosea Mungu ndilo lililomfanya mtumishi huyo kuona kama vile alikuwa akifanyiwa dhihaka katika tukio hilo la kuibiwa pesa,” kilidai chanzo chetu. Inadaiwa kuwa Mzee wa Upako alishindwa kuelewa maana ya ujumbe huo na kuhisi kufanyiwa dhihaka na mtumishi mwenzake Chacha ambaye hakuwa na lengo baya. Aidha, chanzo hicho kilisema kwamba hii ni mara ya pili kwa Mzee wa Upako kumtuhumu Mchungaji Chacha ambaye zamani alikuwa anatoa huduma katika kanisa lake kabla ya kutokea hali ya kutoelewana ambapo alihamia kwa mlezi wake Askofu Mwasota.

  “Inawezekana ana bifu na Mchungaji Chacha kutokana na kuondoka katika huduma yake ndiyo maana ameamua kufanya hivyo, ni jambo la kusikitisha watumishi kupelekana polisi na haya siyo maadili ya kitumishi kabisa,” kiliendelea kusema chanzo hicho.

  Kwa upande wa Askofu Mwasota alisema kwamba baada ya kutoka kituoni kesho yake (Jumanne) alimfuata Mchungaji Chacha na kumpeleka Kituo cha Polisi Mbezi ambapo alikaa kwa muda wa siku mbili ndipo alimtoa kwa dhamana.

  “Mzee wa Upako ni mwanangu na sijagombana naye na sina matatizo naye, ila sijui kwa yeye na Mchungaji Chacha wana matatizo gani kwa sababu walikuwa watu wa karibu, nitaongea naye vizuri nijue tofauti zao,” alisema Askofu Mwasota.

  Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga alipopigiwa simu siku ya Jumapili kuzungumzia sakata hilo alisema bado analifuatilia na tulipomtafuta kabla ya gazeti hili kuingia mitamboni simu zake zote hazikupatikana.
   
 8. A

  Ame JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Nabii acha hasira joho limevalishwa cheo ambacho ni ktakatifu si nafsi ya mtu; mtu anabaki kama amalivyo mpaka atubu na kweli kwa dhamira njema huku akirudisha kila alicho dhulumu na kuomba msamaha wote aliowakosea. Wewe ni nabii ukisemacho wether negative ama positive lazima kiwe so learn to use your mouth positively to take any issue in the direction you want for your own benefit bila kujali aliyeanzisha.

  Si unafahamu Daudi hakumdhuru Saul hata pale alipopewa nafasi ya kufanya hivyo na Mungu pale kwenye pango? Aliheshimu ufalme na mafuta yake japo alijua aliyekalia hicho kiti roho ya mungu imeshamtoka. Tuna haki ya ku exploit kila kilicho haki yetu lakini hukumu ni ya bwana awezaye kuhukumu na kutenda kwa haki. Wakati wa bwana ndiyo wakati ufaao zaidi. Sisi tumepewa neema ya uvumilivu ili bwana atende kwa muda na wakati unaofahaa zaidi kupata perfect will of God. Anasema japo kuwa mnaenda kwenye nchi ya ahadi huko kuna mhiti and the like nami nitawaacha waendelee kuitunza nchi na kuwaondoa mmoja mmoja mpaka mtakapo kuwa na full control.

  Tukiambiwa na bwana tuue wote na kuwamaliza twafanya sawa sawa na neno lake bila huruma. Tukiambiwa tuwaondoe taratibu mmoja baada ya mwingine pia twa tii. Huyo ni mpakwa mafuta wa bwana ni sehemu ya mdomo/sauti ya Mungu kwetu so ni vyema tukawa watii maana kutii ni bora kuliko sadaka.
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Mwasota elewa kuwa kondoo wa bwana wa sasa ni werevu sana, kwa hali hiyo na wewe mchungaji inabidi uwe mwerevu. Usipoangalia kondoo wako wote watachukuliwa na mbwa mwitu. Maneno yako ni kiashiria cha kuruhusu wana kondoo wa Bwana wapotee njia.

  Mwasote amka kabla mambo hayajaenda kombo.
   
 10. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wakuu wa dini wabadilishe mienendo yao, huyu jamaa anajipendekeza kwa mtukufu rais na chama.
  labda njaa ya kukua haraka.
   
 11. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Huyu askofu anaumwa nini?

  Hizi sanaa za JK ndo za kusifiwa namna hii...

  Fyuuuuuu....
   
 12. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ninaomba kutofautia na huyu askofu. Kama huyu askofu alikuwa akiyaona aya haya yote yakifanyika ndani ya taifa hiki na yeye akaishia kusali tu bila ya kukemea basi tunahitaji neema.
  Kuna haja ya kuwahoji hawa viongozi wa dini wanapokuwa wanatoa kauli za namna hii. Ni Mungu yupi anashughulika na watu wanaojifananisha na nyoka, kwani nyoka akivua gamba anageuka kuwa samaki! Askofu tafadhali! Kumbuka mahospitali hayana dawa, elimu bila waalimu, barabara kama zimepigwa mabomu, umeme ni mwendo wa madili, kwenye madini ni shmba la bibi,orodha ni ndefu. Je, yote haya askofu huyaoni. Tembelea Ocean road hospital ni zaidi ya mwezi sasa machine ya mionzi ni mbovu pana umbali gani toka magogoni?
  Kuna haja ya kujitafakari kabla ya kuingia na kucheza huu mdundiko au mchiriku wa kujivua gamba. Naomba kuwakilisha
   
 13. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  mtumishi wa Mungu yupi?,Mungu anapenda binaadamu wake wapate mlo mmoja kwa siku huku baadhi wakishibisha matumbo yao na kusaza!Huyo mtumishi wa Mungu hajui shida za wananchi,"NJAA ITAMUUA"
   
 14. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #14
  Apr 23, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Hatudanganyiki hata kidogo wewe na yeye lenu moja ktk dhamira au kifikra.Juzi tu tuliona ktk vyombo vya habari mama mjamzito alifariki kwa kukosa huduma wakati mabilioni kila siku yanaibwa na viongozi wetu.
   
 15. M

  Mindi JF-Expert Member

  #15
  Apr 23, 2011
  Joined: Apr 5, 2008
  Messages: 1,393
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  Kwa kutumia utaratibu wetu wa siku hizi, kauli ya "Askofu" huyu ni "kuchanganya dini na siasa" haswaa, mchana kweupe. Naam, maana mtu yeyote wa dini akizungumzia mambo ya siasa, huwa tunamtuhumu kwa kuchanganya dini na siasa, kuleta machafuko, na kutuvurugia amani na utulivu wetu uliojengeka toka enzi. ila huwa tunachagua. kama akikosoa, basi ndio anachanganya dini na siasa. ila akisifiasifia kama huyu "Askofu", "Mtumishi wa Mungu", basi hata kama background yake ni shaky kiasi gani, kauli yake itapewa uzito mkuubwa na magazeti yetu "matukufu". kwa hiyo basi, kwa utaratibu wetu inavyoonekana, kukosoa kokote, ni kuvuruga amani na utulivu, na kama anayefanya hivyo ni mtu wa dini, basi anachanganya dini na siasa! Huu ni uzandiki wa hali ya juu. na hatua kama hizi za vyombo vya habari kama hivi kurukia kauli yoyote, ali mradi tu inasifia wakubwa na kuwapandisha gredi, kuipa umuhimu mkubwa, ni kielelezo cha kiasi gani viongozi wetu wameishiwa na kufilisika mbele ya jamii. wanahitaji kupandishwa na kutegemezwa hata kwa majani makavu na makuti!
   
 16. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #16
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,201
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli mimi sijaona huo ujasiri wa Jk anaousemea askofu. Kitu ninachoweza kuona hapa ni jk kuvuviwa ujasiri ambao hana na kumsababishia maumivu makali atakayopata kutoka kwa RACHEL. Kama kweli Jk katangaza nia ya kuwawajibisha RACHEL ijapokuwa haikuwa direct speech bali indirect, basi anakabiliwa na magumu kote kote. Akiwaondoa RACHEL chamani watamgharimu kwani yeye binafsi ni sehemu ya ufisadi wao Ref, Epa. Akiwaacha wao ndio watakaomwondoa kwani ameruhusu wachafuliwe na jamii kwa kuhusishwa na gamba linaloisumbua nyoka ccm. Na akiacha wakati ujisemee wenyewe kwa nia ya kufuata upepo wa jamii inarespond vipi basi jamii haitamwelewa Jk kwani itamwona kama mtu aliyeanzisha vita bila ya kuhesabu gharama na hivyo watamtaka yeye pamoja na watuhumiwa wake wakiachie chama.
  Utakatifu ni zaidi ya watu wanavyowazia, yahitaji kujikana haswa na kuubeba msalaba wako mwenyewe kama umekataa Yesu akubebee kwa kujisalimisha kwenye KWELI.
  Kweli ni nini....???
  .
   
 17. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #17
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hawa watumishi njaa bana....
   
 18. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #18
  Apr 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Haya makanisa ya siku hizi ni ya ujasiriamali na wachungaji wao si lolote na wana upeo mdogo sana,kwanza shule zao sijiu kama zinatosha
   
 19. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #19
  Apr 23, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tulishaambiwa ni chaguo la mungu sio la watz kaeni kimya upepo mbaya upite kama ule wa mwanzo maana maaskofu na manabii tuliambiwa watakuja wauongo ndo kama hawa?
   
 20. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #20
  Apr 23, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Duh, njaa mbaya. Hivi huyo askofu anaweza kuthibitisha hayo. Tukimkosoa hatalialia kweli? This is a very poor theology. Hawa ndo viongoz wa dini wanaojali mitumbo yao na kuganga njaa huku waumini wanakufa njaa. To hell with him
   
Loading...