GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,648
- 10,844
Nilikuwa nimesahau kuwa vikao vya bunge vinaendelea Dodoma!
Muda mfupi uliopita niliingia YouTube nikakutana na "title" yenye maneno kama GWAJIMA KIKAANGONI BUNGENI. Nikifikiri kuwa suala la Gwajima limetua bungeni, niliifungua kwa ajili ya kujua kinachojiri.
Kumbe ni uongo mtu! Nilikuta ni kipindi cha bunge live, tena, Mzungumzaji alikuwa akiongelea mada tofauti kabisa ambayo sikumbuki kwa sababu sikuzingatia kuisikiliza.
Nimejikuta ninajiuliza ni nini hasa lengo la kuweka kichwa cha uongo? Wahusika wanaamini kuwa kwa kuweka kichwa cha habari kinachomhusisha Gwajima ndiyo watu watashawishika kuliangalia bunge live kutokea Dodoma?
Ndiyo kusema kwamba kwa sasa Dr. Josephath Gwajima kalizidi bunge kwa umaarufu?