Askofu Gwajima atembea tena baada ya kupooza

Askofu Gwajima atembea tena baada ya kupooza

geomos

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Posts
625
Reaction score
175
Ilikuwa katika ibada ya pasaka ambapo askofu Gwajima akielezea habari ya kupoteza fahamu. Miguu yake ilitetemeka, akasikika akiwaomba wachungaji wake wamshike mkono wa kuume, akisema nataka kutembea, Yesu nimechoka kukalia kiti cha vilema, heri kufa kuliko kukaa hapo. Nimefufua wafu na kuponya wagonjwa siwezi mimi kukaa hapo. Mara akasema, nasikia sauti inasema 'mimi nimeushinda ulimwengu' akaendelea 'roho wa mungu yu juu yangu' ilikua ni jambo la kupendeza sana, Bishop akaanza kutembea mwenyewe. Hallelujah
 

Attachments

  • 1428348210001.jpg
    1428348210001.jpg
    24.5 KB · Views: 7,070
  • 1428348224028.jpg
    1428348224028.jpg
    32.1 KB · Views: 6,711
  • 1428348241958.jpg
    1428348241958.jpg
    49.2 KB · Views: 6,767
Afadhali mungu amejidhihirisha mwenyewe yupo upande gani. Ni kweli Yesu alisema "Mwivi hali bali ili aue, achinje na kuharibu lakini Yesu amekuja wawe na uzima tele. Siku zote shetani huanza halafu mungu hupindua
 
Akasema, habari ya polisi na pengo hataisema tena. Lakini aliahidi ataendelea kuonya yeyote, awe mbunge, waziri, askofu, mkuu wa majeshi au raisi. Akasema 'Hakuna aliyewahi kushindana na kanisa akashinda
 
aiseee hivi wewe mgalatia huyo mgoni Gwajima kakupa nini mpaka akikudanganya lolote unaamini?!
au unaogopa na wewe atakuwa hakuheshimu tena kama Pengo?

#Zitto
 
Akasema, habari ya polisi na pengo hataisema tena. Lakini aliahidi ataendelea kuonya yeyote, awe mbunge, waziri, askofu, mkuu wa majeshi au raisi. Akasema 'Hakuna aliyewahi kushindana na kanisa akashinda

imamu je?.

hata hivyo nimemvulia kofia ngwajima,asee hajambo kwa maigizo ni haki yake ale sadaka za hao wanaomwamini.
 
Jamani mbona haya sasa makubwa Mshkaji anatwmbea tena kweli kama si sinema hao jamaa waliomfanya akawa kilema kwa muda wataingiwa hofu ya Mungu
 
Mmmmhhhhhh!!!!

Mdanganyano... movie prt 2 itaendelea wiki ijayo???
 
Ama kweli wajinga hua wajinga tu hata awe na PhD madhali ni mjinga ataendelea kua mjinga
 
Kwa hiyo wewe uwezo wa mungu wako unaishia kuua tu, ila kuumba wala kuponya hawezi?

Maana yake unataka kusema mungu wako ni mharibifu tu lakini uwezo wa kufanya jema lolote hana? Au kwako mungu ni sawa na binadamu mweye akili nyingi na ushawishi?

Njoo tusemezane, nami nitakuonyesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua!.

Nilisema huyu shetani hajamaliza maigizo na akitoka huko atakuja na mpya. Tz na Africa ni sheeeeeeeedah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom