Wewe unaonekana hata gazeti hujasoma au umesimuliwa, pili upate nafasi ya karibu kumfuatilia Askofu Gwajima, nadhani katika Taifa hili kwa sasa ndiye kiongozi wa dini anayeongoza kwa kukemea wezi, mafisadi, wala rushwa na kila aina ya uovu unaofanywa na serikali.. Askofu Gwajima pekee katika pita pita zangu niliwahi kumsikia akiwataja wezi wa mali za umma na kuwataka wajiwajibishe na wakigoma wawajibishwe tena sio tu kwa kuvuliwa nyadhifa zao bali kwa kurudisha mali walizoziibia taifa hili kwa miaka mingi.
Ukisoma gazeti vizuri, mwandishi ameweka wazi maneno mafupi aliyonukuu toka kwa Askofu, na pia ni jambo la wazi lisilopingika kuwa hakuna njia kuelekea urais pasipo kutumia fedha, huitaji elimu ya ngazi ya phD kufahamu jambo hili. Kwani kinachomtesa Kikwete leo hii ni nini? Kulipa fadhila kwa pesa alizotumia kabla ya kuteuliwa na chama, wakati wa kuteuliwa, baada ya kuteuliwa, kabla ya kampeni na wakati wa kampeni. Kuunda mitandao ya ushindi mambo yote haya hugharimu pesa, tatizo linakuja ni kuwa, "Je, Pesa unazotumia ni pesa halali??" Pia, kwa historia ya Askofu Gwajima angeishakuwa kiongozi huyu tena hata Mbunge kutokana na ushawishi wake kwa watu wengi hapa nchini ila kwakua si mtu wa tamaa na ameweka mbele maslahi ya imani na kazi ya Mungu anayoiyofanya... Kipindi yupo Ubungo kiongozi huyu wa dini angegombea Ubunge asingeshindwa kupitia CCM na yawezekana kukataa kwake ndio sababu ya yeye kuondolewa pale Ubungo kwani alikosesha CCM jimbo.
Wacha ukweli usemwe wazi kabisa, Ni Askofu gani au kiongozi gani wa dini alishakemea serikali juu ya ujenzi wa Misikiti/Makanisa katika public service centres zaidi ya Gwajima??
Truth must be told openly, tuache ushabiki wa kishamba... soma gazeti kwa umakini wacha kukurupuka.