Askofu Gwajima amtetea Lowassa

Askofu Gwajima amtetea Lowassa

dini za siku hizi sipo kisiasa badala inabidi dini za uganga wa kienyeji zifutwe
 
mtumishi nakupongeza unaakili maana unasema ukweli. wenye akili tunaokubali ukweli tumekuelewa
mfumo uliopo ni wa kibepari , maana azimio la arusha hatunalo tena .pesa inatumika kwa wote labla tofauti ni kiasi gani mtu anachotumia katika hili , automatically aliyenazo nyingi atatoa nyingi aliyenacho kidogo atatoa kidogo, acha wajimwage ndio wakati wao. good:embarrassed:
 
Kutenganisha dini na siasa ni kutenganisha roho na mwili.

Maajenti wa Kuzimu wanapiga kelele usichanganye dini na siasa
 
kwenye maeleo hayo yoote sijaona kamtaja na kumtetea Lowasa au?
 
dini za siku hizi sipo kisiasa badala inabidi dini za uganga wa kienyeji zifutwe

Haya ndio mambo ya hadi akili ndogo kutaka kutawala akili kubwa.
Hivi kwa akili zako pasipo viongozi wa dini na dini zenyewe ufisadi, wizi, uonevu na ukatili wa raia hasa watu wanyinge ungekuwa mkubwa kiasi gani? Uwepo wao mara nyingi kwa kuongea hadharani ukweli na kukaripia uovu kunasaidia sana katika kujenga taifa.

Jamani, kwa Tanzania ya leo nani katika kundi la Viongozi wa dini anasema ukweli na kwa uwazi kama Askofu Josephat Gwajima? Nani anafichua hila za viongozi na watumishi wa umma kama yeye?
Lazima tukubali ukweli, pasipo dini na viongozi wa dini kama hawa na wengine uovu na wizi ungekua wa kiwango kikubwa sana.
 
Lowasa kutetewa na gwajima ni jambo la kawaida make yote mafisadi yanajulikana.
 
Lowasa kutetewa na gwajima ni jambo la kawaida make yote mafisadi yanajulikana.

Umesoma habari lakini?? Acha kukurupuka pasipo kusoma habari semwa. Tatizo unafanya comments za wengine kuwa ndio chanzo chako cha habari.

Achana na habari za magazeti ya udaku, elimika, badilika kisha ishi kwa akili na kama mtu unayeufahamu ukweli na sio kudandia comment za watu kuwa ndio chanzo chako cha habari.

Waseme wanasiasa ila achana kabisa na watumishi wa Mungu wote mana hukuwachagua wewe kuifanya kazi wanayoifanya na wala hujui kwanini waliamua kuzifanya kazi wazifanyazo.

Kama Askofu Gwajima fisadi awezaje tena kuwataja waziwazi mafisadi katika ibada zake? Basi ingekuwa kazi nyepesi kwa viongozi wa CCM kuwajibishana ndani ya chama chao kwakua wanawajua mafisadi.

Alichosema Askofu Gwajima ni kuwa "huwezi kuwa Rais pasipo kutumia fedha" sasa hapo uongo uko wapi? Unless uwe ni tahira, jinga, punguani, mnafiki ndio utasema huo ni uongo.

Jipange upya ndio uje, acha kukurupuka
 
jamaa anatega kotekote,sijui nae anataka uwaziri
 
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa mara ya kwanza amejitosa kwenye harakati za Urais kwa kutoa kauli za ukosoaji zinazowalenga baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaoutaka Urais.

Katika mazungumzo yake na RAI, Gwajima alisema kauli zilizotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, Januari Makamba na Waziri Mkuu wa zamani Cleopa Msuya dhidi ya wanasiasa wenzao zina dhamira ovu ya kupakana matope.

Akizungumzia kauli hizo, Askofu Gwajima alisema wanasiasa wanaodai kuchukizwa na mafisadi na kusema kwamba Watanzania wasiwachague wagombea urais wanaotumia fedha, hawana hoja badala yake wanaendesha vita ya Urais.

"Kwani mtu yeyote mwenye akili timamu anajua kwamba bila fedha huwezi kujenga mtandao wa Urais, ili ufanikiwe unahitaji kutumia fedha kujenga mtandao, kwa mfano unahitaji usaidizi wa watu wa Rukwa, Mwanza n.k; lazima uwe na watu huko Rukwa na Mwanza na lazima utoe fedha ili watu hao waweze kusafiri, kula na kulala."

"Bila fedha huwezi kuwaza suala la Urais, maneno yao yanalenga kupotosha watu kwamba wako watu fulani wasiotumia fedha, huku wakijua ukweli kwamba kila mtu anatumia fedha, kwa mfano fomu ya kuwania Urais ni shilingi milioni tano, sasa wao hizo fedha watakuwa wamezipata wapi? Kiujumla, hatua kubwa kama ya Urais inahitaji fedha," alisema.

SOURCE: GAZETI LA RAI ALHAMISI JANUARI 8-14, 2015
Huyo nabii,mtume au askofu atuuleze wana jamvi Nyerere,Mwinyi na Mkapa walitumia kiasi gani kujenga mitandao ya kupata uraisi wa nchi hii? Tafadhali kama ana maslahi katika hili asituchanganye ndugu zetu wakufa mahospitalini kwa kukosa dawa na wenye ukimwi wanapewa dawa za uongo toka kwa rafiki yake madabida,elimu ya msingi,sekondari na vyuo vikuu majanga kama Lowassa anamfaa ampe uaskofu kwenye kanisa lake!kwa hakika sasa siwakati wakuhangaika na watu waina hii!majaribio basi tena,tumesha choka kuibiwa rasilimali za mama TZ
 
Back
Top Bottom