Askofu Eusebius Nzigirwa: Ukichezea thamani ya Binadamu Kanisa litapinga kwa sauti kubwa

Askofu Eusebius Nzigirwa: Ukichezea thamani ya Binadamu Kanisa litapinga kwa sauti kubwa

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mpanda Eusebius Nzigirwa amesema katika kusherekea sikukuu ya Christmas siku hiyo inawakumbusha watu thamani na hadhi ya utu wa mwanadamu na kanisa limekuwa likisimama kukemea kwa sauti kubwa wale wanaojaribu kuuchezea utu wa mwanadamu.

Askofu Nzigirwa amesema hayo Disemba 25, 2025 wakati wa mahubiri ya sikukuu ya Christmas Jimbo la Mpanda ambapo amesema inapotokea mwanadamu yeyote anamdharau binadamu mwingine kwa namna yeyote ni kudharau hadhi na thamani ya binadamu
aliyopewa na Mungu kanisa litapaza sauti kupinga.

"adhimisho hili liwafundishe thamani na hadhi ya mwanadamu na ndiyo maana kanisa limekuwa likitoa sauti kubwa kwa vitendo vya udhalilishaji limetoa sauti kubwa linavyopinga uumbaji ulioumbwa na Mungu kwa thamani kubwa anatokea binadamu anauchezea chezea"

Amesema ni muhimu watu kuzingatia uumbaji wa mungu na kuacha vitendo vunavyokiuka maadili na thamani ya uumbaji ikiwemo wanaume kujigeuza tabia za wanawake na wanawake kujigeuza vitendo vya kiume ni kudhalilisha utu na uumbaji wa Mungu.

Amesisitiza kuwaombea watoto walio katika dhiki katika matumbo ya mama zao ili wanapozaliwa wawe na uwezo wa kustahimili kama ilivokuwa kuzaliwa Kwa Yesu kristo.

Source Jambo TV
 
Mimi ninachofurahishwa zaidi na Kanisa Catholic ni huwasikii wakisema “ukicheza na thamani ya Mkristo” au ”ukicheza na thamani ya Mkatoliki” wao hujumuisha wote hata wasiokuwemo alimradi ni binadamu aliyeumbwa na Mungu.

Na ndiyo maana wanapata support kutoka kwa wenye akili,
Nb:hii paragraph ya pili kama akili huna huwezi ukanielewa
 
Kikubwa ni Binadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu, haijalishi ni dini gani
 
Samia the Butcher anasambuliwa kama mpira wa Kona,huku ICC akipasha, Roman Catholic wanaye,index for censorship wamependekeza awe dictator wa mwaka 2025.

Huyu akafie kibudu tu
 
Mimi ninachofurahishwa zaidi na Kanisa Catholic ni huwasikii wakisema “ukicheza na thamani ya Mkristo” au ”ukicheza na thamani ya Mkatoliki” wao hujumuisha wote hata wasiokuwemo alimradi ni binadamu aliyeumbwa na Mungu.

Na ndiyo maana wanapata support kutoka kwa wenye akili,
Nb:hii paragraph ya pili kama akili huna huwezi ukanielewa
Vipi sasa na masheikh wa bakwata wanapojibu hoja za hawa Maaskofu! Mbona hujikita zaidi kwenye kuwasimanga tu kwa kigezo cha ukatoliki au ukristo wao?
 
Wakati kanisa linachukua majukumu ya kupinga mungu unakuta kalala?
Mungu anasema na nafsi za hao wanao pata ujasiri wa kupinga huku walijua wanaikabili hatari ya kifo.
Bila kusikiliza sauti ya Mungu mioyoni mwao wangeogopa na kusifia au kutetea uovu kama wenzao.
 
Wanatumia kanisa kufanya harakati wamesahau kuwa jukumu lao ni kuomba kwa Mungu nguvu ya kiroho ambazo zitaimarisha ustawi wa maisha ya binadamu.
Wapunguze kupanic
Alafu hao binadamu waliostawi kwa kuombewa baadaye Samia na genge lake wanawateka na kuwaua.
 
Wanatumia kanisa kufanya harakati wamesahau kuwa jukumu lao ni kuomba kwa Mungu nguvu ya kiroho ambazo zitaimarisha ustawi wa maisha ya binadamu.
Wapunguze kupanic
Naanza kumuelewa Yuda sasa kwanini aliitwa Yuda...
 
Back
Top Bottom