Askofu Emmaus Mwamakula: Balozi Polepole yupo gereza la Ukonga

Askofu Emmaus Mwamakula: Balozi Polepole yupo gereza la Ukonga

Nashangaa kina Kassanga Tumbo waliwekwa kizuizini na Aboud Jumbe alilazimishwa kujiuzulu kama nchimbi lakini hao hao bado wanamuita nyerere ni baba wa taifa

Nyerere alipuyanga pakubwa tu, kitendo cha kuukubali muungano huu, tosha Elimu yake ya Makerere mi buree tu.
 
NDUGU WA POLEPOLE ATETA NA ASKOFU!

Ndugu Watanzania!
Usiku huu nimepokea ujumbe kutoka kwa mtu ambaye ni mmoja wa ndugu wa Mhe. Balozi Humphrey Polepole. Nimebadilisha initials au utambulisho wake kwa sababu za kiusalama. Suala la Polepole lina simanzi isiyoisha, hivyo hatuwezi kupuuzia minong'ono yoyote kuhusu wapi alipo.

Kwa kuwa hakuna mamlaka iliyowahi kusema kuwa inamshikilia, umma umebaki kukisia na kuokoteza taarifa ikiyumkini inaweza kutokea taarifa iliyobeba ukweli. Kwa sababu hiyo hiyo ni vigumu kwa askofu kwenda kumuulizia au kumtafuta Polepole katika mamlaka yoyote ile.

Hata hivyo, nauweka ujumbe huo hapa kwa ajili kuleta hamasa ya maombi ili kumuombea hata kumpazia sauti zaidi yumkini wanaomshikilia wanaweza kuzidiwa au kuogopa kelele nyingi.

Tukikata tamaa na kuacha kupiga kelele juu ya Balozi Humphrey Polepole hata wengine kama Dioniz Kipanya, Deusdedith Soka, Kaswahili, Chaula, Mbise, Mlay, nk tutarajie watu wengi zaidi kuendelea kutekwa na kupotezwa katika siku za kwenye kipanda uso.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 5 Agosti 2026; Saa 7:35 usiku

UJUMBE KUTOKA NDUGU WA POLEPOLE!

Nakusalimu Baba Askofu Mwamakula!
Nisamehe nakuandikia usiku. Nimeona taarifa mtandaoni, ina viashiria kuna ukweli katika hili. Ikupendeze na iwe ni vyema kwako ninaomba uende Ukonga ili kusudi ukamuone Mhe. Balozi Humphrey Polepole, kwa maelekezo ya ujumbe wa mitandaoni kuwa Polepole yupo Ukonga!

Ni mimi K. L. P.,
Ndugu yake na Humphrey Polepole.
5 Septemba 2026
Nchi hii imekuwa ya kipumbavu kwelikweli.

Wote tumefanywa tunekane kuwa wapumbavu
 
Nyerere alipuyanga pakubwa tu, kitendo cha kuukubali muungano huu, tosha Elimu yake ya Makerere mi buree tu.
Sasa wewe ni elimu ya wapi hii unayotumia hapa huoni kuwa unakuwa kama chizi?

Huo Muungano alisema atakuwepo daima kuuendesha yeye?

Wewe mwenye elimu ya sijui wapi, kwa nini unashindwa kuuondoa.
Unayo elimu utashindwa kujuwa njia za kuuondoa?
 
Ndugu zake polepole watakuwa hawana akili timamu. Wanapenda kiki za kijinga kupitia polepole
 
Ataenda kuishi kwao Zanzibar kama nchi huru inayotambulika kimataifa baada ya muungano kuvunjwa na hakuna kitu mtamfanya
Muungano hautaendelea baada ya mgalatia iwe CCM au Upinzani kushika Tanganyika 2030.
Mark my word.
Kwa nini muungano hautaendelea?
 
simuamini polepole mbona kipind cha jiwe hakubadilika au hakuridhk na ulaji wa kyuba? Naamin angepew ulaji mkubwa asingebadilik ni mtu mwwnye asili ya tamaa na kutoridhik. Anyway waacha waoane waache waoanee by chege
Hata aibu unaona mwenyewe na ulichokiandika.
 
Ila uwingi was damu kuvuja kule hawezi kuwa mzima abadani, maana km ni hospital walimpeleka wapi kuokoa uhai wake? Isingejulikana kweli?? Mmmh

Polepole alikua ameshajitoa mzima mzima kumwaga mikakati na siri zote za wahuni, na kadiri muda ulivyokuwa unazidi kwenda alionekana tishio .

Rostam sio mtu wa kufanya interview au press ila uliona kwa mawe aliyotupa alitoka mafichoni hadi kuja kufanya press mara eti hadi akahojiwa mwalimu wake wa shule ya msingi Igunga.

So mission iliyokuwepo juu ya Polepole wakimshapata ni "elimination" na wala sio kitu kingine maana alishaamua kutorudi nyuma na kuamua kumwaga siri na mikakati ya wahuni hivyo wasingeweza kumbakisha akiwa hai.

Familia itambue siku hiyo ndio siku yake ya mwisho kuishi, watafute namna hata kama ni kisasi baada ya kuwajua watekelezaji ila sio kudanganywa ndugu yao kahifadhiwa gerezani.
 
Aisee 😑 😑
 
..basi wautoe hata mwili wake.
Ndiugu na Wananchi ndio Wanatakiwa kufanya hivyo,hizi message za sijui yuko Ukongo Mara kwenye nyumba gani lengo lake no kuneutralise Upinzani na ndugu kwa kuhakikisha wako disillusioned kugoma au kufanya chochote kile kushinikiza uwajibikaji,wako tricky,Wanahakikisha wanapenyeza habari kwa watu wanaoaminiki ambao wanafahamu hao watu hawafahamu mchezo unaochezwa,wanarusha taarifa ambazo hawatakiwi kuzirusha..Tupunguze breaking news ambazo chanzo cha hizo news hakijathibitishwa wakati tuko kwenye crisis kama tunataka watu washinikize jambo.Mdude ilikuwa hivyo hivyo,walisema yuko kwenye Jumba gani sijui,watu wakapata matumaini na kutulia..
 
Ila uwingi was damu kuvuja kule hawezi kuwa mzima abadani, maana km ni hospital walimpeleka wapi kuokoa uhai wake? Isingejulikana kweli?? Mmmh
Damu kuvuja vile sio sababu pekee mkuu. Inaweza ikawa ni mshipa wa damu wa mkononi ulikata, so anaweza akapata msaada na akapona vizuri tu.
 
Back
Top Bottom