Askofu Dr. Valentino Mokiwa Aonya dhidi ya Uchakachuaji Matokeo!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu Dr. Valentino Mokiwa Aonya dhidi ya Uchakachuaji Matokeo!.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Oct 29, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Zikiwa zimebakia siku mbili kabla ya uchaguzi mkuu, Mkuu wa kanisa la Anglicana la Tanzania, Askofu Dr. Valentino Mokiwa, ameonya dhidi ya uchakachaji matokeo ya uchaguzi kwa aina yoyote, huko ni kuhatarisha amani, umoja na mshikamano wa Watanzania.

  Askofu Dr. Mokiwa, ametoa onyo hilo leo, katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi, yaliyofanyika katika Makao Makuu ya Dayosisi ya Kanisa la Anglicana Tanzania, yaliyopo eneo la Ilala hapa jijini Dar es Salaam.

  Askofu Mokiwa amesema uchaguzi huru na wa haki ndicho kipimo cha demokrasia iliyopevuka ambapo mshindi katika uchaguzi ndio chaguo la wengi, hivyo vitendo vyovyote vya kuchakachua matokeo halali ya uchaguza, ni kitu cha hatari kinachoweza kutishia amani, umoja na mshikamano wa Watanzania.

  Pia askofu Dr. Valentino Mokiwa, ametoa angalizo muhimu kwa vyama vya siasa nchini, wagombea wao na Watanzania kwa ujumla, kuwa tayari kuyapokea na kuyakubali matokeo yoyote ya uchaguzi huu, hata kama atakayeshinda sio mgombea uliyemtegemea.

  Askofu Mokiwa, ametoa angalizo hilo kufuatia kampeni za uchaguzi wa mwaka huu, kugubikwa na hamasa ya hali ya juu Ambato ameielezea haijapata kutokea tangu harakati za kupigania uhuru, hivyo kufuatia hamasa hii, inaweza kupelekea vyama na washabiki wake kuhamanikia ushindi, hivyo matokea yakiwa kinyume cha matarajio yao, wanaweza kufanya chochote.

  Askofu Mokiwa amekiri uchaguzi wa mwaka huu, hautabiriki kirahisi kama chaguzi nyingi zilizo tangulia, hivyo ni muhimu kwa wadau wote wanaoshiriki kwenye uchaguzi huu, pamoja na kuwashabikia wagombea wanaowataka, lazima wawe tayari kupokea na kuyakubali kwa moyo, matokeo yoyote ambayo ndio chaguo la wengi.

  Amesema, baada ya kutangazwa kwa matokeo, huo ndio mwisho wa ushindani, hivyo amewaomba wagombea walioshinda na walioshindwa, kushikana mikono, kupongezana na hata kukumbatiana kama ishara ya upendo, kudumisha amani utulivu na mshikamano baina ya Watanzania, na kuwasihi walioshinda, wasiwabeze walioshindwa.

  Askofu Dr. Mokiwa, naye amejiunga na viongozi wengine wa dini nchini kwa kutangaza kuwa Kanisa la Anglican, halina mgombea linalomuunga mkono, na kuwahimiza wafuasi wake, wajitokeze kwa wingi situ ya kupiga kura, na wawapigie wagombea wowote wanaowataka bila kujali dini zao.

  Wakati huo huo, Askofu Mokiwa ametangaza kufanyika kwa misaa maalum ya kuombea uchaguzi wa amani nchini Tanzania, itakayofanyika kesho saa 4:00 asubuhi katika kanisa la St. Albano, lililope eneo la Posta Mpya, watu wote wamekaribishwa. End.

   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  ok !
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  well said..
   
 4. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Wa-tz sio wapumbavu kujua kama jambo fulani limeenda sawa au si sawa. Kauli ya Askofu kuhusu kuchakachua ni sahihi. Haki ni lazima ionekane inatendeka. Watu wakiona haki imetendeka hawawezi kutaa matokeo. Angalizo ni kuwa kukiwa na mashaka kuwa haki haijatendeka lazima matokea yatapingwa tu!!
   
 5. W

  We can JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nimekupta ndg yangu Mo-TOWN. But PRAY to God before you PLAY YOUR PART!

  Ama kweli TZ ya trh1/Nov.2010 inaweza kuwa siyo hii niionayo? Mungu Ibariki Tanzania, Bariki na Afrika yetu.
   
Loading...