Askofu Bagonza; Mahusiano ya Viongozi na Wananchi Wakati wa Dhiki.

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,798
71,218
Askofu Bagonza ashauri viongozi na wananchi wanavyo paswa kuishi wakati mgumu kama huu, jee hawa viongozi wetu wa hapa wanaweza kuelewa au watadharau?

SOLAR PANELS ZAADIMIKA ULAYA

Majira ya baridi kali yamekaribia. Kuna wasiwasi na hofu miongoni mwa watu hapa Ulaya:

1. Gharama za gesi na mafuta ziko juu. Pamoja na serikali zao kuwapa fedha za kukabiliana na makali hayo, bado gharama za kuwasha, kupika, kuchemsha nyumba na kuendesha mashine ndogo za nyumbani ziko juu.

2. Watu wengi wanaweka solar panels kwenye nyumba zao lakini sasa zimeisha madukani na meli nyingi hazipakii kule China.

3. Hofu ya kukata miti mingi ili kuchemsha nyumba nayo imetanda. Mwenye akiba ya kuni anatumia kwa uangalifu sana.

4. Ipo hofu kuwa watu maskini wa kipato watapata shida na kufa ndani ya nyumba zao kwa baridi.

Huu ni mgogoro mkubwa wa nishati uliosababishwa na vita ya Urusi na Ukraine lakini pia vikwazo kwa Urusi ambaye ni mzalishaji mkubwa wa gesi.

Serikali nyingi zinajitahidi kuwapoza raia wake wasilipuke wakati huo huo jitihada za kidiplomasia zikifanyika kumaliza vita.

Tunajifunza nini?

- Wakati wa shida, serikali ikae karibu zaidi na wananchi. Si lazima kuwapa kitu bali kuwa karibu nao. Mbwembwe za ukuu na vimbwanga vya madaraka havifai wakati wa shida.

- Akili nyingi zinatokana na shida kuliko raha na amani. Yawezekana Ujinga wetu unatokana na neema ya hali ya hewa nzuri. Unahitaji akili kuvaa ili kujikinga na baridi lakini huhitaji akili kuvua nguo unaposikia joto.

*********mwisho wa nukuu.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom