Askofu Bagonza: Leadership is not about size, It's about knowledge and Wisdom

Torch

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
1,200
1,116
FB_IMG_1628595286966.jpg

KWA UCHACHE TU

1. Matatizo ya kisiasa hayatatuliwi kisheria.

2. Matatizo ya kisheria hayatatuliwi Kisiasa.

3. Suala la Katiba Mpya lina sheria na siasa. Mazungumzo yasiyo na hila ndani yake hayakwepeki.

4. Walipokuwa tayari hakuwa tayari. Atakapokuwa tayari hawatakuwa tayari. Mtu wa tatu hakwepeki.

5. Uhuru wa habari si kutofungia magazeti. Ni kufungua yaliyofungwa. Zaidi sana ni kuacha kuwa mhariri asiye rasmi kupitia Polisi.

6. Demokrasia ni zaidi ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu. Hivi hata msibani vipo. Demokrasia ni Viongozi kuwa watumishi wa wananchi na wananchi wakawa waajiri wa viongozi. Viongozi wawaogope wananchi na Wananchi wasiogope chochote. Wananchi wawabambikie kesi viongozi na siyo kinyume chake.

7. Uchumi jumuishi huendana na siasa jumuishi. Uchumi bila siasa ni sawa na kunenepesha ng'ombe siku ya mnada. Zawadi nzuri ya mfungwa si pilau na sabuni. Ni tangazo la "uko huru".

8. Madai ya Katiba Mpya si ya Chadema. Rais wetu siyo Chadema. Aliongoza bunge la katiba mpya. Mzee wa Warioba hata rangi ya kadi ya Chadema sidhani kama anaijua. Mimi nina mawazo ya ki-CCM lakini naidai katiba mpya.

9.Kuwaachia waliobambikiwa kesi Kisha ukamteua aliyewabambikia kesi ni kumbambikia cheo kitakachokuwa mzigo kwake.

10. Kuwaachia wabambikiwa kesi kisha ukawabambikia wengine ni sawa na kusimamisha saa ili kukomboa muda. Hiyo wanafanyaga Wajaluo ili kusaidia betri ya saa isiishe haraka!

Kama tunakerwa na kuchefuliwa na wanaodai katiba mpya, watakapokuja wanaodai Ben Saa Nane tujiandae kutapika.

Naomba kuuliza: Hivi mpinzani akiteuliwa anaruhusiwa kuendelea kuwa mpinzani? Siku nyingine nitauliza wanaoenda gerezani wanaruhusiwa kuunga mkono juhudi wakiwa huko?
 
hii nummber 10 imenichekesaha sana aisee 🀣 🀣 🀣

10. Kuwaachia wabambikiwa kesi kisha ukawabambikia wengine ni sawa na kusimamisha saa ili kukomboa muda. Hiyo wanafanyaga Wajaluo ili kusaidia betri ya saa isiishe haraka!
Nouma snaa
 
Zawadi nzuri ya mfungwa si pilau na sabuni ni tangazo "uko huru"

Hiyo kauli inamaanisha mwananchi asidanganyike kwa kupewa kidogo huku akinyimwa kikubwa.

Mfano wa hiyo kauli ni kuwaruhusu wawekezaji warudi nchini huku ukiwafunga midomo wananchi wako wasitoe mawazo yao kusema wanachotaka (Katiba Mpya).
 
Bagonza anakichwa Hatari sana
 
Good
 
Well said
View attachment 1887170
KWA UCHACHE TU

1. Matatizo ya kisiasa hayatatuliwi kisheria.

2. Matatizo ya kisheria hayatatuliwi Kisiasa.

3. Suala la Katiba Mpya lina sheria na siasa. Mazungumzo yasiyo na hila ndani yake hayakwepeki.

4. Walipokuwa tayari hakuwa tayari. Atakapokuwa tayari hawatakuwa tayari. Mtu wa tatu hakwepeki.

5. Uhuru wa habari si kutofungia magazeti. Ni kufungua yaliyofungwa. Zaidi sana ni kuacha kuwa mhariri asiye rasmi kupitia Polisi.

6. Demokrasia ni zaidi ya vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu. Hivi hata msibani vipo. Demokrasia ni Viongozi kuwa watumishi wa wananchi na wananchi wakawa waajiri wa viongozi. Viongozi wawaogope wananchi na Wananchi wasiogope chochote. Wananchi wawabambikie kesi viongozi na siyo kinyume chake.

7. Uchumi jumuishi huendana na siasa jumuishi. Uchumi bila siasa ni sawa na kunenepesha ng'ombe siku ya mnada. Zawadi nzuri ya mfungwa si pilau na sabuni. Ni tangazo la "uko huru".

8. Madai ya Katiba Mpya si ya Chadema. Rais wetu siyo Chadema. Aliongoza bunge la katiba mpya. Mzee wa Warioba hata rangi ya kadi ya Chadema sidhani kama anaijua. Mimi nina mawazo ya ki-CCM lakini naidai katiba mpya.

9.Kuwaachia waliobambikiwa kesi Kisha ukamteua aliyewabambikia kesi ni kumbambikia cheo kitakachokuwa mzigo kwake.

10. Kuwaachia wabambikiwa kesi kisha ukawabambikia wengine ni sawa na kusimamisha saa ili kukomboa muda. Hiyo wanafanyaga Wajaluo ili kusaidia betri ya saa isiishe haraka!

Kama tunakerwa na kuchefuliwa na wanaodai katiba mpya, watakapokuja wanaodai Ben Saa Nane tujiandae kutapika.

Naomba kuuliza: Hivi mpinzani akiteuliwa anaruhusiwa kuendelea kuwa mpinzani? Siku nyingine nitauliza wanaoenda gerezani wanaruhusiwa kuunga mkono juhudi wakiwa huko?
 
Ngoja kwa muda huu niishie ku-πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Back
Top Bottom