Askofu Bagonza: Kuna kitu hakiko sawa

Askofu Bagonza: Kuna kitu hakiko sawa

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283
CORONA BADO IPO DUNIANI

Kufuatia taharuki inayotokana na vifo kadhaa mwishoni na mwanzoni mwa mwaka hapa Karagwe, watu wengi wamekuwa wanapiga simu kwangu na kwa uongozi wa hospitali teule ya Nyakahanga kuulizia kulikoni? Jibu hili litoshe kusaidia kujibu maswali hayo:

1. Corona BADO iko duniani. Tanzania ni sehemu ya dunia. Malizia sehemu inayobaki. Maswali yaliyobaki waulizeni wenye dhamana na masuala ya Afya ngazi ya Mkoa na Wilaya.

2. Tanzania si makao makuu ya Mungu. Yeye ni wa wakati wote na wa mahali pote. Mahali alipo, Corona yaweza kuwapo pia. Wenye dhambi na watakatifu wote wanaugua na kufa. Makutano yetu ni ufufuko.

3. Uhai tulio nao si mali ya serikali wala ya dini yoyote. Tuna wajibu wa kuulinda. Tuchukue tahadhari zote bila kusubiri maagizo ya serikali au ya dini. Nawa mikono, tumia barakoa, jiepushe na mikusanyiko, nyungu haizuiwi na tiba mbadala nyingine hazizuiwi. Ramli ni marufuku hospitalini.

4. Kama si lazima usiende hospitalini kutembea. Kama si lazima tibiwa nyumbani kwako. Kama si lazima usizushe kuwa una ugonjwa ambao haujathibitishwa kwa vipimo.

5. Tunapakana na nchi zilizojitangaza kuwa zina maambukizi makubwa ya Corona. Majirani wema huzaa watoto wanaofanana kwa sababu ya kuhusiana vizuri. Hii ni vita, ujirani uchukue viwango vipya.

6. Idadi ya wagonjwa wenye matatizo ya kupumua imeongezeka ndani ya muda mfupi. Yawezekana ni uchovu wa mwisho wa mwaka! Idadi ya mitungi ya Oksijeni tuliyo nayo ni ndogo. Wasamaria wema wanakaribishwa kusaidia mitungi zaidi. Siasa safi ni kujitolea mitungi zaidi ili wenye shida ya kupumua wasaidiwe. Karibuni.

Kwa nia njema na kwa mapenzi makubwa kwa watu nilioagizwa kuwachunga na kuwalisha.
 
Corona ipo ila tumshukuru Mungu wengi tumeweza kuishi nayo kwa miili kujenga kinga. Baadhi wanasayansi wanapendekeza kutovaa musk ili kubadilishana virus na bacteria kujenga kinga imara zaidi.
 
Serikali ikisema wapinzani wataanza kupinga

Hapana Mkuu wapinzani wanasema kwamba korona ipo ila serikali inaficha na kila siku wanawapa tahadhari wananchi wachukue!! kwahiyo serikali ikitoa tamko waoinzani wataunga mkono.
 
Hili nalo neno, 'Tanzania si makao makuu ya Mungu'
Tatizo Bagonza mpagani hajui hata Mungu anaishi wapo makao makuu ya Mungu yako ndani ya za wamchao anasema niko mlangoni nabisha mtu akinikaribisha nitafanya makao kwake

Mungu wetu anaitwa Emmanuel yaani Mungu pamoja nasi

Kwa alichoandika kakufuru tunamwachia Mungu atajua cha kufanua

Heri angebaki kuongelea siasa lakini huko kwa Mungu aliyetudhindia Corona kachokonoa mzinga wa nyuki na aweza ondoka kwa hiyo Corona anayopenda kuiabudu na kuitumiakumdhalilisha Mungu Mark my words

Kazi aliyofanya Mungu Tanzania kwenye issue ya Corona ni kubwa Mno na haitakiwi kkudhihakiwa atakiona cha mtena joho lake pete na kofia na fimbo yake ya kiaskofu ni takataka tu Mbele za Mungu aliyemdhihaki baada ya kufanya kazi kubwa ya kupigania Tanzania dhidi ya Corona
 
Usikute kayaongea haya kwenye ibada ya watu zaidi ya 200 na wote hawajavaa mask na bado wamesongamana kwenye kutoa sadaka alaf bado anashindwa kumtukuza Munga kwa hilo yeye analeta janja janja za siasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom