BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,013
HATARI!!!
KUBAMBIKIWA KITI na MICROPHONE ni Hatari kuliko Corona, Barakoa na Chanjo!
Rais Jakaya Kikwete aliwahi kulijulisha Taifa kuwa kutokana uhasama ndani ya medani za Kisiasa, ilifika wakati "watu walikuwa hawaachiani glasi walipotoka kwenda maliwatoni". Siasa za makundi na uhasama vilitawala na kuondoa kutoaminiana.
Wakati fulani hayati Samuel Sitta akiwa Spika, zilitolewa tuhuma za Mbunge fulani kuonekana akimimina vitu kama unga kwenye baadhi ya viti vya wabunge. Tendo hilo lilizua tafrani bungeni.
Wiki hii Taifa limeshuhudia Mbunge wa CCM ambaye ni Askofu wa Kanisa, akiwa mbele ya Kamati ya Bunge la Wana CCM, akikataa kutumia kiti na microphones vilivyoandaliwa ili aweze kuvitumia wakati anahojiwa na Kamati.
Kitendo hicho si cha kupuuza kwa sababu zifuatazo:
1. Tuhuma za muda mrefu kuhusu kuwekeana sumu, kuuana na kukolimbana, Sasa zinapata msukumo mpya.
2. Aliyeshtuka ni Askofu anayeaminika na watu wengi. Kwa hiyo mashaka yake yanapewa uzito.
3. Ziko tuhuma za watu KUBAMBIKIWA Kesi mbaya kwa sababu za Kisiasa. Kama aliye ndani ya mfumo wa utawala anashtuka, je aliye nje afanye nini?
4. Askofu huyu amekuwa na mashaka juu ya uwepo wa Corona, baadaye akawa na mashaka juu ya chanjo. Sasa anashtukia kiti na microphone. Nini kinafuata?
5. Ikiwa viti na microphones vinaweza kutumiwa kudhuru mtu asiyekubaliana na mfumo wa utawala, je usalama wa wanaosimamia mfumo huo ukoje?
6. Ikiwa jengo la bunge ambalo ni madhabahu ya Taifa letu inahofiwa, je maeneo mengine ya utawala yakoje?
7. Madai ya Askofu kuwa Rais hana tatizo lakini washauri na wasaidizi wake ndio wabaya, yana taswira gani kwa usalama wa Rais? Kumbuka haya yamesemwa na Mbunge na mwana CCM.
8. Mungu anayeweza kumlinda mtu dhidi ya Corona anashindwaje kumlinda mtu na madhara ya kiti na microphone?
Taifa letu linaumwa. Corona ni cha mtoto. Tutafute suluhu nje ya SULUHU. Naendelea kusisitiza, "Kifo cha mbwa huanza kwa kupoteza uwezo wa kunusa hatari".
Askofu Bagonza