Kuwaza kutumia nguvu na hila kwenye Uchaguzi wakati hukubaliki ni hatari kwa Usalama wa nchi

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
715
1,774
Nimemsikiliza Rais wakati akiwaapisha mawaziri ukweli ni kwamba kuwaza kuwa na uchaguzi kama wa 2020 kwa Rais huyu mwenye ushawishi kidogo au wa wastani ni kutaka kuleta fujo nchini.

Wakati wachache wanadai uchaguzi wa 2019/2020 uliibiwa wengi wa wananchi wanaamini Magufuli alishinda kihaki ndio maana hata upinzani ulififia sana.

Kazi za hayati Magufuli kwa Taifa hili zilimbeba sana na akaaaminiwa sana na wema na kuogopwa sana na waovu. Naiona hatari ya utawala huu wa urithi kuwaza kuwa unaweza kucheza na uchaguzi.

Utawala huu hauaminiki wala hauogopwi na yoyote kwasababu kuna hila hila nyingi.

UCHAGUZI WA HAKI, HURU NA WA UWAZI NDIO UTATULIZA HII NCHI
 
Wakati wachache wanadai uchaguzi wa 2019/2020 uliibiwa wengi wa wananchi wanaamini Magufuli alishinda kihaki ndio maana hata upinzani ulififia sana.
Mkuu acha kujiaibisha. Uchaguzi chini ya magufuli haukuwa tofauti na ule wa Juzi wa Nchini Gaboni. Tofauti tu ni mapinduzi.
 
Back
Top Bottom