Kutoka mwanakijiji.com
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Mwanza Mhashamu Antony Mayalla amefariki duniani. Hadi tunaingia mitamboni hatujajua bado chanzo cha kifo chake. Askofu Mayalla alizaliwa tarehe 23 Aprili, 1940 huko Mwabagole, Kwimba mkoani Mwanza. Baada ya masomo ya msingi na Sekondari na baadaye Useminari alipewa daraja takatifu la Upadrisho tarehe 20 Disemba mwaka 1970.
Aliteuliwa kuwa Askofu wa Musoma mwaka 1979 (miaka tisa tu baada ya upadrisho) na kuwa miongoni mwa maaskofu vijana wa Kanisa Katoliki akiwa na miaka 39 tu. Alisimikwa kuwa Askofu wa Jimbo la Musoma tarehe 22 Aprili, 1979 na Muadhama Kardinali Laurean Rugambwa akishirikiana na Maaskofu James Rubin M.Mafr. na Askofu Renatus Butibubage aliyekuwa Askofu wa Mwanza wa wakati huo. Kufuatia kujiuzulu kwa Askofu Butibubage mwaka 1987, Baba Mtakatifu Yohanne Paulo wa Pili alimteua Askofu Mayalla wa Musoma kuliongoza Jimbo Kuu la Mwanza kama Askofu wake Mkuu Novemba mwaka huo. Alisimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Mwanza 28 Februari, 1988 na hivyo kuanza utawala wa Utume wake wa kiaskofu.
Baada ya kusimikwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Askofu Mayalla alisimamia kwa kiasi kikubwa uhamishaji wa Makao Makuu ya Askofu kutoka Bugando kwenda kilima kingine cha Kawekamo maili chache toka Uwanja wa ndege wa Mwanza.
askofu Mayalla ameweza kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kichungaji jimboni mwake huku akiongoza kwa kupata waseminari na mapadre wapya, kufungua seminari ya kwanza ya Wasichana Jimboni na vile vile kuendelea kufungua vituo vya afya, shule za sekondari na programu mbalimbali za Afya. Jimbo la Mwanza chini ya Askofu Mayalla limendelea kutoa mojawapo ya mafunzo ambayo kwa muda mrefu yalikuwa yanatolewa Mwanza tu nayo ni yale ya Clinical Pastoral Education ambayo yalikuwa yanahusisha watu wa dini mbalimbali kujifunza jinsi ya kuhudumia wagonjwa.
Wengi watamkumbuka katika maadhimisho ya Misa ya Papa Yohanne Paulo wa 2 kwenye viwanja vya Kawekamo Mwanza na pia katika misa ya kumuaga marehemu Baba wa Taifa huko Butiama ambayo yeye aliiongoza.
Mipango ya mazishi itajulikana baadaye.
Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi, Amina
Asante Lunyungu kwa post hii. Masanilo alishatoka na breaking news yake dakika 42 kabla ya post yako. Nashauri umuombe mod aiunganishe ili tuendelee na eulogy moja for this great man
RIP Bishop Mayalla.
Unafiki gani aliokufanyia? Weka wazi watu tujue.
RIP askofu Mayalla, utakumbukwa daima hapa chuoni bugando.
Naomba mumusamehe bure shem wangu Yo Yo hajui alitendalo!
Archbishop Anthony Mayala of the Archdiocese of Mwanza, Tanzania is dead.
According to the Very Rev. Fr. Pius Rutechura, the Secretary General for the Association of member Episcopal Conferences of Eastern Africa (AMECEA), Archbishop Mayala passed away on August 19, 2009 as he was undergoing treatment at Bugando Hospital, Mwanza where he had been rushed in the morning after experiencing some health complications.
Actually, these news are coming too fast, for as early as yesterday, the archbishop spent the day in his office and was healthy, said Fr. Rutechura.
The Secretary General could not immediately confirm the cause of the death, though he said the late bishop was suffering from hypertension.
The late former board member of the Catholic University of Eastern Africa was born in 1940, ordained Bishop of Musoma diocese, Tanzania in 1979, and later ordained the Archbishop of Mwanza in 1987, an archdiocese he was shepherding till his demise.
Fr. Rutechura, who, as the Secretary General of the Tanzania Episcopal Conference, worked with the deceased for six years described the late archbishop as fatherly, caring, and strong believer of unity and togetherness.
The burial plans are yet to be made.
Masanha jambo hili mni zito lakini Mayala alikuja kunipa kipaimara ( Confirmation) na akasema atapenda kuniona niko Seminary , baada ya Ibada aliniombea baraka na kunishika kimwani na kweli nikatinga Seminary .Huyu mzee alikuwa mwelewa alipenda wasomi.Jimbo la Mwanza nina imani lina ongoza sana kwa kuwa na mapadre wasomi maana alifika kote Duniani kuulizia kama anaweza kusomesha mapadre huko.Kazi za injili ujenzi wa zahanati , mashule na misaada hakika the man worked hard .Again apumzike kwa amani .