Askari wetu wa barabarani waone aibu!

feyzal

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
6,803
12,667
Habari ya asubuhi waungwana.

Ukweli hii tabia ya hawa askari wa barabarani kuchukua rushwa imekithiri sana tena wanachukua wazi wazi na bila kuogopa.Leo asubuhi nimepanda daladala kutoka Rang 3 naelekea vingunguti nikawa nimekaa siti ya mbele kabisa,tumetoka kituo kikuu cha Rang 3 tunafika Kizuiani trafki akasimamisha dereva akafyonya "aah hawa jamaa washaanza asubuhi asubuhi kutaka hela akamwita konda wake jina oya Bonge mpelekee elfu mbili yake tuondoke" na kweli konda akafanya hivyo.

Gari ikaondoka tumefika Sokota ikasimamishwa tena na askari wa kike aliyekuepo pale kiwanda cha maji ya afya.Dereva "oya bonge shuka mwambie tushaunga uko nyuma" konda akaenda lakini akakawia ikabidi dereva nae ashuke akaenda akarudi na hasira "huyu dada njaa sana,sasa kila tukisimamishwa tutakua tunatoa hela" kuna mzee jirani yangu akamuuliza kwani gari inakosa gani? Dereva akajibu "unafikiri mzee gari inakosa yaani hawa trafki gari hata iwe mpya imetoka leo lazima uwape hela ukiwanyima njia utaihama watakavyokuandama kwahiyo imekua kama desturi,ngoja huku tunapoenda utakuta wengine watasimamisha na dau lao ni hilo hilo 2000-3000 kwa asubuhi".

Tulipofika buguruni sheli tukasimamishwa tena na matrafiki wa tatu wawili wanaume na mmoja wa kike kondakta akashuka tena kupeleka elfu 2,kitu cha ajabu wakisimamisha wala hawakagui gari wanazuga wanachukua chao kisha wanaondoka.

Jeshi la polisi usalama barabarani limeoza linahitaji kufumuliwa hii tabia imekithiri sana na sio mara moja kushuhudia,madereva na makonda wa daladala wengi hawana mshahara wanaamka mida mibaya kutafuta pesa lakini trafki badala kufanya kazi kwa ueledi wao wananyanyasa bila huruma wao wana mishahara na viposho lakini tamaa mbele.Na ninyi madereva na makondkta pia acheni unyonge na tabia hii ya kutoa hela hovyo hovyo hata kama huna kosa ni mnafuga ugonjwa,ukiwa na kosa kheri uandikiwe uichangie serikali kuliko kuwapa hao wafuga vigambi.
 
Wabongo mna mabichwa magumu balaaa.

Magufuli alishawaruhusu hao traffic kuchukua rushwa.

Alisema pesa wanayochukua ni ndogo tu ya kubrush viatu.

Sasa unakuta takataka kama ninyi mnaoimba kila siku Magufuli baba lao kakomesha rushwa eti mnalalamika huku mkijifanya kuwalaumu traffic wakati chanzo mnajifanya hamkioni.
 
Kuwa mstaarabu hakuna mahala nimetukana wala kumwita mtu takataka..

Mara moja moja jaribu kuficha upumbavu wako.
Wabongo mna mabichwa magumu balaaa.

Magufuli alishawaruhusu hao traffic kuchukua rushwa.

Alisema pesa wanayochukua ni ndogo tu ya kubrush viatu.

Sasa unakuta takataka kama ninyi mnaoimba kila siku Magufuli baba lao kakomesha rushwa eti mnalalamika huku mkijifanya kuwalaumu traffic wakati chanzo mnajifanya hamkioni.
 
Kuhusu aliwaajiri mi naona kosa lao wenyewe hao askari maana anawanyanyasa na bado wanamtetea na kumlinda kwa nguvu zote.

28/10/2020 ni Yeye tuondoe huu upuuzi.
Aliewaajiri je anawalisha posho za kutosha juani na kuwapa stahiki zao vizuri au wao ndo wamejiongeza kwa kukiuka viapo na miiko ya kazi ili jua lisiwababue bure?
 
Hii serikali iondoke maana inafanya upumbavu sana tena awamu hii ndo balaa tupu askari wana jeuri sana.
Halafu takukuru jioni wanarudi nyumbani eti hakuna aliyepokea rushwa. Wao kila kukicha wanaamkia mahakamani utadhani ni wafanyakazi wa mahakama
 
Inawezekana mkuu.

Ukatili sio tu kupiga hata kuchukua pesa isiyo halali yako kwa kutumia mamlaka uliyonayo ni ukatili pia.
Wakati mwingine nafikiri kama kuna somo la ukatili kwa raia kwenye mafunzo yao.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Wabongo mna mabichwa magumu balaaa.

Magufuli alishawaruhusu hao traffic kuchukua rushwa.

Alisema pesa wanayochukua ni ndogo tu ya kubrush viatu.

Sasa unakuta takataka kama ninyi mnaoimba kila siku Magufuli baba lao kakomesha rushwa eti mnalalamika huku mkijifanya kuwalaumu traffic wakati chanzo mnajifanya hamkioni.

Thread Closed.
 
Mishahara midogo hamna nyongeza mazingira ya kazi magumu wataachaje kuomba rushwa walimu ndo wanatia huruma.

Mimi nimeshawazoea tunaowatembea na pikapu tunaelewa.

Pickup
Canter
Fuso
Kirikuu
Coaster
Hiace
 
Wabongo mna mabichwa magumu balaaa.

Magufuli alishawaruhusu hao traffic kuchukua rushwa.

Alisema pesa wanayochukua ni ndogo tu ya kubrush viatu.

Sasa unakuta takataka kama ninyi mnaoimba kila siku Magufuli baba lao kakomesha rushwa eti mnalalamika huku mkijifanya kuwalaumu traffic wakati chanzo mnajifanya hamkioni.
Amesahau huyo,acha niitafute ile clip
 
Back
Top Bottom