Askari wetu wa barabarani waone aibu!

Uzi nimeleta kwa sababu mara kadhaa nimewahi sikia hao madereva na makonda unakuta ikifika jioni wakitoa pesa ya mafuta na hesabu unaweza kuta inabaki mfano elfu 30 na wako wa tatu.Sasa fikiria umeamka saa 10 alfajiri inafika saa nne usiku una elfu 30 mgawane watu watatu na unafamilia hayo maisha unadhani yatakua ya namna gani? Waoneeni huruma wazee
unajua mkuu, siku zote mtu anaefata sheria barabarani na hana dosari hua hata trafiki wanamuogopa!?.. daladala wengi gari zao zina makosa kwahyo wanakua kwenye disadvantage sana hata haya magari makubwa mkuu baadhi ambayo hayafanyiwi servicw mara kwa mara hua wanapigwa sana ila yale yaliyokua na service na hayana makosa hata madereva wanakuaga wakorofi kwa trafiki..

so all in all, wao makosa yao madereva wanashindwa kutatatua kwakua wanajua nikimpa 2000 trafiki atatuachia tu,.
 
Halafu takukuru jioni wanarudi nyumbani eti hakuna aliyepokea rushwa. Wao kila kukicha wanaamkia mahakamani utadhani ni wafanyakazi wa mahakama
braza nikuibie siri tu, hakuna sehemu inayoongoza kwa kula rushwa kubwakubwa kama takukuru. . wanakula rushwa ili kuwaficha wala rushwa.

sijui tunaelewana hapa?.
 
bora kutoa 2000 kuliko 30000, polisi wa Tanzania ni waungwana sana kwenye mambo yasiyohusu ccm.
 
Habari ya asubuhi waungwana.

Ukweli hii tabia ya hawa askari wa barabarani kuchukua rushwa imekithiri sana tena wanachukua wazi wazi na bila kuogopa.Leo asubuhi nimepanda daladala kutoka Rang 3 naelekea vingunguti nikawa nimekaa siti ya mbele kabisa,tumetoka kituo kikuu cha Rang 3 tunafika Kizuiani trafki akasimamisha dereva akafyonya "aah hawa jamaa washaanza asubuhi asubuhi kutaka hela akamwita konda wake jina oya Bonge mpelekee elfu mbili yake tuondoke" na kweli konda akafanya hivyo.

Gari ikaondoka tumefika Sokota ikasimamishwa tena na askari wa kike aliyekuepo pale kiwanda cha maji ya afya.Dereva "oya bonge shuka mwambie tushaunga uko nyuma" konda akaenda lakini akakawia ikabidi dereva nae ashuke akaenda akarudi na hasira "huyu dada njaa sana,sasa kila tukisimamishwa tutakua tunatoa hela" kuna mzee jirani yangu akamuuliza kwani gari inakosa gani? Dereva akajibu "unafikiri mzee gari inakosa yaani hawa trafki gari hata iwe mpya imetoka leo lazima uwape hela ukiwanyima njia utaihama watakavyokuandama kwahiyo imekua kama desturi,ngoja huku tunapoenda utakuta wengine watasimamisha na dau lao ni hilo hilo 2000-3000 kwa asubuhi".

Tulipofika buguruni sheli tukasimamishwa tena na matrafiki wa tatu wawili wanaume na mmoja wa kike kondakta akashuka tena kupeleka elfu 2,kitu cha ajabu wakisimamisha wala hawakagui gari wanazuga wanachukua chao kisha wanaondoka.

Jeshi la polisi usalama barabarani limeoza linahitaji kufumuliwa hii tabia imekithiri sana na sio mara moja kushuhudia,madereva na makonda wa daladala wengi hawana mshahara wanaamka mida mibaya kutafuta pesa lakini trafki badala kufanya kazi kwa ueledi wao wananyanyasa bila huruma wao wana mishahara na viposho lakini tamaa mbele.Na ninyi madereva na makondkta pia acheni unyonge na tabia hii ya kutoa hela hovyo hovyo hata kama huna kosa ni mnafuga ugonjwa,ukiwa na kosa kheri uandikiwe uichangie serikali kuliko kuwapa hao wafuga vigambi.
Hiyo ni kubrashia viatu mbona inaeleweka au ww mgeni hapa Tanzania
 
Wabongo mna mabichwa magumu balaaa.

Magufuli alishawaruhusu hao traffic kuchukua rushwa.

Alisema pesa wanayochukua ni ndogo tu ya kubrush viatu.

Sasa unakuta takataka kama ninyi mnaoimba kila siku Magufuli baba lao kakomesha rushwa eti mnalalamika huku mkijifanya kuwalaumu traffic wakati chanzo mnajifanya hamkioni.
Tunajua tatizo lilipo lakini hatulijadili.
Tukichagua vizuri tar 28/10 na tukilinda kila aina ya hujuma tutaondokana na matatizo mengi.
Suluhisho la matatizo yetu ni sisi wenyewe, tukiamua sasa basi itakuwa hivyo.
Kenya na Nigeria ni mifano, hakuna nguvu inayoizidi nguvu ya umma.
Umma ukikataa kwa dhati hakuna anayeweza kuzuia
 
Halafu takukuru jioni wanarudi nyumbani eti hakuna aliyepokea rushwa. Wao kila kukicha wanaamkia mahakamani utadhani ni wafanyakazi wa mahakama
Wao takukuru husubilia rushwa za wanyonge tu maana wao na polisi kitu kimoja, hiyo ni tasisis ya kupamba rushwa
 
Mbona mwendo kazi hayakamatwi? Na sometimes huwa zinajazaga abiria wengi kuliko kawaida.....? Hii sio poa jamani Askari wetu muwe mnafuata maadili ya kazi
 
Habari ya asubuhi waungwana.

Ukweli hii tabia ya hawa askari wa barabarani kuchukua rushwa imekithiri sana tena wanachukua wazi wazi na bila kuogopa.Leo asubuhi nimepanda daladala kutoka Rang 3 naelekea vingunguti nikawa nimekaa siti ya mbele kabisa,tumetoka kituo kikuu cha Rang 3 tunafika Kizuiani trafki akasimamisha dereva akafyonya "aah hawa jamaa washaanza asubuhi asubuhi kutaka hela akamwita konda wake jina oya Bonge mpelekee elfu mbili yake tuondoke" na kweli konda akafanya hivyo.

Gari ikaondoka tumefika Sokota ikasimamishwa tena na askari wa kike aliyekuepo pale kiwanda cha maji ya afya.Dereva "oya bonge shuka mwambie tushaunga uko nyuma" konda akaenda lakini akakawia ikabidi dereva nae ashuke akaenda akarudi na hasira "huyu dada njaa sana,sasa kila tukisimamishwa tutakua tunatoa hela" kuna mzee jirani yangu akamuuliza kwani gari inakosa gani? Dereva akajibu "unafikiri mzee gari inakosa yaani hawa trafki gari hata iwe mpya imetoka leo lazima uwape hela ukiwanyima njia utaihama watakavyokuandama kwahiyo imekua kama desturi,ngoja huku tunapoenda utakuta wengine watasimamisha na dau lao ni hilo hilo 2000-3000 kwa asubuhi".

Tulipofika buguruni sheli tukasimamishwa tena na matrafiki wa tatu wawili wanaume na mmoja wa kike kondakta akashuka tena kupeleka elfu 2,kitu cha ajabu wakisimamisha wala hawakagui gari wanazuga wanachukua chao kisha wanaondoka.

Jeshi la polisi usalama barabarani limeoza linahitaji kufumuliwa hii tabia imekithiri sana na sio mara moja kushuhudia,madereva na makonda wa daladala wengi hawana mshahara wanaamka mida mibaya kutafuta pesa lakini trafki badala kufanya kazi kwa ueledi wao wananyanyasa bila huruma wao wana mishahara na viposho lakini tamaa mbele.Na ninyi madereva na makondkta pia acheni unyonge na tabia hii ya kutoa hela hovyo hovyo hata kama huna kosa ni mnafuga ugonjwa,ukiwa na kosa kheri uandikiwe uichangie serikali kuliko kuwapa hao wafuga vigambi.
Yaonyesha Wewe ni Mgeni hapa Dar es Salaam ndiyo maana hili limekushagaza' mno. Sasa kwa Kukusaidia tu na kwa taarifa yako wenye 'Matatizo' wala siyo hao 'Trafiki' uliokutana nao huko kote ulikopita. Unavyoona wanaenda 'Resi' hivyo jua ya kwamba 'Mabosi' zao walioegesha tu 'Makende / Mapumbu' yao 'Ofisini' huku wakisoma 'Magazeti' na Kujipepea 'Feni' jioni wanataka 'Mgawo' wao unaoanzisha Tsh 75,000 mpaka Tsh 100,000 kutegemeana na Barabara uliyopo.

Yeye hapo kama akila sana basi 'Ganji' yake ni Tsh 15,000 hadi Tsh 25,000 tu. Na 'Trafiki' anayeshindwa 'Kukusanya' Pesa nyingi kwa 'Mabosi' zao hao walio 'Maofisini' huamishwa Mkoa na kupelekwa ama Tandahimba au Nachingwe huko tena 'Kijijni' kabisa ukapambane na 'Matrekta' ya Michanga au 'Mikokoteni' iliyobeba 'Kinyesi' cha Wanyama kinachotumika Mashambani. Kuna Mmoja 'alikamata' Gari 'akalikagua' na kukuta halina 'Kosa' na alipoona atakosa Hela kwa 'Makusudi' kabisa akamsingizia Dereva 'amemjambia' akiwa Kazini na Jamaa akampoza Tsh 5,000.
 
Habari ya asubuhi waungwana.

Ukweli hii tabia ya hawa askari wa barabarani kuchukua rushwa imekithiri sana tena wanachukua wazi wazi na bila kuogopa.Leo asubuhi nimepanda daladala kutoka Rang 3 naelekea vingunguti nikawa nimekaa siti ya mbele kabisa,tumetoka kituo kikuu cha Rang 3 tunafika Kizuiani trafki akasimamisha dereva akafyonya "aah hawa jamaa washaanza asubuhi asubuhi kutaka hela akamwita konda wake jina oya Bonge mpelekee elfu mbili yake tuondoke" na kweli konda akafanya hivyo.

Gari ikaondoka tumefika Sokota ikasimamishwa tena na askari wa kike aliyekuepo pale kiwanda cha maji ya afya.Dereva "oya bonge shuka mwambie tushaunga uko nyuma" konda akaenda lakini akakawia ikabidi dereva nae ashuke akaenda akarudi na hasira "huyu dada njaa sana,sasa kila tukisimamishwa tutakua tunatoa hela" kuna mzee jirani yangu akamuuliza kwani gari inakosa gani? Dereva akajibu "unafikiri mzee gari inakosa yaani hawa trafki gari hata iwe mpya imetoka leo lazima uwape hela ukiwanyima njia utaihama watakavyokuandama kwahiyo imekua kama desturi,ngoja huku tunapoenda utakuta wengine watasimamisha na dau lao ni hilo hilo 2000-3000 kwa asubuhi".

Tulipofika buguruni sheli tukasimamishwa tena na matrafiki wa tatu wawili wanaume na mmoja wa kike kondakta akashuka tena kupeleka elfu 2,kitu cha ajabu wakisimamisha wala hawakagui gari wanazuga wanachukua chao kisha wanaondoka.

Jeshi la polisi usalama barabarani limeoza linahitaji kufumuliwa hii tabia imekithiri sana na sio mara moja kushuhudia,madereva na makonda wa daladala wengi hawana mshahara wanaamka mida mibaya kutafuta pesa lakini trafki badala kufanya kazi kwa ueledi wao wananyanyasa bila huruma wao wana mishahara na viposho lakini tamaa mbele.Na ninyi madereva na makondkta pia acheni unyonge na tabia hii ya kutoa hela hovyo hovyo hata kama huna kosa ni mnafuga ugonjwa,ukiwa na kosa kheri uandikiwe uichangie serikali kuliko kuwapa hao wafuga vigambi.
Ukiwasikia madereva watakupotosha. Makosa haya ni dhahiri kwa madereva:-
1. Kuzidisha abiria
2. Kutofunga mkanda
3. Tyre mbovu
4. Kuendesha bila lesen
5. Mwendo kasi. Vibao vya 20kph anapita na 40kph
6. Madeni yaliyogota.

Sasa madereva hawataki kuwajibika, wanatumia hizo 2,000 kukwepa uwajibikaji. Kama yeye ni msafi, asitoe hiyo hela, akaguliwe alipishwe faini.

Kama wanaonewa, wawasakizie za takukuru. Si ipo?

Usiwaamini madereva
 
Wabongo mna mabichwa magumu balaaa.

Magufuli alishawaruhusu hao traffic kuchukua rushwa.

Alisema pesa wanayochukua ni ndogo tu ya kubrush viatu.

Sasa unakuta takataka kama ninyi mnaoimba kila siku Magufuli baba lao kakomesha rushwa eti mnalalamika huku mkijifanya kuwalaumu traffic wakati chanzo mnajifanya hamkioni.
Hii ni sababu nyingine ya kumuondoa Magufuli kwenye sanduku la kura.

Anatetea rushwa.
 
Habari ya asubuhi waungwana.

Ukweli hii tabia ya hawa askari wa barabarani kuchukua rushwa imekithiri sana tena wanachukua wazi wazi na bila kuogopa.Leo asubuhi nimepanda daladala kutoka Rang 3 naelekea vingunguti nikawa nimekaa siti ya mbele kabisa,tumetoka kituo kikuu cha Rang 3 tunafika Kizuiani trafki akasimamisha dereva akafyonya "aah hawa jamaa washaanza asubuhi asubuhi kutaka hela akamwita konda wake jina oya Bonge mpelekee elfu mbili yake tuondoke" na kweli konda akafanya hivyo.

Gari ikaondoka tumefika Sokota ikasimamishwa tena na askari wa kike aliyekuepo pale kiwanda cha maji ya afya.Dereva "oya bonge shuka mwambie tushaunga uko nyuma" konda akaenda lakini akakawia ikabidi dereva nae ashuke akaenda akarudi na hasira "huyu dada njaa sana,sasa kila tukisimamishwa tutakua tunatoa hela" kuna mzee jirani yangu akamuuliza kwani gari inakosa gani? Dereva akajibu "unafikiri mzee gari inakosa yaani hawa trafki gari hata iwe mpya imetoka leo lazima uwape hela ukiwanyima njia utaihama watakavyokuandama kwahiyo imekua kama desturi,ngoja huku tunapoenda utakuta wengine watasimamisha na dau lao ni hilo hilo 2000-3000 kwa asubuhi".

Tulipofika buguruni sheli tukasimamishwa tena na matrafiki wa tatu wawili wanaume na mmoja wa kike kondakta akashuka tena kupeleka elfu 2,kitu cha ajabu wakisimamisha wala hawakagui gari wanazuga wanachukua chao kisha wanaondoka.

Jeshi la polisi usalama barabarani limeoza linahitaji kufumuliwa hii tabia imekithiri sana na sio mara moja kushuhudia,madereva na makonda wa daladala wengi hawana mshahara wanaamka mida mibaya kutafuta pesa lakini trafki badala kufanya kazi kwa ueledi wao wananyanyasa bila huruma wao wana mishahara na viposho lakini tamaa mbele.Na ninyi madereva na makondkta pia acheni unyonge na tabia hii ya kutoa hela hovyo hovyo hata kama huna kosa ni mnafuga ugonjwa,ukiwa na kosa kheri uandikiwe uichangie serikali kuliko kuwapa hao wafuga vigambi.
Chukua ushahidi peleka TAKUKURU acha kulalamika
 
Naona tatizo hilo lipo dar zaidi mikoani sijaona hayo mambo ya daladala kuonewa
 
Nchi hii bado serikali aijAtangaza kuisha kwa corona daladala zinajaza abiria kwelikweli traffic wanatumia fursa iyo..ukipigwa mkono jiongeze mkuu..mAmbo madogo yanakuwa makubwa hutoamini
 
Back
Top Bottom