Askari wenye vyeti feki

Linawezekana lkn sio muhimu kwa sasa
 
Sababu serikali inanzotoa, kama kweli ndio hizo hazina mashiko hata chembe mkuu.Mbona wakifanya makosa mengine wanafukuzwa na hawasemi kwamba wataanzisha magenge ya unyang'anyi.Hawa wanapashwa kushuhulikiwa kama watumishi wengine!
 
Walimu na nurses sio watu?? Polisi ndio watuu
Ndivyo ulivyoelewa? Nilimaanisha,issue ya vyeti kwao ikifanyika, itakuwa na treatment tofauti ! Wanaweza kuondolewa katika "silent mode" watakaothibitika kugushi! Wengine kama uliotaja, tumeona wanaondolewa kwa "loud mode". Nahisi umenipata,G/night.
 
Wameishahakikiwa na waliofoji wameishafukuzwa.kuna lingine???

Au unataka majina yao???
Yamebandikwa vikosini kwao, wewe fika geti la kambi yoyote ya jeshi utakalopenda, mwambie mlinzi wa getini akuelekeze yalipo majina ya maaskari bashite, utaenda kujionea huko.
 
Acha kutudanganya wew ulienda huko kambini ukayakuta hayo majina?
 
Acha kutudanganya wew ulienda huko kambini ukayakuta hayo majina?
Kwani kama huamini si ni suala tu, kufanya nilivyoeleza hapo juu.

Mimi nimeenda na nikayaona, nikapata wasaa wa kuzungumza na jamaa hao ambao kwa wakati huo wengine walikuwa wanafungasha vitu tayari kwa kuondoka zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…