Askari wa usalama barabarani aliyekwaruzana na mke wa waziri apandishwa cheo

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
TRAFIKI-1.jpg

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Deogratius Mbango akiwa kazini kabla ya kupandishwa cheo.

Deogratius Mbango, askari wa kikosi cha usalama barabarani (trafiki) ambaye hivi karibuni alitukanwa na mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga baada ya kulikamata gari lake kwa kuvunja sheria za barabarani, hatimaye amepandishwa cheo ikiwa ni maagizo ya Rais Dk. John Magufuli.

Askari huyo ambaye alilikamata gari la mke wa waziri huyo baada ya kuvuka sehemu ya waendao kwa miguu eneo la Namanga jijini Dar es Salaam, amepandishwa hatua moja mbele, kutoka koplo hadi sajenti.

Kitendo hicho cha kulikamata gari hilo, bila kujali utambulisho na matusi ya mwanamke aliyedai kuwa mke wa waziri, kilimfanya Rais Magufuli kumsifu na kumuona kuwa jasiri kazini kwake, hivyo kuliagiza jeshi la Polisi kumpa promosheni mara moja.

Juzi Jumapili, gazeti la Uwazi lilimkuta trafiki huyo akiongoza magari maeneo ya Makumbusho katika lango la kuingilia daladala akiwa na cheo kipya cha usajenti.

Alipoulizwa kuhusu kuula huko, Mbango alikiri kutokea kwa jambo hilo na kumshukuru Mungu pamoja na uongozi wa Jeshi la Polisi kwa kumpandisha cheo.

Chanzo: UWAZI
 
Kuna baadhi ya watu walidai huyu polisi alivunja kanuni za polisi kwa kutoa siri za polisi na kwa maana hiyo hakupaswa kupandishwa cheo bali alipaswa kuadhibiwa kwa mujibu wa kanuni za polisi.

Kutumia kanuni bila hekima na busara wakati mwingine husababisha kutotenda haki.

Polisi wametumia hekima na busara katika kusimamia kanuni za polisi.

Kitendo alichokifanya huyu polisi kimetoa somo zuri kwa wale wanaodhani ni ‘’untouchable’’ na pia kimetoa motisha kikazi kwa wafanyakazi ambao husita kukabiliana na mazingira kama alivyokabiliana huyu polisi (courageous in the face of adversity).
 
Kwa wajuzi wa vyeo vya polisi hicho cheo alicho vaa ni koplo au sanjenti?
 
Anastahili Deo Mbango kupandishwa cheo kwani amedhihirisha kwa vitendo kauli mbiu ya Mhe. JPM ya hapa kazi tu. Kongole Deo Mbango, keep it up.
 
Kwa wajuzi wa vyeo vya polisi hicho cheo alicho vaa ni koplo au sanjenti?
Koplo
TRAFIKI-1.jpg

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Deogratius Mbango.

Deogratius Mbango, askari wa kikosi cha usalama barabarani (trafiki) ambaye hivi karibuni alitukanwa na mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga baada ya kulikamata gari lake kwa kuvunja sheria za barabarani, hatimaye amepandishwa cheo ikiwa ni maagizo ya Rais Dk. John Magufuli.

Askari huyo ambaye alilikamata gari la mke wa waziri huyo baada ya kuvuka sehemu ya waendao kwa miguu eneo la Namanga jijini Dar es Salaam, amepandishwa hatua moja mbele, kutoka koplo hadi sajenti.

Kitendo hicho cha kulikamata gari hilo, bila kujali utambulisho na matusi ya mwanamke aliyedai kuwa mke wa waziri, kilimfanya Rais Magufuli kumsifu na kumuona kuwa jasiri kazini kwake, hivyo kuliagiza jeshi la Polisi kumpa promosheni mara moja.

Juzi Jumapili, gazeti la Uwazi lilimkuta trafiki huyo akiongoza magari maeneo ya Makumbusho katika lango la kuingilia daladala akiwa na cheo kipya cha usajenti.

Alipoulizwa kuhusu kuula huko, Mbango alikiri kutokea kwa jambo hilo na kumshukuru Mungu pamoja na uongozi wa Jeshi la Polisi kwa kumpandisha cheo.

Chanzo: UWAZI
 
ninavyo jua kuwa vyeo vya vikosi na majeshi hupatikana kwa kwenda kozi sasa hv vyeo vya kupeana tu tena kwa kauli za wanasiasa kuna cku atakokea coplo kupandiswa mpaka kuwa IGP kwa kauli ya mtu
 
Sasa mbona mleta uzi kasema kapandishwa cheo kipya cha usanjenti?au hiyo picha ni ya zamani?
 
ninavyo jua kuwa vyeo vya vikosi na majeshi hupatikana kwa kwenda kozi sasa hv vyeo vya kupeana tu tena kwa kauli za wanasiasa kuna cku atakokea koplo kupandiswa mpaka kuwa IGP kwa kauli ya mtu

Kama enzi za copro fode sanko
 
Back
Top Bottom