Askari wa JKT ndani ya STK 3970 aporomosha matusi ya nguoni kulinda msafara wa kiongozi!

Ndio maana tunasema heshimu kila mtu hata kama humjui..What if huyo askari angekuwa anamtukana Kiongozi wake?? au baba yake?...Unaweza mtukana mtu au kumdharau na kesho ndo anakuwa msaada wako mkubwa na unabaki kuaibika...
 
Tena kijeshi kukutukana amekuheshimu wewe mjinga angeshuka akupe kichapo cha mbwa mwizi na hiyi dar ungeisikia kwny bomba yani kifaa cha Chadema ndo uvunje sheria tena wee unatakiwa ukamatwe mara moja!
 
Ndio maana tunasema heshimu kila mtu hata kama humjui..What if huyo askari angekuwa anamtukana Kiongozi wake?? au baba yake?...Unaweza mtukana mtu au kumdharau na kesho ndo anakuwa msaada wako mkubwa na unabaki kuaibika...
Asante kwa hiyo hekima, hao vijana wangejua tu wanaye mtukana kuwa ni Masopakyindi mwenye connections!
 
Hahaha...wadau wa huku wamenfurahisha aisee duh!
nway, pole masopakyindi, hakutakiwa kukutukana.
 
Last edited by a moderator:
Usitake kuhalalisha kutanua. Kwani hao wengine unajua wanaenda wapi. Kutanua ni kuwa selfish tu, kama kifaa ni muhimu si ungekodi helcopter? Mie mtu anaetanua unless amebeba mgonjwa mahututi sina hata habari nae, na kuliko anichomekee nora nimgonge nimlipe!

Nakubaliana na wewe sana, mijitu mingine huwa inajifanya inaharaka sana- halafu wakashaovataki wanakenua as if wao ndio wajanja kuliko wengine!!!
 
Ilikuwa mida ya saa nne usiku na nilikuwa katika mwendo kasi kidogo maana nimetoka mbali, nimesha tembea kilometa 750 na bado kama km 50 kufika Dar.

Mara naona mlolongo wa foleni inayoenda pole pole, na mimi nina kifaa cha mtambo wa utangazaji kinachotakiwa kufikishwa kwa mtaalam kabla ya saa tano usiku huu.

Kwa vile mwendo wangu ulikuwa kasi na hakuna on-coming traffic nikakanyaga mafuta na kifaa cha mjapani kika paa kwenda mbele.

Kufumba na kufumbua naona kumbe nimeyapita magari mawili moja lina maandishi ya sarufi ikiashiria ni kiongozi wa juu, naye akanipa ishara niridi nyuma nami nikatii.

Huyu wa pili, STK 3970 abiria akafungua dirisha, na akaporomosha matusi ambayo heshima yangu hainiruhusu kuyarudia mtandaoni.
Yalikuwa matusi ya nguoni, kama alivyosema mzee Ruksa.

Haya yote tametokea pale sehemu ya Ruvu darajani.

Pamoja na kunitia simanzi nimejiuliza maswali kadhaa. Nimepita JKT na najua heshima anayopaswa kuwa nayo askari lakini hii imenisikitsha.

Kweli nilikosea maana kwa nyuma ya msafara, tena usiku, hakuna ishara yoyote kuwa kuna msafara unaoendelea mbele, na mpaka naandika sijui ulikuwa msafara wa nani.

Kwa tunaoifahamu JKT huyo kijana ndani ya hilo gari STK 3970 hafai kuwa ndani ya Jeshi.
UPDATE
Nimefuatilia Sources MMJKT na wamethibitisha hilo si gari lao na halipo kwenye orodha ya magari yao ya kiraia.

Kunradhi JKT na mniwie radhi kwa hilo, lakini ndani ya gari hilo walikuwemo vijana waliovaa sare inayolingana.
Gari lilielekea usawa wa TAZARA.
Narudia tena kunradhi JKT.

Kwa nini ulikurupuka kuovertake? Hata kama una haraka kiasi gani, mazingira kama haya ndio huwa chanzo mojawapo cha ajali. Foleni inaenda polepole ulifikiri wote hawana haraka?

Just quoting your own statement.
 
Ndio maana tunasema heshimu kila mtu hata kama humjui..What if huyo askari angekuwa anamtukana Kiongozi wake?? au baba yake?...Unaweza mtukana mtu au kumdharau na kesho ndo anakuwa msaada wako mkubwa na unabaki kuaibika...

Mtu anaye overtake foleni inayoenda taratibu anaheshimu wengine? Labda kama alidhani ni msafara wa harusi! Halafu hilo eneo analosema kati ya daraja la reli na ruvu darajani pana kona inayoishia kwenye kijiji cha Ruvu Darajani amabapo mie hupenda kusimama kupata nyanya, vitunguu, viazi, bamia n.k. Hapafai kuovertake msafara! Think again, take action.
 
Tena kijeshi kukutukana amekuheshimu wewe mjinga angeshuka akupe kichapo cha mbwa mwizi na hiyi dar ungeisikia kwny bomba yani kifaa cha Chadema ndo uvunje sheria tena wee unatakiwa ukamatwe mara moja!

sheria ipi iliyovunjwa na huyu ndugu yetu?yeye huyo askari angetumia sheria ipi kutoa adhabu?maana ulivyopost ni kama unajua-hujuhi sheria kwa wakat mmoja,unasema huyu tusimvumilie maana kavunja sheria,hapo hapo unahalalisha askari kupga raia..duh kaz kweli kweli
 
Mimi naamini kwa nguvu sana yakuwa huu ni ule wakati wa kuangamia kwa kukosa maarifa, na imani kuwa wengi wetu hatufikiri tena bali tunajikumbusha tu. Mimi naona na haki ya kusema haya baada ya kufuatilia huu uzi toka mwanzo na mawazo mliyo changia, baadhi yenu ni magreat thinker kweli, wamewaonea huruma WANANUKUU kwa ugumu wa ujumbe kuuchambua na kuwapa ufupisho wa taarifa lakini wapi bwana! Imeshindikana kutafsiri na kutoa maoni mwendano na hali halisi kwa sasa na badae, NYIE WANANUKUU TOKENI NENDENI KWENYE MAJUKWAA YENU MFURAHIE KUNUKUU AKILINI MWENU MDA WOTE.
Narudi tena kuchangia.
Kwanza mtu yeyote ambaye anawaza kawaida kijamii angeanza na kuona ile ni kama jamii hii yetu ila wametuzidi kuishi kwa masharti na sheria katika mafunzo lkn nikama nyumba ya jirani. Embu fikiria kama watoto wanaropoka matusi makubwaaa pemben ya wakubwa zao si inamaana pengine hawa wakubwa wanayafanya mbele za hao wadogo. Mimi najua hawa jeshi linapokosa nidhamu, ueledi na utii hushinda hata jamii yetu iwapo dhaifu kwa maovu na makosa . Yule kakutukana ila ni kama katuma ujumbe kwetu wote yakuwa hakuna heshma tena kati yao na hata kati yao na sisi. Tabiri nini kimejengeka kati yao na sisi pia.., na kwa nini? Hivi pakitokea jambo latuitaji ushirika wa kupambania je tutaendana kweli? Kama hali itaendelea hivi itakua tabu sana, askari wa siku hizi wanamaneno sana! Sijui nawafikiriaje? We pesi wa shari? aaagh!! **pana! Wakoje? Tunaitawala sheria nasio kinyume. Unaelewa lakini?
Badae.
 
kwanza mtukachungulia tu dirishani akakutukana tayari usawataja JKT si uropokaji huu?
Pili kama dereve tena upo kasi, ukiona kitu kisicho cha kawaida na madereva wenzako wametulia wewe kwanini usijiuleze ni kwanini? Tulia chunguza ndio uchukue hatua ukishapata uhakika.
Huko pia ni kukurupuka. Hitimisho kukurupuka jumlisha kukurupuka unakuwa MKURUPUKAJI.
 
Pole sana mkuu, kama unataka kulijua hilo gari nenda Wizara ya ujenzi watakupa details kamili na ofisi linakotumika.
 
Tena kijeshi kukutukana amekuheshimu wewe mjinga angeshuka akupe kichapo cha mbwa mwizi na hiyi dar ungeisikia kwny bomba yani kifaa cha Chadema ndo uvunje sheria tena wee unatakiwa ukamatwe mara moja!

mmh zinakutosha kweli??
 
Kutokana na sheria za Usalama Barabarani ulikuwa hujafanya kosa lolote. Hii ni kwa sababu ukiangalia maelezo yako ilikuwa usiku na wewe ulikuwa unatoka nyuma kuyapita magari hayo mawili. Sheria ya Usalalama barabarani kifungu cha 43 kinasema:" Any person who drives a motor vehicle or trailer in such a way as to obstruct, hinder or impede the progress of an official motorcade , or who disobeys the instruction, conveyed orally, by signals or otherwise, of any police officer or other public officer in any vehicle escorting or forming part of the official mortocade, or of any police officer or other public officer on any road or other public place along which an official motorcade is passing or is about to pass, shall be guilty of an offence"(2) For the purposes of this section, "an official motorcade" means a motorcade of two or more motor vehicles escorted by or carrying a police officer to ensure that such motorcade has a safe and unimpeded journey to its destination.Kwa maelezo yako na vifungu vya sheria hapo juu ni dhahiri kuwa hakukuwa na motorcade hapo, hukudharau instructions oral, by signal or otherwise.Assuming kuwa ulikuwa umetenda, kitu ambacho tunasisitiza hukufnya kosa lolote, ulitakiwa uwe arressted kwa utaratibu uliowekwa kisheria na sio kutukanwa.
 
Back
Top Bottom